Kapeace
JF-Expert Member
- May 26, 2017
- 24,514
- 65,521
Mi ni binadamu naanguka nakung'uta vumbi na kusonga mbele,Asante rafiki...Vp na wewe huna majuto?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mi ni binadamu naanguka nakung'uta vumbi na kusonga mbele,Asante rafiki...Vp na wewe huna majuto?
Kweli kabisa....ishu ni kutokukata tamaa tu!Mi ni binadamu naanguka nakung'uta vumbi na kusonga mbele,
Kuhusu maisha!senior wengi wana mengi wamepitia!wanakupa info ya mambo mengi kuhusu maisha na maamuzi ya kuchukua!!!mkuu ni stori zipi unazomaanisha
kabisa kaka, sema mda mwingine ujana unasumbua huwezi kukumbuka hayoKuhusu maisha!senior wengi wana mengi wamepitia!wanakupa info ya mambo mengi kuhusu maisha na maamuzi ya kuchukua!!!
majuto ya nyuma yanaumiza sana mkuuAisee, hii stori inasomo kubwa
ujana huwa unasumbua wengi mkuuUnabahat ajira hujappteza. Kuna rafiki angu hapa alikuwa accacia. Milion moja kwake ilikuwa sio pesa. Anatumia wanawake atakavyo. Akatumbuliwa sasa hivi kawa dalali na anaish kwa kubet. Kiinua mgongo chake cha m60 cha maana ni Gar bac.
Sanaa bob.Kuna watu wana bahati sana dunia hii. Sanaa yan.All in all mkuu una bahati sana you get a job with 21 yrs and u paid over 850k,wengine we are approaching 32yrs with no reliable job hata laki 5 it's big deal then unakopeshwa over 45m kwa ajili tu ya ujenz na bado unafanya uhuni, some people are really blessed!
Sent using Jamii Forums mobile app
sikatai boss inawezekana umri na kutokea shule kulichangiaUlikuwa sahihi tu kuyapitia uliyoyapitia miaka 21,22,23 ni mtoto mdogo sana kukamata hela nyingi tena ukitokea shuleni,ungetokea mtaani ungekuwa na mtazamo wa msoto,na usingeyapitia hayo kwa wakati ule ungekuja kuyapitia ukubwani,Uzuri umestuka mapema kuna wengi tu wanastaafia nyumba za serikali/mashirika wakipewa pensions ndipo wanajenga na kausafiri kisha wanakufa kwa stress na kukaa bila kufanya kazi mwili unakoswa mazoezi.
ubarikiwe sana bossHapo kwenye anasa na kuendekeza mademu ndio mtego wa vijana wengi ulipo..ila kwa bandiko hili una thawabu zako mkuu kwa Mungu.. wenye macho wanaona mkuu!
Kuna mda huwa tunafanya makosa mengi sana katika maisha tena mengine ya kujitakia kabisa ambayo ukiyakumbuka baadae unayajutia sana. Binafsi kama ningetumia mda vizuri ningekuwa mbali sana sana kimafanikio kuliko nilivo sasa.
Kipindi namaliza O' level baada ya matokeo kutoka nikapangwa Moshi Technical kwa elimu ya Advance, nikabadili kwenda Dar Es Salaam Institute of Technology (DIT) kusoma FTC kwa miaka 3, nilipomaliza tu nikaunganisha degree MIST, nikiwa semister ya kwanza na umri wangu wa 21yrs naelekea 22 MUNGU akawa upande wangu nikaajiriwa nikiwa kijana mdogo kabisa nikiwa na 21 kama technician katika moja ya taasisi inayolipa vizuri sana hapa nchini ikabidi niahirishe chuo kwa mda niingie kwenye ajira hii ilikuwa 2009 mwishoni, kwa kipindi hicho kwa hiyo level yangu nilikuwa nalipwa 840k kama mshahara kwa mwezi, bado kulikuwa na housing Allowance 240k,Transport allowance 200k, posho ya mawasiliano 60k, Lunch 150k na Extra duty ambayo hii tulikuwa tunaingiziwa wafanyakazi wote sawa kila mwisho wa mwezi 350k na bado kukawa na safari nyingi sana ilikuwa ni kawaida kumaliza mwezi sijaona mlango wa ofisi, nakuwa safarini tu huko mikoani site kikazi napambana na per diem kila uchao.
