Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
- Thread starter
- #461
Mkuu Zomba, nilitembelea UN kama visiting journalist, na nadhani mimi ndie mwanahabari wa kwanza private kutoka nchini Tanzania kuripoti UN General Assembly mara 3, nikitokea New York. Waandishi wengine wote private wameanza kwenda na awamu ya JK. Journalist wote wanaoripoti GA wana full access na viongozi wote wa dunia hii kwa kuhudhuria press co zao au kufanya appointment. Mimi sikufanya appointment na yoyote!.Huyo alitembelea jengo la UN akaenda ofisi za ubalozi wa Tanzania UN.
Sasa fikiria kesi ya nyani uipeleke kwa ngedere.
Aseme UN alionana na nani zaidi ya maafisa ubalozi wa Tanzania? Katibu Mkuu wa UN? Naibu Katibu Mkuu UN? Baraza la Usalama wa UN? au alitembelea jengo la UN kama mtalii tu? (kuna program pale ya watalii wanaotembelea jengo la UN).
Jibu lake hapo utacheka.
Mwaka huu nitakwenda tena na this time nitairipotia JF, live from New York!.
NB. Sio huko tuu, pia ni mimi ndie niliyeiripotia JF process yote ya maridhiano nikitokea Baraza la Wawakilishi na nilizuiliwa na kutolewa nje ya baraza na ni yule yule dada yenu mliyemsingizia humu, aliyenisaidia nikaruhusiwa kuendelea kuutangaza muafaka!.(mseme tena nimewatukana!).
Ni mimi ndie niliyeutangaza ule ushindi wa CUF 1995, uliopelekea kituo changu kupigwa faini kwa kutangaza matokeo ya halali!.
Ni mimi ndie nilyepiga zile picha za vurugu za 1996, na nilishikwa kituo cha Mwembe Madema nikiwa na Ali Saleh na Mwandishi wa gazeti la Majira. Nikanyang'wa kamera ya DV, polisi wakaniambia niwaonyeshe picha nilizopiga, nikawaambia sijapiga picha!. Wakaichukua kamera kuipeleka TVZ, Mungu bariki, TVZ walikuwa bado wako VHS, DV hawajui, wakairudisha na kuthibitisha hakuna picha!. Nikafukuzwa Zanzibar under escort. Kufika bara, jioni mimi mwenyewe nikatangaza vurugu za Zanzibar na picha juu!. Ulimwengu ukaona!. Picha hizo zilipelekea Kituo cha DTV kupigwa marufuku Zanzibar!.
Pia ni mimi niliyetangaza zile vurugu za Mwembechai nikiwa in a line of fire!. Japo ni mwandishi wa habari, backround yangu ni jeshini, JWTZ kikosi cha Paratrouper!. Naombeni msiniulize kwanini niliondoka jeshini!.
Pia ni mimi nakuja kuwatangazia wana jf, maandimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, nikitokea uwanja wa Amani hapo Zanzibar!.
Pasco.
