Wasalam,
Miaka 15 iliyopita kuna uncle wangu mmoja ambaye hatukuwa tunapisha sana umri alifariki kwa ajali akiwa anatoka Dodoma kuja Dar.
Labda nikupe historia kidogo ya huyu uncle ambaye pia alikuwa rafiki na mshikaji wa karibu sana.
Huyu uncle alikuwa mtu wa mambo mengi sana kwenye kutafuta hela, alifanya biashara, aliwahi kuwa baharia lakini pia alikuwa na mambo mengine mengi.
Na kwa kweli alipata mafanikio mapema sana. Baada ya kufanya ubaharia kwa miaka 4 alirudi Tanzania na kuanza kufanya biashara zake mbalimbali.
Yeye aliishia kidato cha nne na kuanza kutafuta hela wakati sisi wengine tuliendelelea na masuala ya kitaaluma.
Miaka kadhaa nyuma aliwahi kuja kuishi kwa dada yake ambaye ni mama yangu, wakati huo mimi nilikuwa naendelea na elimu yeye akiwa na mambo yake.
Wakati akiishi kwetu alikuwa na mahusiano na binti mmoja wa Kisomali, miaka ile Wasomali walikuwa wengi sana mitaa ya Ilala.
Binafsi nilikuwa najua yale mahusiano maana nilitambulishwa na uncle, baadaye binti akapata ujauzito, uncle akawa anahudumia ile mimba na kwa kweli ni mimi pekee niliyekuwa najua kuhusu hilo suala.
Kabla mtoto hajazaliwa uncle akaondoka safari yake ya kwanza ya ubaharia.
Nachokumbuka ni kwamba jamaa aliacha fedha kwa yule dada kwa ajili ya matumizi yake na gharama za hospitali na kiasi cha kuanzia malezi ya mtoto.
Yule dada naye akasafiri, aliniaga tu kuwa anaenda kujifungulia Arusha kwa sababu kule ndio kuna ndugu zake.
Maisha yakaendelea na mimi nikaendelea na maisha yangu baada ya kumaliza masomo ya chuo.
Baada ya miezi kama 10 hizi uncle akarudi na kwenda Arusha kuona mtoto wake, nikapewa taarifa kuwa amezaliwa mtoto wa kiume na kwa mujibu wa anko dogo anafanana sana na yeye. Nikampa hongera na maisha yakaendelea.
Nikiwa nimeshaanza kazi nikapata nafasi ya kwenda Arusha miaka ile wakati ndio ujenzi wa Makao Makuu ya Afrika Mashariki unaanza pale Arusha.
Nikamcheki anko kuwa nitakuwa Arusha kwa siku kadhaa basi akanipa namba ya dada Msomali na hatimaye nikapata nafasi ya kumuona dogo ambaye kwa kweli alikuwa na sura ya anko kabisa.
Wakati huo dogo alikuwa na miaka mitano. Nilichogundua wakati huo ni kwamba dada Msomali alikuwa ameshaolewa na mwanaume mwingine ambaye alikuwa msomali mwenzake.
Dada Msomalia akanieleza kuwa uncle wako hawezi kumuoa kwa sababu kadhaa ikiwemo ya kidini. Hivyo yeye ameolewa na kwa kweli uncle alikuwa anatunza mtoto wake kwa makubaliano kuwa mtoto akifika walau miaka 10 uncle atamchukua mtoto wake.
Turudi kwa uncle sasa, yeye akaendelea na maisha yake na akaoa mwanamke mwingine. Nakumbuka niliwahi kumuuliza, je mkewe anajua kuwa ana mtoto nje? Uncle alikuwa anacheka na kunijibu kuwa wakati ukifika basi atamjulisha mke wake.
Kifo cha ghafla.
Miaka minne baada ya kuoa akiwa na watoto wawili kwa mke wake wa ndoa, na dogo wa Arusha akiwa na miaka 9, uncle anapata ajali ya gari na kufariki.
Wakati huu uncle alikuwa tayari na investments mbalimbali, biashara, nyumba kadhaa na magari. Kiufupi alikuwa ametoka katika watu wa kipato cha kati bali kiwango cha juu. Maisha yalikuwa mazuri.