Ofisi ilikuwa inatoa mikopo kwa wafanyakazi wake wapya ya bila riba za kujengea nyumba, kwa level yangu kipindi hicho nilikopeshwa 48m na zikawa zinakatwa kwenye posho na sio kwenye mshahara. Kiukweli kitu ambacho ninakijutia mpaka leo nikikumbuka naumia sana basi ni miaka yangu 4 ya mwanzo kwenye ajira (2009-2012) nilipoteza pesa nyingi sana kwenye mambo ya kijinga kabisa na badala yake nikawa mtu wa hovyo sana kuliko kipindi chochote katika historia ya maisha yangu, nadhani umri na kutopata washauri wazuri pia kulichangia hili.
Nilipopangiwa kituo changu cha kazi nilipewa 3+m za kujikimu, karibia robo tatu za hizi pesa nilitumia kujivinjari na wasichana wa CBE waliokuwa wananitolea nje kipindi cha zamani na hata nilipopewa pesa ya mkopo wa ofisi sikuweza kufanya la maana kubwa la kuweza kujivunia japokuwa kiasi cha pesa katika huo mkopo nilitumia kuwajengea na kukarabati nyumba ya zamani ya wazazi na mwaka uliofuata nikakopa CRDB tena 15m kupitia mshahara wangu, kipindi nakopa hii pesa nilikuwa nakaribia kwenda likizo yangu ya mwaka na asilimia 80 ya hizi pesa niliitumia kwenye starehe na wanawake kwenye hoteli tofauti tofauti, Sasa nikawa nakatwa kwenye mshahara na posho zinakatwa kulipia madeni ya mkopo nikawa napata kiasi kidogo tu japo kwa matumizi ya kawaida kilikuwa kinatosha kwa kujibana ikizingatiwa wazazi nao tayari nilikuwa tegemeo lao, Nikaanza kuishi kwa kutegemea zaidi per diem za safari za kikazi.
Mwaka 2011 nilimpa mdada mmoja mimba alikuwa anamalizia diploma yake TPSC ikabidi nikae nae kama mke wangu hata hatukufanya harusi mwenyewe hakutaka kabisa japo wazazi wa pande zote walitaka tufunge harusi kanisani na sherehe ifanyike na kiukweli hata uchumi wangu ulikuwa hauruhusu hili nadhani wife alisoma upepo mapema , Nilimshirikisha Mkurugenzi wangu tulichoafikiana na mwenzangu kuhusu ndoa yetu na jinsi ya kupata cheti cha ndoa ili aweze kupata bima ya afya kupitia kazi yangu kama mke wangu halali, Wakubwa wanajuana bhana, usiku wa siku hiyohiyo ananipigia simu akinitaarifu tujiandae kesho yake anakuja kutuchukua tukasaini cheti cha ndoa nadhani ilikuwa ni RITA pale kama kumbukumbu zangu ziko sawa, lilikuwa ni jengo la ofisi za mkuu wa wilaya na mle ndani ndo kulikuwa na hizo ofisi za RITA sikujua hata kimelipiwa bei gani hicho cheti tulisaini tu na mashahidi zetu wawili wa pale ofisini akiwemo mkurugenzi then tukachukua vyeti tukamrudisha wife nyumbani mimi nikaingia kazini kuendelea na majukumu na hapa ndipo maisha mapya yalipoanza.
Mwaka 2012 nikahamishiwa Arusha na kupewa ruhusa ya kuendelea na masomo yangu ya shahada ATC kwa kujilipia mwenyewe, hapa pia ndipo nilipoanza kufeel ule ugumu wa maisha na kuona utofauti kati ya akili ya kikubwa na kitoto.Posho zina madeni, mshahara una madeni, safari zimepungua kwa sababu niko shule nina mke,mtoto wote wananiangalia mimi , maisha yalikuwa magumu sana kwangu kwa kipindi hicho huku nikiona wenzangu tulioajiriwa nao waliokuwa na umri mkubwa kidogo wao wakiwa mbali sana kimaendeleo na wakawa wananishangaa mimi kuona Inawezekanaje kuishi maisha yale ninayoishi na kwa namna ile tunayolipwa huku nikiwa sina majukumu mengi.
