Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Kwa akili yangu hii sitajiua kwa chochote, nikifanya hivyo itakuwa nimepatwa tatizo la akili.
Ukitembea namwanaume bila condom ni sawa sawa na kujiua, nahisi umeshajiua mara nyingi tuu
 
Watu wakija humu kuomba ushauri wanaambulia kebehi na mizaha tu, matokeo ndo haya.
ok acha vijana wajimalize kama wanaona dawa ya kukwepa kuishi bila ajira hapa duniani ndio hiyo ila kiukweli ikinitokea mimi tamaa ya kuyakatisha maisha yangu sitafanya kama alivyofanya huyo dogo bali nitamuondoa mt...............kama huko ...........
 
Pole sana kijana...pumzika kwa amani.
Naona faraja kutoka kwa watu wako wa karibu na ulikua na matarajio ya hali ya juu ilhali u mdogo..miaka 25 tu..
Afadhali ulibahatika kuwa na hiyo degree..sisi wengine hatuijui

Ndugu wana jf mnapojikuta katika wakati mgumu jaribu kujilinganisha na mwingine halafu jiulize ningekua kama yule ninfefanyaje?mimi tu niko hivi nina challenge hizi na hizi nataka kujiua lakini mbona yule hana wazo la kujiua na yuko happy na situation yake?
Itakusaidia believe me
 
Kuna watu nadhani hawajawahi pigwa na maisha... Wao wanajua kula na kulala tu! Hawajawahi pata majukumu yanayozidi uwezo na huna kituu aisee... Acha mkuu


Hasa hasa huyu anaejiita demi, utakuta ni slay queen anaekula na kujamba kwa wazazi wake..akishatoa kunduchi kwa madanga yake mawili na kupewa hela ya kula bhaaas maisha kwake anayaona ni marahisi rikiboy
 
Hasa hasa huyu anaejiita demi, utakuta ni slay queen anaekula na kujamba kwa wazazi wake..akishatoa kunduchi kwa madanga yake mawili na kupewa hela ya kula bhaaas maisha kwake anayaona ni marahisi rikiboy
[emoji23][emoji23][emoji23]Huwezi sikia mwanamke amejinyonga kisa maisha magumu...!! Wanaume ndo kila siku sababu sio mapenzi tuu.. Mwanamke ulie nae akuchanganye.. kazi zinazingua..madeni kila konaa.. Familia yako wewe ndo tegemeo aiseee... Kuumbwa mwanaume means kuwa mwanajeshi..Vitani kila mudaa
 
Jaribu kuwa muelewa... tatizo sio bei ya pombe nimejiuliza tu kwa nini mtu uwe mlevi kisa huna kazi? Unawezaje kupata hata hiyo kazi wakati unajiharibu kwa ulevi? Kwa hiyo wewe unaona ilikuwa sawa anywe pombe sababu hana kazi na sababu pombe ni shilingi 500?
KwanzA Nani kakwambia kunywa pombe ni kujiharibu ??.

Mbona kuna watu wanakunywa pombe miaka nenda rudi na wako imara?? Acheni ujinga msijifiche kwenye sababu nyepesi.


Wapeni vijana ajira na wawezesheni wapewe mikopo kwenye taasisi za kifedha watimize ndoto zao, nchi nyingi zilizoendelea kwa kutojua hawawezi kuajiri kila mtu wanawasaidia vijana kwa model hiyo na sio Sababu uchwara kama zako
 
Imeandikwa Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.Kuna umuhimu kuwa na Somo la ujasiriamali kama mmojawapo ya Core subject kwenye syllabus zetu ngazi zote za elimu.
 
KwanzA Nani kakwambia kunywa pombe ni kujiharibu ??.

Mbona kuna watu wanakunywa pombe miaka nenda rudi na wako imara?? Acheni ujinga msijifiche kwenye sababu nyepesi.


Wapeni vijana ajira na wawezesheni wapewe mikopo kwenye taasisi za kifedha watimize ndoto zao, nchi nyingi zilizoendelea kwa kutojua hawawezi kuajiri kila mtu wanawasaidia vijana kwa model hiyo na sio Sababu uchwara kama zako
Tatizo lako umejawa na Negativity kichwani Mwako. Fanya utafiti utakuja Gundua kuwa vijana wengi wa Kitanzania sio tu kwamba hawaajiriki bali hata kukopesheka hawakopesheki pia..Mtu ambae kama wewe ambaye hutaki kuamini kuwa ulevi ni tatizo ni tatizo pia.
 
Ally (25), mkazi wa Kiloleli wilayani Ilemela jijini hapa anayedaiwa kuwa na elimu ya chuo kikuu, amejirusha katika jengo la la Rocky City Mall na kufariki dunia.

Imeelezwa kuwa Musa alichukua uamuzi huo kutokana na kuwa na msongo wa mawazo, kukosa kazi.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Desemba 21, 2018 kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Advera Bulimba amesema tukio hilo limetokea leo saa saba mchana.

Bulimba amesema kijana huyo alionekana akiwa amelewa kupita kiasi na tangu Desemba 16, 2018 na alikamatwa na kuwekwa kituo cha polisi Kirumba, kilevi kilipopungua aliachiwa.

Amesema katika uchunguzi wa awali marehemu alibainisha kuwa alikuwa na msongo wa mawazo kwa sababu ya kukosa kazi licha ya kuwa na elimu ya juu.

Bulimba amesema baada ya polisi kumuachia alikwenda kunywa tena pombe na baadaye kujirusha kutoka ghorofa ya tatu na kukutwa na pombe kali na ugoro.

“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa kijana huyo amesema amejiingiza kwenye ulevi na asilaumiwe mtu yeyote.

Amesema amechukua uamuzi huo yeye binafsi, pia akidai yeye ni masikini hana baba wala mama,” amesema Bulimba.

Amesema mwili umehifadhiwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi licha ya kutotaja jina la hospitali hiyo.

Bulimba amesema, maandishi aliyokutwa nayo marehemu yalisomeka kwamba “yeye ana shahada sayansi ya kompyuta aliyoipata Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).”

Chanzo:Mwananchi.

Police wamesomba Picha zimekataa kuupload. Ila nimeattach kwenye comment no 6 na 7.
Ajira ajira ajira
 
R.I.P ndugu japo huna wazazi ila hukupaswa kufanya hivyo
Tupo wengi tu tena wenye umri mkubwa kuliko ww na tunasuffer tokea tumemaliza 2015
Ila tumepotezea hizo elimu na kuziba masikio maana ukifanya kazi ngum kama kwenye ubebaji zege wanaadam waliokosa mtazamo chanya watakusema kuwa elimu yako ni bure
Ukikaa kitaa utaambiwa unachagua kazi
Kikubwa kama huna connection kwa wahanga wenzangu ni kukomaa tu bila kujali maneno ya binaadam


Naumia sana ninaposikia taarfa kama hizi maana nikiwa kama muhanga wa ukosefu wa ajira huwa naumia sana ila nilishaweza kujicontrol na naishi maisha yenye furaha tu japo kuna siku nikaangalia makabrasha yote ya BAEd huwa naumia mno
Mungu atusimamie na atuongoze na atuepushe na mawazo yaliyopitiliza
 
Back
Top Bottom