Mheshiwa Lissu kajitetea vibaya kwenye kipengele cha heshima kubwa aliyonayo kimataifa

Mheshiwa Lissu kajitetea vibaya kwenye kipengele cha heshima kubwa aliyonayo kimataifa

Soma threads zangu kuhusu Lissu kabla ya No reforms no election na kususia kutia saini kanuni za uchaguzi. Mimi simchukii mtanzania mwenzangu kwakuwa nimeshavuka huko. Hata sasa simchukii ila namchukia mtu yeyote anaetumia jinsia ya Rais Samia kumdharau na kumchukia bila sababu.

Kwa mahaba ya Samia kwa Lissu hakustahili kusumbuliwa na Lissu kama hivi anavyomsumbua na kumbeza.

Hata wewe mheshimiwa utakuwa hutendi haki kama utamfurahia mtu yeyote ambae anadai haki kwa kutuharibia miundombinu yetu inayotudumia ambayo iliyotugharimu sisi wote kuijenga
Taifa halipigi hatua kisa mtu anaposhindwa kuwa mkweli kwa mwenzie kisa kulinda wema uliowahi kutendewa zamani...hoja za lissu kuhusu kususia uchaguzi wewe unazionaje?
 
Nilimsikia Mh. Lissu kwenye moja ya majibu yake mahakamani akisema na kukubali kuwa yeye ni mtu anaehishimika sana ndani na nje ya nchi kiasi cha jumuiya za kimataifa kumtambua na kumheshimisha kwa kumpatia tuzo.

Kama Lissu mwenyewewe anakili kuwa yeye ni mtu muhimu na anaekubalika nchini na kimataifa kwa kiasi cha kupewa tuzo basi lazima akili pia kuwa maneno aliyosema kwenye hotuba yake ya no reforms no election, tutazuia uchaguzi , tutaasi na tutakinukisha vibaya sana Oct29 yaliwashawishi watu kufanya vurugu October 29 na baada ya Oct29 kwakuwa yalitolewa na mtu anaeheshimika sana ndani na nje ya nchi.

Watu wanaoheshimika sana kwenye jamii ni watu ambao hawapuuzwi kwenye kila kitu. Watu watamtii na watamuiga hata kuvaa, kusema, kutembea, kula na kunywa. Wataheshimu na kutekeleza bila kusita kile wanachoagizwa na kusemwa na mtu wanaemheshimu.

Sifa hii ya kuheshimika aliyojipa kwenye utetezi wake inaweza kumtia matatani kwenye kuwashawishi wale wanaomtii, mheshimu na muamini kufanya vurugu zile zilizotokea siku ile. Na kama uchaguzi wa Kikatiba ukivurugwa maana yake umevunja Katiba, umehujumu fedha zote zilizotumika kuandaa uchaguzi, ingesababisha viongozi walioko madarakani kuendelea kubaki madarakani kinyume na katiba au nchi ingebaki bila na Rais, wabunge na madiwani halali kwa mujibu wa katiba.

Ningekuwa mimi ningesema kuwa mimi ni raia tu wa kawaida kwenye jamii nisieweza kumshawishi mtu yeyoyote kufanya kama walichofanya.
Sasa kesi iliyoko mahakamani na ya Okt.29 vinauhusiano gani mkuu
 
Lakini amekubali mahakamani kuwa amesema no reforms no election, tutazuia uchaguzi, tutakinukisha na tutaasi. Kama yeye ni mtu maarufu na anaeheshimika sana bila shaka wafuasi wake hawakumpuuza bosi wao, hivyo walikwenda kuchoma masanduku ya kura ili kuzuia uchaguzi kwakuwa hizo reforms alizotaka zifanywe ili uchaguzi ufanyike hazikufanyiwa, na wala yeye hakwenda mahakamani kudai zifanyike kabla ya uchaguzi
Alisema anazuia uchaguzi, hivyo alizuia? Kumbe hakukufanyika uchaguzi kura zilichomwa sasa hizo 98% za ushindi zilipatikaneje?
 
kwa yaliyotokea octoba29 lissu hakuwepo uraiani mlishamfunga tayari hivyo mungu kumuepusha na hila zenu mbaya itoshe kusema Mungu huwa yuko mbele ya muda siku zote kama tu mna mu implicate kwa hayo wakati alikuwa ndani vipi kama angekuwa nje? si ajabu hata mngemuuwa tena kwa mara ya pili.
Hakika yangemwua ,Mungu alimwepusha na lawama hizi hakika
 
Lakini amekubali mahakamani kuwa amesema no reforms no election, tutazuia uchaguzi, tutakinukisha na tutaasi. Kama yeye ni mtu maarufu na anaeheshimika sana bila shaka wafuasi wake hawakumpuuza bosi wao, hivyo walikwenda kuchoma masanduku ya kura ili kuzuia uchaguzi kwakuwa hizo reforms alizotaka zifanywe ili uchaguzi ufanyike hazikufanyiwa, na wala yeye hakwenda mahakamani kudai zifanyike kabla ya uchaguzi
Sasa huo ni uhaini? Kama ni uhaini? Uhaini ni nini?
 
