kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Nilimsikia Mh. Lissu kwenye moja ya majibu yake mahakamani akisema na kukubali kuwa yeye ni mtu anaehishimika sana ndani na nje ya nchi kiasi cha jumuiya za kimataifa kumtambua na kumheshimisha kwa kumpatia tuzo.
Kama Lissu mwenyewewe anakili kuwa yeye ni mtu muhimu na anaekubalika nchini na kimataifa kwa kiasi cha kupewa tuzo basi lazima akiri pia kuwa maneno aliyosema kwenye hotuba yake ya no reforms no election, tutazuia uchaguzi , tutaasi na tutakinukisha vibaya sana Oct29 yaliwashawishi watu kufanya vurugu October 29 na baada ya Oct29 kwakuwa yalitolewa na mtu anaeheshimika sana ndani na nje ya nchi.
Watu wanaoheshimika sana kwenye jamii ni watu ambao hawapuuzwi kwenye kila kitu. Watu watamtii na watamuiga hata kuvaa, kusema, kutembea, kula na kunywa. Wataheshimu na kutekeleza bila kusita kile wanachoagizwa na kusemwa na mtu wanaemheshimu.
Sifa hii ya kuheshimika aliyojipa kwenye utetezi wake inaweza kumtia matatani kwenye kuwashawishi wale wanaomtii, mheshimu na muamini kufanya vurugu zile zilizotokea siku ile. Na kama uchaguzi wa Kikatiba ukivurugwa maana yake umevunja Katiba, umehujumu fedha zote zilizotumika kuandaa uchaguzi, ingesababisha viongozi walioko madarakani kuendelea kubaki madarakani kinyume na katiba au nchi ingebaki bila na Rais, wabunge na madiwani halali kwa mujibu wa katiba.
Ningekuwa mimi ningesema kuwa mimi ni raia tu wa kawaida kwenye jamii nisieweza kumshawishi mtu yeyoyote kufanya kama walichofanya.
Mashahidi wake hawasaidii kumtoa Lissu kwenye ukweli kwamba alisambaza ujumbe wa no reforms no election na tutakwenda kuzuia uchaguzi kwakuwa yeye ndiye mkuu wa chama na hakukerwa na uwepo wa vyombo vya habari kwenye mkutano ambao yeye alikuwa mzungumzaji mkuu. Kama angekuwa hataki uwepo wa vyombo vya habari kwenye mkutano angefanya kati ya mambo yafuatayo:
1. Kuvifukuza kwenye mkutano
2. Kunyamaza/kugoma kuhutubia hadi viondoke
3. Angeahirisha mkutano au mada
4. Angewachukulia hatua waliovialika.
Common sense na common practice kila anaealika vyombo vya habari anataka bahari yake/jambo lake lisambazwe kuwafikia watu wwngi zaidi kupitia kalamu, sauti na picha (mass communication)