Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa muono wangu huyu bwana ndio anafaa kumrithi Kikwete, kwa Nchi yetu ilipofikia tunahitaji Rais mwenye msimamo na mbabe kama huyu jamaa, hatuhitaji tena mtu soft!!!!!
kufokafoka hovyo hakumaanishi kwamba yeye ni kiongozi bora na mara nyingi mtu mkali na mfokaji sana nyuma yake kuna kitu anaficha.kwa muono wangu huyu bwana ndio anafaa kumrithi kikwete, kwa nchi yetu ilipofikia tunahitaji rais mwenye msimamo na mbabe kama huyu jamaa, hatuhitaji tena mtu soft!!!!!
Yalikuwa ni maamuzi ya serikali nzima JK kipindi hicho akiwemo iweje umuhukumu yeye binafsi, yeye alitekeleza kama waziri mwenye dhamana! Au nawe ndo wale wanawahukumu kwa kuwaandika majina watendaji wa serikali badala ya kuishitaki serikali?
Si kila waziri anaweza kuwa raisi wa nchi. Mhe. Magufuli ana uthubuti wa kupewa majukumu na kuyasimamia na si vinginevyo. Kwa misimamo yake bora abaki kuwa waziri kwani zaidi ya hapo anaweza kuongoza nchi kidikteta.
Ninamkumbuka sana Magufuli kwa haya yafuatayo:
1. Alipokuwa Mifugo na Uvuvi Tanzanzia kwa mara ya kwanza ilikamata maharamia wa kigeni waliokuwa wamezoea kupora samaki wetu - alitoka na msemo wa bahari yetu siyo shamba la bibi. Kikubwa zaidi maharamia hao tena wa kigeni wamehukumiwa kifungo ndani ya ardhi ya Tanzania, waziri gani mwingine kafanya tukio kama hili?? Huyu kwangu ni shujaa!
2. Miaka ya 2000 alikamata magari ya serikali zaidi ya 21,000 ikiwemo mitambo na pikipiki. Magari enzi hizo yalikuwa yakiandikwa mpaka majina binafsi mfano nakumbuka moja liliandikwa Mwakajinga! Isitoshe zoezi hilo limerudiwa juzi kati ambapo magari zaidi ya 1000 yamealikuwa yanatumika vibaya kwa kuwa yalikuwa na namba za kiraia - kwangu mimi huyu ni kiongozi anayelinda mali za umma na kuhimiza matumizi sahihi ya mali za umma. Lakini maadui zake walioguswa na zoezi hili wanamshambulia, ni jukumu la wananchi wa kawaida kulijua hili!!
3. Amejenga barabara za lami zaidi ya kilometa 11000 na mpaka CCM wamekuwa vihelele wakimtumia kwenye majukwaa ili afanye presentation kuhusu mafanikio ktk ujenzi wa barabara tangu uhuru, lakini kibaya zaidi humohumo ndani ya CCM kuna kundi lipo kimkakati kumvuruga pengine aonekane si kitu!
4. Kumekuwa na malamiko ya barabara kujengwa chini ya kiwango, Magufuli kawakaba makandarasi wote na sasa barabara ya Singida kwenda Shelui, upande wa Sekenke inarudiwa na Mkandarasi kwa gharama zake zipatazo shilingi bilioni 15 na juzi kati tumeona makamu wa rais akifungua ile ya Mbagala ambapo Mkandarasi alirudia kwa hela zake, leo Magufuli anaoneka mbaya?
5. Alipokuwa wizara ya ardhi alianzisha mradi wa Viwanja 20,000 kule Kigamboni na kurudisha uwajibikaji wa wafanyakazi wa ardhi kiasi cha wananchi kusifia huduma za Wizara, leo hii mtu huyu anaonekana si lolote ndani ya CCM
6. Akiwa Ujenzi alizuia meli kubwa kusafirishwa kwa njia ya barabara ambapo ingeharibu barabara na hata meli hilo lisingeweza kupita ktk madaraja , lakini CCM hawaoni hili??
7. Kuhusu nyumba nakumbuka lilikuwa ni Azimio la Serikali nzima ambapo baraka zilitoka ktk baraza la mawaziri na yeye alikuwa na jukumu la kutekeleza tu! Sasa wana CCM hata siku moja hawatokei kumtetea hata kwa maneno mepesi tu, mtu huyu anaonekana kwao mbaya! Lakini katika hili nakumbuka hata Nyerere aliuza nyumba za serikali mfano pale Magomeni, Mwanza( Ghana Cottage), Tabora etc wana CCM wameshindwa kutumia mfano huu kumlinda kijana wao???
8. Humu jamvini Watu wanaandika Magufuli kawahi kuwa meneja TANROADS Morogoro ? Uvivu wa kufuatilia taarifa sahihi za viongozi - Hebu angalia CV za wabunge ktk tovuti ya bunge kama Magufuli aliwahi ajiliwa na Wizara ya Ujenzi kama mtumishi wa Umma?
9. Aliwahi chafuliwa kwa kuandikwa na gazeti moja kwa kipindi cha Miezi minane mfululizo, na baadae aliyefanya/tekeleza kazi hiyo kazawadiwa ukuu wa wilaya fulani- sisi siyo wajinga, tunajua mambo hayo!
10. Katika chaguzi za mwaka 2000 na 2005 alipita bila kupingwa jimboni kwake Chato na hata chaguzi za 1995 na 2010 ukiangalia matokeo utajua ni jinsi gani wananchi wake wanamhusudu lakini leo hii watu wanataka kuupoteza ukweli!
