Kama huna ushaidi na hicho unachokidai mkuu, hoja yako itakuwa haina tofauti na maneno ya kwenye vijiwe vya kahawa na mafundi washona viatu pale posta.
Shida yako kwake ni ipi mkuu? kuanzisha biashara kwa kutumia "pesa chafu" kama unavyodai au yeye kutumia ubunifu wake kufanikiwa kibiashara? Hapo la mhm na la kujifunza ni ubunifu wa biashara zake na vipi ameweza kuendelea ku survive na kuwa mfanyabiashara mkubwa ktk eneo hilo.
Lakini yakupasa ujue ya kuwa, kutoa pesa toka kwa source yyt ile, iwe halali au haramu na kuanzisha biashara, ni kitu kingine.....na kufanikiwa au kuifanya hy biashara ikue na kudumu ni kitu kingine.
Hakuna mfanyabiashara mkubwa hata mmj, ambae alianza au anaendelea kufanya biashara bila kufanya kitu kinyume na sheria na taratibu, ingawa mimi si advocate mabaya kwenye biashara, ila nachojaribu ni kuangalia mambo ktk jicho la tatu. Kuna wanaowadhulumu wafanyakazi wao, kuna wanaokwepa kodi, kuna wanaoua n.k.
Ila bado mimi sitaki kuamini kama inteligensia yako iko vzr sana, kuliko ya waliopewa mamlaka hayo, ambao hadi leo hawajampeleka mahakamani.
Nakusihi dada yangu fanya kazi kwa bidii mpk na wewe siku moja tuje tukuite majina kama freemason, tajiri wa ngadu, muuza sembe, punda n.k maana ndy tunayoyaweza, ila kwa sasa wacha jamaa atunyooshe sisi wavivu na waoga wa kuchangamkia fursa.
Adios!