Kuna unachoelewa basi wewe upo ili mradi unapumua! matumizi mabaya ya oksijeni
Umemsikia shahidi Mnyika alivyovorunda mahakamani? Anaulizwa kama yuko raia ambae anaweza kuzuia uchaguzi wa kikatiba usifanyike, akajibu hakuna, isipokuwa kama uchaguzi huo sio huru na haki. Hebu angalia hapa, ni nani anapaswa kutamka kuwa uchaguzi sio huru na wahaki wakati hawakupeleka shauri lao mahakamani kuupinga uchaguzi huo ambao haukuwa huru na wa haki kwao? Je, namna uchaguzi ulivyofanyika ulivunja kifungu chochote cha Katiba ya 1977 au sheria nyingine? Je, chadema walikuwa na mamlaka ya kutangaza uchaguzi sio huru na haki? na Je, walikuwa na uhalali wa kushawishi watanzania wasusie uchaguzi wa kikatiba? Na je, walikuwa wanatambua matokeo ya kuuzuia uchaguzi usifanyike? Je, ni nchi gani chama na raia walishawahi kuzuia uchaguzi usifanyike kwa njia za kidemokrasia?
 
LIssu amesema mtu mmoja hawezi kuitishia serikali. Kosa lake hapa ni kule kutumia maneno "...tuta..."kwenda kuzuia, tutakwenda kukinukisha, tutakwenda kuzuia.... maana yake hakuwa peke yake, alimaanisha wako zaidi ya mtu mmoja watakaokwenda kuuvuruga uchaguzi. Na kweli vurugu zilihusisha watu wengi....
 
dah ,hapo anagonga nyundo anatoa hkumu aliyoambiwa
Mashahidi wa lissu wanasema uongo. Katibu hawezi kuitisha mkutano au kikao bila kuagizwa au kushauriana kwanza na m/kiti wake.
dah ,hapo anagonga nyundo anatoa hkumu aliyoambiwa
Kapanga njama za kukinukisha. Nadhani utetezi wake ungekuwa na maana kama Oct29 kusingetokea vurugu za kuvuruga uchaguzi na kuharibu mali ya umma. Aliitishia serikali ambayo ina jukumu la kulinda uchaguzi, amani, watu na mali zao na vyombo vinavyolinda amani, uchaguzi, watu na mali zao viko chini ya Rais. Hivyo automatically atakuwa amemtishia Rais na Amirijeshi Mkuu.
 
Sasa huo ni uhaini? Kama ni uhaini? Uhaini ni nini?
Hata siwaelewi hakiyanani!! Kwani tunabishana kuwa sio akina Lissu waliochoma moto mali za watu na zile za umma? Mnabisha kuwa hawakutaka kuipindua serikali?. Au wamechoma lakini mnatafuta njia ya kukwepa adhabu?

Kama mnawaza hivyo basi hamko sawasawa kila mahali.
 
Alichokisema kabla ya kukamatwa kilichochea kilichotokea Oct29, hasa kutokana na heshima aliyonayo kitaifa na kimataifa kama alivyokiri mwenyewe kuwa heshima hiyo anayo kubwa.
je heshima yako kwenye jamii inatosha kushawishi watu wafanye maovu au heshima hiyo ni kikwazo kwake kufanya maovu km uhaini.
 
Mashahidi wa lissu wanasema uongo. Katibu hawezi kuitisha mkutano au kikao bila kuagizwa au kushauriana kwanza na m/kiti wake.

Kapanga njama za kukinukisha. Nadhani utetezi wake ungekuwa na maana kama Oct29 kusingetokea vurugu za kuvuruga uchaguzi na kuharibu mali ya umma. Aliitishia serikali ambayo ina jukumu la kulinda uchaguzi, amani, watu na mali zao na vyombo vinavyolinda amani, uchaguzi, watu na mali zao viko chini ya Rais. Hivyo automatically atakuwa amemtishia Rais na Amirijeshi Mkuu.
je matamko tu yanatosha kisheria kuonyesha nia thabiti ya kosa.
 
Mleta mada, pole sana, umedhihirisha uwezo mdogo wa akili.

Kwanza kufanya uasi kwa jambo inalojua ni batili, siyo kosa. Na kamwe haliwezi kua ni uhaini. Hata wewe, kutiba unakuelekeza kuasi chochote kilicho kinyume cha katiba, mara unapogunfua. Lisu ameeleza vizuri sana. Katiba yeti inatamka kuwa kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki, Lisu ameeleza na kutoa vithibitisho mbalimbali kuwa chaguzi zetu siyo huru na za haki. Hivyo wananchi watii katiba, walistahili kufanya uasi dhidi ya mfumo unaodanya uchaguzi usiwe huru na wa haki. Kiuhalisia ni kwamba walipridhia kushiriki uchaguzi wa namna hiyo, huku wakijua, kwa mujibu wa katiba yetu, ni wahalifu. Vithibitisho vya kuwa mifumo ya ucjaguzi wa Tanzania haina uwezo wa kuufanya uchaguzi huru na wa haki, ni pamoja na taarifa za tume mbalimbali kuanzia ile ya Jaji Nyalali, na wengine wengi, na taarifa za taasisi mbalimbali za watazamaji wa kimataifa. Na hayo yote Lisu ameyaeleza na kuyafafanua vizuri sana.