Baada ya kumaliza chuo 2015, ikabidi nijipange upya na mkopo ukawa umemalizikia na hata biashara sikuwa nayo pamoja na kukopa pesa zote hizo na kuugulia maumivu ya mkopo kwa miaka 5 na dogo nae anatakiwa aanze kindergarten na tayari ana mdogo wake mwingine😀😀 MAISHA HAYA. nikaanza kusuka mipango upya utafikiri ndio nimeanza ajira rasmi, Kibaya zaidi kipindi hicho wenzangu nilioajiriwa nao baadhi wako mbali sana, wana familia, wana nyumba nzuri, wana gari na biashara zao wakati mimi nimepanga chumba kimoja tu wakati huo mpaka namaliza masomo yangu ATC😎
Yale maisha na nikiwaangalia wenzangu itabaki kuwa kumbukumbu mbaya kichwani mwangu, uzuri nilitambua baadhi ya makosa yangu mapema nikajipanga upya nikiwa na akili ya kikubwa zaidi kuliko wakati ule, Japo sio sana ila somehow nime - win kidogo, lakini sio kama hatua walizo nazo wenzangu, ningekuwa na akili ya kikubwa kipindi kile ningekuwa mbali, mwaka jana nimetimiza miaka 10 ya utumishi wa umma nikiwa mwajiriwa na naelekea miaka 32 kiumri miezi michache ijayo bado ile kumbukumbu inagoma kabisa kufutika katika fikra zangu.unaweza kudhani natania lakini huu ndio ukweli kiasi ambacho nikikumbuka inaniuma sana hata kuandika hapa nakuwa kama napunguza mzigo wa maumivu wa ujinga wangu niliobeba moyoni
Pamoja na yote, mungu alinionesha mwanamke bora sana kwenye maisha yangu ambae hata sikuwahi kufikiria kumuoa ilitokea kama emergency tu hakuwa kati ya wasichana niliodumu nao kimahusiano kwa mda mrefu wala sikuwahi kumpenda, moyo wangu ulipenda kwingine kabisa na hata kwenye mipango yangu hakuwepo kabisa. Lakini kadri nilivoishi nae nimefahamu KWELI MKE BORA ANATOKA KWA MUNGU, mawazo yake yamebadili KABISA maisha yetu , kuna mda naona kabisa huyu kanizidi uwezo wa kufikiri hapa namzidi pesa tu, ni zaidi ya spiritual woman na mrembo haswa ni kivile tu wanaume huwa haturidhiki lazma tukaonje radha zingine nje.
Nashehekea miaka yangu 10 ya utumishi nikiwa na mtazamo mpya kabisa wa kuacha kazi ndani ya miaka 5 ijayo nijikite zaidi kuendesha miradi na biashara zangu niliyofungua ili kufikia malengo yangu niliyojiwekea. Kwa sasa ni baba wa familia, nina watoto kadhaa na mwanagu wa kwanza nimempata nikiwa na miaka 23 tu kwa sasa ana 8yrs anaelekea 9 miezi michache ijayo
Pole sana ndugu yangu, haya mapito huwa yanaumiza sana kuyakumbukaMkuu Hongera sana kwa kuinuka tena. Mimi story yangu inafanana na ya kwako ila kikubwa kilichonitesa mimi ni pombe. Ilinitesa mnooo. Kiasi kwamba ndoa yangu ilitetereka. Kama sio mke wangu kusimama kwenye maombi hata kazi ningepoteza. Nilikuja kuamka nikasema kuanzia leo (POMBE NO) toka pale nikauona ukuu wa Mungu. Maisha yangu yamebadilika kabisaa.
kabisa ndugu yangu, hayo yameshapita tunajikumbusha ili kutoa uvundo kifuaniPole sana kiongozi, kwa angle nyingine nakupa hongera. Wewe ni age mate kwangu.
Mimi binasfi niko na miaka 15 ya kujiaji baada ya mafunzo ya ufundi.
Kweli ukitathimini kwa kina miaka 10 imeishaje huwa majibu hakuna.
Uzembe, kutokujua, kutokua na maono, mwelekeo mbovu nknk ndio hugarimu ndoto za vijana wengi.
Pia kukosa msingi mzuri wa maisha nayo huchagi.
Lakini tunamshukuru Mungu hutuinua tena pale tunapoanguka.
Nukuu fulani inasema usiangalie pale ulipoangukia bali ulipotelezea ukaparekebishe.
Katika maisha Hakuna kuchelewa Wala kuwahi heri yako ulifungulia zipu na starehe ujana, kuwekeza sio kupata wawezawekeza na zisizae vile vile.Kuna wengine wamewekeza zaid ya milioni 200 jumla ya miaka 15 na zote zimezama kila wakiwekeza tena kwa kujinyima na Wana miaka 50 bado awajatoka Wala kukata tamaa,wanaamini zitarudi tu.Kuna mda huwa tunafanya makosa mengi sana katika maisha tena mengine ya kujitakia kabisa ambayo ukiyakumbuka baadae unayajutia sana. Binafsi kama ningetumia mda vizuri ningekuwa mbali sana sana kimafanikio kuliko nilivo sasa.
