Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Alitakiwa kupelekwa kwenye psychological and counselling centres kwa msaada zaidi akitokea Polisi ili kumsaidia.
 
Mim nikisikia mtu kajiua kwa sababu yoyote ile siwezi kumshangaa sana wala kumjudge kama mpuuzi coz I know everything controlled by hormone
 
Ally (25), mkazi wa Kiloleli wilayani Ilemela jijini hapa anayedaiwa kuwa na elimu ya chuo kikuu, amejirusha katika jengo la la Rocky City Mall na kufariki dunia.

Imeelezwa kuwa Musa alichukua uamuzi huo kutokana na kuwa na msongo wa mawazo, kukosa kazi.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Desemba 21, 2018 kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Advera Bulimba amesema tukio hilo limetokea leo saa saba mchana.

Bulimba amesema kijana huyo alionekana akiwa amelewa kupita kiasi na tangu Desemba 16, 2018 na alikamatwa na kuwekwa kituo cha polisi Kirumba, kilevi kilipopungua aliachiwa.

Amesema katika uchunguzi wa awali marehemu alibainisha kuwa alikuwa na msongo wa mawazo kwa sababu ya kukosa kazi licha ya kuwa na elimu ya juu.

Bulimba amesema baada ya polisi kumuachia alikwenda kunywa tena pombe na baadaye kujirusha kutoka ghorofa ya tatu na kukutwa na pombe kali na ugoro.

“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa kijana huyo amesema amejiingiza kwenye ulevi na asilaumiwe mtu yeyote.

Amesema amechukua uamuzi huo yeye binafsi, pia akidai yeye ni masikini hana baba wala mama,” amesema Bulimba.

Amesema mwili umehifadhiwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi licha ya kutotaja jina la hospitali hiyo.

Bulimba amesema, maandishi aliyokutwa nayo marehemu yalisomeka kwamba “yeye ana shahada sayansi ya kompyuta aliyoipata Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).”

Chanzo:Mwananchi.

Police wamesomba Picha zimekataa kuupload. Ila nimeattach kwenye comment no 6 na 7.

IMG_20181223_083826.jpg
ajirusha ghorofani.jpeg
pic+msomi.jpg


R. I. P ndugu yetu Mussa Ally.

Mfumo wetu wa elimu unatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa, ili kila mhitimu akimalizia masomo yake aweze kujiajiri mwenyewe kwa elimu aliyoipata.
 
Computer science anajiua . Siangeenda nchi nyingine akatafute kazi .
 
madhara ya kuamini kuwa ukifika chuo basi lazima upate kazi ndo haya...

tupo watu tushasahau hata lini tulimaliza na bado twang'aza sharubu tu street!

Mungu amrehemu..
 
, ww unacheza?msoto huu co,mlioajiriwa mshahara ukikawia mna kuwa desperate saana ,je huyo kijana mdgo jobless inakuwaje!,mnajishau saana
Sijaajiriwa. Kijana mdogo atakuwa katoka chuo juzi Leo aseme amesota ajira? Watu wana zaidi ya miaka kumi hawajawahi sikia ajira sijaona wamejiua
 
Uwezo wa
Sijaajiriwa. Kijana mdogo atakuwa katoka chuo juzi Leo aseme amesota ajira? Watu wana zaidi ya miaka kumi hawajawahi sikia ajira sijaona wamejiua
watu wana mshahara lkn wanatembea wajiongelea wenyewe ,tuna manage stress tofauti kulingana na hali zetu ,weng rohoni pamechafuka saana,
 
Kweli magumu lakini kwanini kaamua kujitanguliza JAHANAM mwenyewe bora angevuta subra
 
Jiwe anaambiwa vyuma vimekaza yy anagawa vitambulisho. Angalia sasa kijana mdogo kajiua.
Kama mhitimu wa chuo kikuu anashindwa kujiongeza na mpaka anafikia kujiua hapa ujue upo walakini mkubwa sana ktk elimu tutoayo ktk vyuo vyetu vikuu, au ktk kuitafsiri elimu itolewayo ktk vyuo vyetu! Kama wale wasiofika hata chuo cha 'certificate' wanaweza kupambana na mazingira yao na kufanikiwa, iweje mhitimu wa choo kikuu!?
Naamini kuna jambo nyuma ya pazia tusilolijua juu ya sababu halisi ya kifo chake.
kama alikuwa na hela ya kulewa…alishindwaje kuibadili kuwa mtaji…najaribu kutafakari kwa maandishi tu!
 
Mkitaka serikal itoe ajira wote ambao hawana ajira mjiue ili serikal iogope itoe ajira asante sana kijana kwa kuonyesha mfano umeonyesh uzalendo unasoma zaid ya miaka 15 alaf serikal inajifanya haikufaham nawakati wanataarifa zako tangia ukiwa darasa la kwanza

Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
 
Mimi Tumaini Geofrey Temu limbukenitutababanana humuhumu nilisha tibiwa kichaa niwemuachia nyie na raisi wenu,, 2020.. Mrema agustino wariri mkuu Mama Maria Malkia Amitipal Sing Bhogal,,,
 
Na bado Mheshimiwa Rais anatwambia watanzania tutembee vifua mbele kwa kuwa we are in the right track!

Hii damu isiyo na hatia inayomwagika itaendelea kumlilia Jiwe kizazi na kizazi!
Sasa damu iliyofika chuo kikuu na ku- graduate Kisha kushindwa kutumia vyema alichojifunza huko chuoni kama wafanyavyo vijana wenzake na kuamua kujitoa uhai, hatia ipo wapi hapo??? Cha zaidi naona ameitia hasara serikali yetu, maana kale kamkopo ketu kimepotea sasa.
 
Bottom line ni kwamba binadamu ukiwa na changamoto ni vizuri ukashirikisha watu wako wa karibu kama huna tafuta hata mpita njia ongea naye. Pia epuka kuwa peke yako kabisa maana hii ndiyo itakuletea shida ya kuwaza.

Kikubwa zaidi kuna wasomi wa masuala ya saikolojia na sosholojia ila hawataki kufungua rehabilitation centres. Tanzania wengi kwa sasa wana msongo wa mawazo mno kwenye maeneo mbalimbali ila hawana wa kuwashauri na kila siku tunasikia mara kujiua mara kuua na kujiua yaani full stress tu.
 
Back
Top Bottom