Ni mwendawazimu pekee anayeweza kusema kuwa neno kukinukisha ni uhalifu. Nenda kasome hata kamusi ya Kiswahili ujue maana ya kunuka, kunukisha.
Kwa tafsiri rahisi, kama unafanya hadaa, na unaheshimika na jamii, mtu anayekuja kuanika uovu wako, hapo amekunukisha, kwa sababu anawafanya watu waujue uhalisia wako, kuwa wewe unafanya hadaa, na baada ya hapo hutaheshimika, utanuka.

Mwendawazimu pekee ndiye anaweza hata kufikiria kuwa kusema nitakinukisha, ni kosa la jinai.
Mahakama zenye uadilifu lazima zitete vitendo vya kimaadili na kufuata sheria iwe kwenye uchaguzi,serikalini na popote kwa maana ya Justice. Na hicho ndicho kinachotegemewa kwenye Sura ya Judgement. Ni lazima kupima context -mukhtadha ya matamko ya Lissu kufikia hukumu iliyo bora kwa maslahi mapana ya nchi,taifa na dunia kwa ujumla.
 
Hata siwaelewi hakiyanani!! Kwani tunabishana kuwa sio akina Lissu waliochoma moto mali za watu na zile za umma? Mnabisha kuwa hawakutaka kuipindua serikali?. Au wamechoma lakini mnatafuta njia ya kukwepa adhabu?

Kama mnawaza hivyo basi hamko sawasawa kila mahali.
Ulisikiliza hotuba ya Chande ?

Nanukuu ...' tume imebaini waliokamatwa katika vurugu zile walikuwa
-vijana waliokuwa wakitaka mabadiliko ya kimfumo hasa Katiba Mpya
-Wanasiasa waliokatwa katika kugombea nafasi mbalimbali katika vyama vyao
-vijana waliokosa ajira baada ya Kukaa muda mrefu nyumbani baada ya kumaliza vyuo
-Madai mbalimbali ambayo Serikali imekaa kimya bila kuyafanyia kazi
-Baadhi ya waumini ambao walidai kutotendewa haki..na nyumba zao za Ibada kufungwa na kuzingirwa na Polisi

Nimemaliza...

Sasa hao waliotajwa na Chande ni watu wa Lissu wote ?

Nakupa na nyingine....
Tume ilibaini kauli mbiu zilizochochea vurugu...

+ No reforms no Election
+October tunatiki
+October tunatoka

Ukiangalia hapo tayari ni kauli za CCM na CHADEMA

Pia hii kesi ya Lissu sijui kutishia Serikali au sijui Vurugu, uasi au kuzuia Uchaguzi havipo katika viini vya Uhaini

Bado watu wengi hawajui uhaini ni Nini...

Kwa kifupi uhaini Duniani kote viini vyake ni
- Njama/ Mipango ya Siri ya kupindua Serikali kwa njia haramu

- Kupanga kudhuru Rais aliyepo madarakani

-Kutafuta fedha, silaha na watu hasa wenye mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya Mipango hiyo
 
je heshima yako kwenye jamii inatosha kushawishi watu wafanye maovu au heshima hiyo ni kikwazo kwake kufanya maovu km uhaini.
Heshima yake ndani na nje ya mipaka ni hatari sana kwa usalama wa taifa. Heshima yake ilishawishi watu nchini wafanye kama vilevile alivyotamka ifanyike OCT29. Heshima yake kimataifa iliwashawishi watu wa jumuiya kama Tabo Mbeki, EU, Jumuiya ya madola watamke maneno mengi kuhusu uchaguzi wetu. Maneno ambayo yanamuunga mkono Lissu.

Hii ni kuonyesha kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya tamko la Lissu na kilichotokea oct29 (p-value is <0.0001)
 
wewe utakua wakili wa serikali
 
wewe utakua wakili wa serikali
Nasikia watu wameshaanza kususa kwenda mahakamani, idadi imepungua mno. Huyu Golugwa ndio bure kabisa kumbe. Ni mweupe pee kichwani. Kumbe tujifunze kuacha kuropoka tu bila kuwa na ushahidi wa kuona sisi wenyewe. Tuachane na habari za kusikiasikia kama zile za vifuu huko Tanga vinaongea kama ukivikanyaga makusudi.

Za kuambiwa changanya na zako

Hebu ona, kuna katibu gani wa taasisi yoyote anaeweza kuitisha mkutano au kikao bila kuagizwa na mwenyekiti wake? Lissu ni mwanasheria nguli lakini mganga hajigangi.
 
Back
Top Bottom