Mhubiri afukuzwa akiwa anahubiri Kariakoo, kwa madai ya kuleta usumbufu kwenye biashara

TheCrocodile

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2021
Posts
1,864
Reaction score
5,254
Muhubiri wa neno la Mungu, mkazi wa wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam, aitwae Evod Medson, amedai kuwa amejikuta kwenye hali ya sintofahamu wakati akitoa mahubiri, baada mwanamke mmoja kumtaka akatishe mahubiri mara moja, kwa tuhuma kuwa mahubiri hayo yanaleta usumbufu kwenye biashara.

Katika tukio hilo ambalo linadaiwa kutokea maeneo ya Kariakoo Jijini humo, Agasti 11, 2026, Evod amesema kuwa baada ya kutakiwa kusitisha mahubiri, aliondoka na kwenda sehemu nyingine, licha ya watu kadhaa kuonyesha utayari wakusikiliza mahubiri katika eneo hilo.

Aidha, Evod amesema kuwa hata kama angelikuwa kinyume na sheria za nchi kwenye eneo lile, waliopaswa kumuondosha ni viongozi wa eneo husika na sio kwa kufukuzwa kama ilivyotokea.

"...alikuwa anasema napigia wateja kelele, nikamwambia asubiri nimalizie kuhubiri, akafanya vurugu, nikaamua kuondoka" Evod.

Kadhalika, Evod amesema tukio hilo limempa sitofahamu zaidi ukilinganisha kuwa eneo lile ni stendi na kulikuwa na kelele nyingi za magari na purukushani nyingine, lakini mwanamke huyo akamnyooshea kidole yeye tu.

Video:
View: https://www.facebook.com/share/v/1BChj6dEtM/
 
Sawa sawa
 
Tatizo wafanyabiashara na walokole wamezingatia nadharia ya Kibongo bongo kwamba ni lazima kupiga kelele, kutoka mipovu mdomoni na mishipa ya paji la uso na shingo isimame dede ili watu washawishike.

Huko mitaani ni hivyo vivyo, mtu anafungulia mziki kwa sauti kubwa inayokera walio karibu, ukimgusa ananuka kwa madai kwamba anafanya biashara. Mbona benki zinafanya biashara kubwa lakini hazizalishi makelele kwa washikadau?
 
Kuna wengine pia wanatupigia makelele ya kengere kila saa 11 alfajiri na 12 jioni. Wajirekebishe pia maana huo ni usumbufu. Karne hii kuna saa za mkononi na simu zinazoonyesha muda hakuna haja ya kuitana kwa kengere.
 
Safi sana hii ni noise pollution ukitaka kuhubiri subiri jumapili nenda kanisani ukapige kelele..wadili na wale wengine ikifika ijumaa wanafunga barabara kuleta usumbufu kwa watumiaji barabara
 
Back
Top Bottom