Kipindi namaliza O' level baada ya matokeo kutoka nikapangwa Moshi Technical kwa elimu ya Advance, nikabadili kwenda Dar Es Salaam Institute of Technology (DIT) kusoma FTC kwa miaka 3, nilipomaliza tu nikaunganisha degree MIST, nikiwa semister ya kwanza na umri wangu wa 21yrs naelekea 22 MUNGU akawa upande wangu nikaajiriwa nikiwa kijana mdogo kabisa nikiwa na 21 kama technician katika moja ya taasisi inayolipa vizuri sana hapa nchini ikabidi niahirishe chuo kwa mda niingie kwenye ajira hii ilikuwa 2009 mwishoni, kwa kipindi hicho kwa hiyo level yangu nilikuwa nalipwa 840k kama mshahara kwa mwezi, bado kulikuwa na housing Allowance 240k,Transport allowance 200k, posho ya mawasiliano 60k, Lunch 150k na Extra duty ambayo hii tulikuwa tunaingiziwa wafanyakazi wote sawa kila mwisho wa mwezi 350k na bado kukawa na safari nyingi sana ilikuwa ni kawaida kumaliza mwezi sijaona mlango wa ofisi, nakuwa safarini tu huko mikoani site kikazi napambana na per diem kila uchao.
Ofisi ilikuwa inatoa mikopo kwa wafanyakazi wake wapya ya bila riba za kujengea nyumba, kwa level yangu kipindi hicho nilikopeshwa 48m na zikawa zinakatwa kwenye posho na sio kwenye mshahara. Kiukweli kitu ambacho ninakijutia mpaka leo nikikumbuka naumia sana basi ni miaka yangu 4 ya mwanzo kwenye ajira (2009-2012) nilipoteza pesa nyingi sana kwenye mambo ya kijinga kabisa na badala yake nikawa mtu wa hovyo sana kuliko kipindi chochote katika historia ya maisha yangu, nadhani umri na kutopata washauri wazuri pia kulichangia hili.
Nilipopangiwa kituo changu cha kazi nilipewa 3+m za kujikimu, karibia robo tatu za hizi pesa nilitumia kujivinjari na wasichana wa CBE waliokuwa wananitolea nje kipindi cha zamani na hata nilipopewa pesa ya mkopo wa ofisi sikuweza kufanya la maana kubwa la kuweza kujivunia japokuwa kiasi cha pesa katika huo mkopo nilitumia kuwajengea na kukarabati nyumba ya zamani ya wazazi na mwaka uliofuata nikakopa CRDB tena 15m kupitia mshahara wangu, kipindi nakopa hii pesa nilikuwa nakaribia kwenda likizo yangu ya mwaka na asilimia 80 ya hizi pesa niliitumia kwenye starehe na wanawake kwenye hoteli tofauti tofauti, Sasa nikawa nakatwa kwenye mshahara na posho zinakatwa kulipia madeni ya mkopo nikawa napata kiasi kidogo tu japo kwa matumizi ya kawaida kilikuwa kinatosha kwa kujibana ikizingatiwa wazazi nao tayari nilikuwa tegemeo lao, Nikaanza kuishi kwa kutegemea zaidi per diem za safari za kikazi.
Mwaka 2011 nilimpa mdada mmoja mimba alikuwa anamalizia diploma yake TPSC ikabidi nikae nae kama mke wangu hata hatukufanya harusi mwenyewe hakutaka kabisa japo wazazi wa pande zote walitaka tufunge harusi kanisani na sherehe ifanyike na kiukweli hata uchumi wangu ulikuwa hauruhusu hili nadhani wife alisoma upepo mapema , Nilimshirikisha Mkurugenzi wangu tulichoafikiana na mwenzangu kuhusu ndoa yetu na jinsi ya kupata cheti cha ndoa ili aweze kupata bima ya afya kupitia kazi yangu kama mke wangu halali, Wakubwa wanajuana bhana, usiku wa siku hiyohiyo ananipigia simu akinitaarifu tujiandae kesho yake anakuja kutuchukua tukasaini cheti cha ndoa nadhani ilikuwa ni RITA pale kama kumbukumbu zangu ziko sawa, lilikuwa ni jengo la ofisi za mkuu wa wilaya na mle ndani ndo kulikuwa na hizo ofisi za RITA sikujua hata kimelipiwa bei gani hicho cheti tulisaini tu na mashahidi zetu wawili wa pale ofisini akiwemo mkurugenzi then tukachukua vyeti tukamrudisha wife nyumbani mimi nikaingia kazini kuendelea na majukumu na hapa ndipo maisha mapya yalipoanza.
