Mhubiri afukuzwa akiwa anahubiri Kariakoo, kwa madai ya kuleta usumbufu kwenye biashara

Mhubiri afukuzwa akiwa anahubiri Kariakoo, kwa madai ya kuleta usumbufu kwenye biashara

Safi sana hii ni noise pollution ukitaka kuhubiri subiri jumapili nenda kanisani ukapige kelele..wadili na wale wengine ikifika ijumaa wanafunga barabara kuleta usumbufu kwa watumiaji barabara
Utaambiwa unaingilia uhuru wa watu kuabudu mkuu.
 
Tatizo wafanyabiashara na walokole wamezingatia nadharia ya Kibongo bongo kwamba ni lazima kupiga kelele, kutoka mipovu mdomoni na mishipa ya paji la uso na shingo isimame dede ili watu washawishike.

Huko mitaani ni hivyo vivyo, mtu anafungulia mziki kwa sauti kubwa inayokera walio karibu, ukimgusa ananuka kwa madai kwamba anafanya biashara. Mbona benki zinafanya biashara kubwa lakini hazizalishi makelele kwa washikadau?
Nakubali. Yaani suala la noise pollution limekua ni la kawaida kwenye mitaa yetu.
 
Kuna chizi mmoja nae katoka West Africa alijiingiza kwenye sintofahamu kama hiyo, Picadilly, London. Ndio ujue kuna watu hawana akili, yaani wewe utoke kwnu Africa ukahubiri injili kwa wazungu wakati wao wametulea biblia. Ndio wengi wa hawa watu ni machizi
 
Namuonea huruma huyo mama,....pona yake aokoke vinginevyo kuna giza mbeleni
Only if huyo Mtumishi anachokifanya ametumwa na Mungu na sio kutumwa na Mtu au kujituma mwenyewe, vinginevyo laana isiyo haki haimpati mtu.

Ukitumwa na Mungu unapata kibali kisicho na makandokando,atakayeinuka kukupinga atakutana na upinzani kutoka kwa wale wanaobarikiwa na Injili unayowahubiria.

Mungu akikutuma anakupa Hekima ya kukusaidia kuepuka manung'uniko(malalamiko) halali. Ndio,kuna malalamiko halali kabisa,kwa mfano umeenda kuweka spika mahali ambapo kuna mjasiriamali huwa anapanga biashara yake au umeblock biashara ya mtu haionekani kwa wapita njia n.k.

Nimeshare uzoefu wangu wa kuhubiri Injili mitaani. Katika mitaa niliyotumwa na Mungu nikaihubiri Habari yake njema kote nilipata ushirikiano wa kutosha sana. Kwa kifupi wapo ambao hata sasa wananiuliza nitaenda tena lini wasijue kwamba kazi ya Mungu inaenda na majira . Majira husika yakipita yamepita!šŸ˜€

Kosa la wahubiri wengi huwa wanajituma wao au wanatumwa na watu badala ya kusubiri waandaliwe na watumwe na Mungu mwenyewe,matokeo yake wanafanya jina la Mungu linatukanwa badala ya kutukuzwa!

Kuna tofauti kati ya kuifanya kazi ya Mungu na kufanya kazi na Mungu!
 
Back
Top Bottom