Muhubiri wa neno la Mungu, mkazi wa wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam, aitwae Evod Medson, amedai kuwa amejikuta kwenye hali ya sintofahamu wakati akitoa mahubiri, baada mwanamke mmoja kumtaka akatishe mahubiri mara moja, kwa tuhuma kuwa mahubiri hayo yanaleta usumbufu kwenye biashara.
Katika tukio hilo ambalo linadaiwa kutokea maeneo ya Kariakoo Jijini humo, Agasti 11, 2026, Evod amesema kuwa baada ya kutakiwa kusitisha mahubiri, aliondoka na kwenda sehemu nyingine, licha ya watu kadhaa kuonyesha utayari wakusikiliza mahubiri katika eneo hilo.
Aidha, Evod amesema kuwa hata kama angelikuwa kinyume na sheria za nchi kwenye eneo lile, waliopaswa kumuondosha ni viongozi wa eneo husika na sio kwa kufukuzwa kama ilivyotokea.
"...alikuwa anasema napigia wateja kelele, nikamwambia asubiri nimalizie kuhubiri, akafanya vurugu, nikaamua kuondoka" Evod.
Kadhalika, Evod amesema tukio hilo limempa sitofahamu zaidi ukilinganisha kuwa eneo lile ni stendi na kulikuwa na kelele nyingi za magari na purukushani nyingine, lakini mwanamke huyo akamnyooshea kidole yeye tu.
Video:
View: https://www.facebook.com/share/v/1BChj6dEtM/