11. Lakini hata hivyo, mawaziri wenzake wanakubaliana naye jinsi anavyofanya kazi bila kuogopa mtu!
12. Ndiye aliyeanzisha mfumo wa kujenga barabara kwa kutumia hela zetu za ndani bila kutegemea wafadhiri na alianzisha model ya design and build mpaka wenzetu jirani Kenya wakaja kuiga kipindi hicho Raila Odinga akiwa waziri wa barabara wa Kenya!
13. Ni waziri pekee aliyekaa Wizara ya ujenzi kwa muda mrefu penye vishawishi vya rushwa bila shutuma yeyote ile
WITO WANGU KWA MHESHIMIWA MAGUFULI:
1. Wanaokuchafua sio sisi CHADEMA bali ni wana CCM wenzako ambao kila kukicha wanakuogopa kwa vile unakubalika na wananchi walio wengi!
2. Nakushauri jiunge na CHADEMA ili uje kushirikiana na Dr . Slaa tayari kwa ukombozi wa taifa hili
3. NAKUSISITIZA MHESHIMIWA MAGUFULI NI WAKATI WAKO SASA KUHAMIA CHADEMA
Unaonekana ulizaliwa kabla ya siku zako hazijatimia - kwa akili ya kawaida tu tembelea tovuti ya TANROADS utaona barabara zinazofadhiliwa na donors na zile zinazotumia hela za serikali, utagundua zaidi ya asilimia 70 ya barabara zote zinajengwa kwa hela za serikali, serikali ilishaacha ule mtindo wa kusubiria wafadhiri ndo ijenge barabara na CNN juzi juzi wametangaza Tanzania ni moja Kati ya nchi tano zinzoinvest heavily kwenye infrastructure za barabara na ni ya kwanza kwa Africa Mashariki!
Umeniboa sana uliposema tuna asilimia kumi tu katika kuchangia Ujenzi wa barabara, ni uongo na upotoshaji wa kutupa! Tena huyo Magufuli ndo alilazimisha kwanza kujanga barabara kwa kutumia fedha zetu za ndani iweje leo unalazimisha kusahau historia au umetumwa?
Slaa hata akihamia CCM hatakuja kuwa rais wa Tanzania
Ukimjua utakuwa wa kwanza Kumpinga kwa Nguvu zote, Binafsi hata angegombea na nani siwezi mpa kura yangu[
NI KWELI SIJUI HUWA WANAMPENDEA NINI
ni mbabbe asiye na huruma ......huwezi chekelea kuwabomolea maskini katika nchi ambayo hakuna sera /haitekezwi .....asiliamia 90 ya makazi hayajapimwa ni kosa la wamiliki wa nyumba au serikalihebu endeleeni kumchambua maana sie wengine huwa tunamsikia tu kwenye ufunguzi wa ujenzi wa mabarabara.
Dodoma yote pale mjini ni nyanza, haka kakampuni kana mlio wa mbu, anaekajua atumwagieKuna kakipande ka barabara fulani kako mwanza palipoishia barabara ya Green Acre. Kila mwezi Nyanza toad wako aple wanajenga toka mwaka 2005. Unajua ni project ya nani? Mi mwenye nisingempa kura yangu bora nipigie jiwe.
Hivi wewe ulielewa nilichokiandika au ulipokuwa unasoma ulikuwa umelewa???? Unajua hesabu wewe?? Hivi miradi 29 kati ya 68 ndio 70%, what have you been drinking sir??
Hebu nionyeshe nilipoandika ulichodai kuwa nimeandika hapo kwenye RED. Uwe unasoma na kuelewa, au na wewe ni "educated illiterate"???
Kwenye RED; that is precisely kinachosemwa na watu tunaomfahamu Magufuli kwa kufanyakaz nae. Usichokijua wewe (na wenye mtazamo wako kuhusu Magufuli) ni kuwa huyu bwana huwa anafanya mambo bila kufikiri kitakachotokea baadae. Kwa taarifa yako, Mwakajinga alikopeshwa hilo gari (kuna kipindi serikali iliwakopesha maofisa stahili magari ambayo yalikuwa yanamilikiwa na serikali na mkopaji hakurushusiwa kubadilisha namba hadi amalize kulipa). Udhalilishwaji huo kwa Mwakajinga na wengine kuliigharimu serikali maana wote waliochukua hatua walilipwa fidia. Waziri makini angejua hayo kabla hajayatangaza hadharani.
Umem-credit Magufuli na ujenzi wa km 11000 za barabara, ila usichokijua ni kuwa barabara hizo zote zimejengwa kwa fedha za wafadhili au mikopo ya benki ya dunia (na usimamizi wake hufanywa na donors wenyewe). Na process ya kupata fedha za kujenga hizo barabara zilianza na kujadiliwa kwa proposals za serikali ya awamu ya kwanza na ya pili. Unamsifia aliekabidhiwa barabara iliyokamilika wakati aliefanya kazi ya kujenga si yeye!
Kwa kifupi; huo "uchapakazi" wa Magufuli ni wa media tu!
Una agenda yako ya Siri, Magufuli jembe japo hajastahili kuwa Rais. Au na wewe (Jamaa yako) ni mmoja wa waliokuwa wameregister magari ya umma kwa jina binafsi.
Nikibishana na wewe nitaonekana pia sina akili, wewe ni wa kukuacha mwenye kuelewa atafuatilia na tajua ukweli upo wapi!