Ndugu na jamaa tukapata taarifa ya kifo cha uncle.
Kama ilivyo kawaida ya Waafrika, tukakusanyika kwa ajili ya msiba na kumpumzisha marehemu.
Huzuni na simanzi za kutosha kwetu sisi kama familia lakini kwa mke aliyeachiwa watoto wawili wadogo.
Siku ya tatu baada ya kuzika familia ikaamua kuwe na kikao kidogo kuhusu mustakabali wa familia ya Marehemu.
Baada ya majadiliano marefu babu yangu akauliza kuwa anasikia marehemu aliwahi kuwa na mtoto kabla ya ndoa, je ni kweli? Na kama ni kweli huyo mtoto yupo wapi?
Wafamilia wote wakawa kimya, nikiwa nyuma kabisa nikajikuta nasema ni kweli marehemu ana mtoto.
Babu akaniambia, sogea hapa mbele utueleze vizuri.
Hapo sasa ndio nikasogea mbele, huku mama yangu akiniangalia kwa umakini sana, nilikuwa na hakika kuwa ndugu wengi walikuwa wanajua kuwa marehemu ana mtoto ambaye kwa wakati juo alikuwa na miaka 9.
Basi nikaanza maelezo marefu kuhusu mtoto wa marehemu; nikatoa simu Nokia E63 na hata kuingia Facebook kwenye account ya dada wa Kisomali ili kuthibitisha maneno yangu.
Wakati simu ikiendelea kutembea mikononi ya watu ili waone picha ya mtoto wa marehemu; mke wa marehemu akaanza kulia huku akisema kuwa yeye hatambua mtoto mwingine yoyote zaidi ya watoto wawili wa marehemu. Nikaona hapa tayari ishapigwa hesabu ya nyumba, magari na pesa za marehemu.
Kikao kikaisha, mimi sasa nikaanza kushambuliwa kuwa sikuwa na haja ya kueleza hayo mambo kwa sababu nitavuruga masuala ya urithi. Naikauliza, mimi kosa langu ni nini? Nikajibiwa kuwa kosa lako ni kuwa ‘‘kimbelembele’’.
Nikaondoka msibani nikiwa adui wa karibu kila mwana familia. Nikajilaumu sana.
Dada Msomali nilimjulisha kuwa mzazi mwenzake amefariki; akahaidi akipata muda atakuja kuhani msiba.
Miaka ikapita, nilikuwa nikiwasiliana na dada Msomali mara chache walau kujua maendeleo ya dogo.
Dogo alisoma mpaka kidato cha sita, baada ya hapo nikasikia kuwa anafanya biashara na ndugu zake masuala ya mafuta.
Na mimi nikaendelea na maisha yangu si unajua bongo ukilemaa unazeeka bila chochote.
Sasa mwaka jana napokea simu namba ngeni, napokea nakutana na sauti nzito baada ya salaam, akajitambulisha kuwa yeye ni mtoto wa anko, nikashtuka.
Akaniambia kwanza anataka kuona kaburi la baba yake na ikiwezekana na ndugu zake pia.
Nikakutana naye, kisha tukaanza safari kwenda kwa familia ya uncle maana alipozikwa ni karibu kabisa na nyumbani kwake.
Kwa kumuona tu japo bado kijana mdogo wa miaka 25 nikajua jamaa maisha yameenda vizuri, gari aliyokuwa anaendesha na mazungumzo kadhaa baada ya kumhoji anachofanya, maisha yapo vizuri.
Tukamaliza zoezi la yeye kuzuru kaburi la baba yake na kurudi.
Taarifa ikawafikia familia kwamba yule dogo mliyemkataa miaka 15 iliyopita amekuja na kwa kwa kweli anaonekana kuwa na maisha yake.
Simu ya kwanza ikatoka kwa shangazi, anauliza ni kweli habari anazosikia? Nikaona sasa ni wakati muafaka, nikamjibu sio kweli na sijui lolote kuhusu huyo kijana.
Nilichojifunza:
Maisha hayatabirikiMkiwa na mtoto/watoto nje ya ndoa wajulishemi watu kwa wazi
Mtoto wa nje ukikataliwa, usilazimishe
Samehe na endele na masiha yako.