H r n
JF-Expert Member
- Oct 3, 2019
- 1,100
- 2,079
Kuna jambo ambalo binafsi huwa linanikera sana; kuona mtu amevaa nguo lakini nguo za ndani zinaonekana wazi. Kwa upande wa wanawake, wengine huvaa nguo nyepesi au zinazobana kiasi kwamba chupi inaonekana kwa urahisi, naye anaona yupo sawa tu, na unakuta anakaa kwao anatoka mpaka ndugu zake wanamwona wala hajili au hata aibu halioni zamani huwezi kuta mama zetu wanavaa kama hivi vibinti vya 2004 huwezi kuta huu ujinga sijui wameutoa wapi.
Kwa upande wa wanaume, kuna wanaovaa suruali zilizoshuka hadi boxer kuonekana wazi wakiamini ni fasheni au mtindo wa kisasa. Boxer chenyewe sasa unakuta kichafu ops yaani kina rangi mbili wendawazimu tu unamwonyesha nani na ili iwaje nonsense.
Je, hii ni ishara ya kujiamini na kufuata mitindo ya mavazi ya sasa, au ni tabia inayopunguza heshima na staha katika jamii? Kwa maoni yenu, kuna tofauti kati ya fasheni na kuvaa kwa namna inayovutia umakini usio wa lazima?
Ningependa kusikia maoni yenu:
Kwa nini watu hufanya hivyo?
Je, mnadhani ni fasheni au kutafuta attention?
Kwenu ni jambo la kawaida au linawakera pia?