Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bando ni mgogoroMnaishigi wapi au bando mzozo
Ally (25), mkazi wa Kiloleli wilayani Ilemela jijini hapa anayedaiwa kuwa na elimu ya chuo kikuu, amejirusha katika jengo la la Rocky City Mall na kufariki dunia.
Imeelezwa kuwa Musa alichukua uamuzi huo kutokana na kuwa na msongo wa mawazo, kukosa kazi.
Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Desemba 21, 2018 kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Advera Bulimba amesema tukio hilo limetokea leo saa saba mchana.
Bulimba amesema kijana huyo alionekana akiwa amelewa kupita kiasi na tangu Desemba 16, 2018 na alikamatwa na kuwekwa kituo cha polisi Kirumba, kilevi kilipopungua aliachiwa.
Amesema katika uchunguzi wa awali marehemu alibainisha kuwa alikuwa na msongo wa mawazo kwa sababu ya kukosa kazi licha ya kuwa na elimu ya juu.
Bulimba amesema baada ya polisi kumuachia alikwenda kunywa tena pombe na baadaye kujirusha kutoka ghorofa ya tatu na kukutwa na pombe kali na ugoro.
“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa kijana huyo amesema amejiingiza kwenye ulevi na asilaumiwe mtu yeyote.
Amesema amechukua uamuzi huo yeye binafsi, pia akidai yeye ni masikini hana baba wala mama,” amesema Bulimba.
Amesema mwili umehifadhiwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi licha ya kutotaja jina la hospitali hiyo.
Bulimba amesema, maandishi aliyokutwa nayo marehemu yalisomeka kwamba “yeye ana shahada sayansi ya kompyuta aliyoipata Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).”
Chanzo:Mwananchi.
Police wamesomba Picha zimekataa kuupload. Ila nimeattach kwenye comment no 6 na 7.
Sijaajiriwa. Kijana mdogo atakuwa katoka chuo juzi Leo aseme amesota ajira? Watu wana zaidi ya miaka kumi hawajawahi sikia ajira sijaona wamejiua, ww unacheza?msoto huu co,mlioajiriwa mshahara ukikawia mna kuwa desperate saana ,je huyo kijana mdgo jobless inakuwaje!,mnajishau saana
watu wana mshahara lkn wanatembea wajiongelea wenyewe ,tuna manage stress tofauti kulingana na hali zetu ,weng rohoni pamechafuka saana,Sijaajiriwa. Kijana mdogo atakuwa katoka chuo juzi Leo aseme amesota ajira? Watu wana zaidi ya miaka kumi hawajawahi sikia ajira sijaona wamejiua
Kama mhitimu wa chuo kikuu anashindwa kujiongeza na mpaka anafikia kujiua hapa ujue upo walakini mkubwa sana ktk elimu tutoayo ktk vyuo vyetu vikuu, au ktk kuitafsiri elimu itolewayo ktk vyuo vyetu! Kama wale wasiofika hata chuo cha 'certificate' wanaweza kupambana na mazingira yao na kufanikiwa, iweje mhitimu wa choo kikuu!?Jiwe anaambiwa vyuma vimekaza yy anagawa vitambulisho. Angalia sasa kijana mdogo kajiua.
Unajidanganya sanaHii inikumbusha Mohammed Bouaziz alivyojichoma moto na Ku spark mabadiliko ya utawala wa kidikteta na kishenzi pale Tunisia. One day yes!
Kwani lazima ukubali uongo wangu?Unajidanganya sana
Sasa damu iliyofika chuo kikuu na ku- graduate Kisha kushindwa kutumia vyema alichojifunza huko chuoni kama wafanyavyo vijana wenzake na kuamua kujitoa uhai, hatia ipo wapi hapo??? Cha zaidi naona ameitia hasara serikali yetu, maana kale kamkopo ketu kimepotea sasa.Na bado Mheshimiwa Rais anatwambia watanzania tutembee vifua mbele kwa kuwa we are in the right track!
Hii damu isiyo na hatia inayomwagika itaendelea kumlilia Jiwe kizazi na kizazi!