Mwaka 2012 nikahamishiwa Arusha na kupewa ruhusa ya kuendelea na masomo yangu ya shahada ATC kwa kujilipia mwenyewe, hapa pia ndipo nilipoanza kufeel ule ugumu wa maisha na kuona utofauti kati ya akili ya kikubwa na kitoto.Posho zina madeni, mshahara una madeni, safari zimepungua kwa sababu niko shule nina mke,mtoto wote wananiangalia mimi , maisha yalikuwa magumu sana kwangu kwa kipindi hicho huku nikiona wenzangu tulioajiriwa nao waliokuwa na umri mkubwa kidogo wao wakiwa mbali sana kimaendeleo na wakawa wananishangaa mimi kuona Inawezekanaje kuishi maisha yale ninayoishi na kwa namna ile tunayolipwa huku nikiwa sina majukumu mengi.
Baada ya kumaliza chuo 2015, ikabidi nijipange upya na mkopo ukawa umemalizikia na hata biashara sikuwa nayo pamoja na kukopa pesa zote hizo na kuugulia maumivu ya mkopo kwa miaka 5 na dogo nae anatakiwa aanze kindergarten na tayari ana mdogo wake mwingine😀😀 MAISHA HAYA. nikaanza kusuka mipango upya utafikiri ndio nimeanza ajira rasmi, Kibaya zaidi kipindi hicho wenzangu nilioajiriwa nao baadhi wako mbali sana, wana familia, wana nyumba nzuri, wana gari na biashara zao wakati mimi nimepanga chumba kimoja tu wakati huo mpaka namaliza masomo yangu ATC😎
Yale maisha na nikiwaangalia wenzangu itabaki kuwa kumbukumbu mbaya kichwani mwangu, uzuri nilitambua baadhi ya makosa yangu mapema nikajipanga upya nikiwa na akili ya kikubwa zaidi kuliko wakati ule, Japo sio sana ila somehow nime - win kidogo, lakini sio kama hatua walizo nazo wenzangu, ningekuwa na akili ya kikubwa kipindi kile ningekuwa mbali, mwaka jana nimetimiza miaka 10 ya utumishi wa umma nikiwa mwajiriwa na naelekea miaka 32 kiumri miezi michache ijayo bado ile kumbukumbu inagoma kabisa kufutika katika fikra zangu.unaweza kudhani natania lakini huu ndio ukweli kiasi ambacho nikikumbuka inaniuma sana hata kuandika hapa nakuwa kama napunguza mzigo wa maumivu wa ujinga wangu niliobeba moyoni
Pamoja na yote, mungu alinionesha mwanamke bora sana kwenye maisha yangu ambae hata sikuwahi kufikiria kumuoa ilitokea kama emergency tu hakuwa kati ya wasichana niliodumu nao kimahusiano kwa mda mrefu wala sikuwahi kumpenda, moyo wangu ulipenda kwingine kabisa na hata kwenye mipango yangu hakuwepo kabisa. Lakini kadri nilivoishi nae nimefahamu KWELI MKE BORA ANATOKA KWA MUNGU, mawazo yake yamebadili KABISA maisha yetu , kuna mda naona kabisa huyu kanizidi uwezo wa kufikiri hapa namzidi pesa tu, ni zaidi ya spiritual woman na mrembo haswa ni kivile tu wanaume huwa haturidhiki lazma tukaonje radha zingine nje.
Nashehekea miaka yangu 10 ya utumishi nikiwa na mtazamo mpya kabisa wa kuacha kazi ndani ya miaka 5 ijayo nijikite zaidi kuendesha miradi na biashara zangu niliyofungua ili kufikia malengo yangu niliyojiwekea. Kwa sasa ni baba wa familia, nina watoto kadhaa na mwanagu wa kwanza nimempata nikiwa na miaka 23 tu kwa sasa ana 8yrs anaelekea 9 miezi michache ijayo
😀😀 Boss acha utani, unanitakiwa kheri ya kufungulia zipu hahaKatika maisha Hakuna kuchelewa Wala kuwahi heri yako ulifungulia zipu na starehe ujana, kuwekeza sio kupata wawezawekeza na zisizae vile vile.Kuna wengine wamewekeza zaid ya milioni 200 jumla ya miaka 15 na zote zimezama kila wakiwekeza tena kwa kujinyima na Wana miaka 50 bado awajatoka Wala kukata tamaa,wanaamini zitarudi tu.
serious?Ni heri upoteze pesa kwenye starehe za ujana kuliko kupotea kwenye uwekezaji huku ukijinyima.