Vawulence
JF-Expert Member
- Jan 4, 2009
- 1,982
- 2,338
Kavulana ndiyo umeandika upuuzi gani? Kesi ya Lissu haina tofauti na wale wanaotumia mstari mmoja wa Biblia kuhalalisha uovu wao.Nilimsikia Mh. Lissu kwenye moja ya majibu yake mahakamani ni kusema na kukubali kuwa yeye ni mtu anaehishima sana ndani na nje ya nchi kiasi cha jumuiya za kimataifa kumtambua na kumheshimisha kwa kumpatia tuzo.
Kama Lissu mwenyewewe anakili kuwa yeye ni mtu muhimu na anaekubalika nchini na kimataifa kwa kiasi cha kupewa tuzo basi lazima akili pia kuwa maneno aliyosema kwenye hotuba yake ya no reforms no election, tutazuia uchaguzi , tutaasi na tutakinukisha vibaya sana Oct29 yaliwashawishi watu kufanya vurugu October 29 na baada ya Oct29 kwakuwa yalitolewa na mtu anaeheshimika sana ndani na nje ya nchi.
Watu wanaoheshimika sana kwenye jamii ni watu ambao hawapuuzwi kwenye kila kitu. Watu watamtii, watamuiga hata kuvaa, kusema, kutembea hata kula na kunywa.
Sifa hii ya kuheshimika aliyojipa kwenye utetezi wake inaweza kumtia matatani kwenye kuwashawishi wale wanaomtii, mheshimu na muamini kufanya vurugu zile zilizotokea siku ile. Na kama uchaguzi wa Kikatiba ukivurugwa maana yake umevunja Katiba, umehujumu fedha zote zilizotumika kuandaa uchaguzi, ingesababisha viongozi walioko madarakani kuendelea kubaki madarakani kinyume na katiba au nchi ingebaki bila na Rais, wabunge na madiwani halali kwa mujibu wa katiba.
Ningekuwa mimi ningesema kuwa mimi ni raia tu wa kawaida kwenye jamii nisieweza kumshawishi mtu yeyoyote kufanya kama walichofanya.
Hoja ya Lissu ni kuwa inakuwaje aliongea masaa zaidi ya 3 lakini wakachukua sentensi moja tu?