Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
TUJIKUMBUSHE HISTORIA YA BAKWATA OCTOBER HADI DECEMBER 1968 SEHEMU YA KWANZA
"... ikadhihirika kuwa serikali ilikuwa imepania kuivunja EAMWS kwa kuwatumia Waislam wachache walioteuliwa kwa kazi hiyo.
Lengo likiwa ni kuanzisha taasisi mpya ambayo serikali itaweza kuiamuru.
Ieleweke hapa kuwa kama tulivyokwisha eleza hapo nyuma, serikali nzima ya Tanzania ilikuwa mikononi mwa Wakristo na watendaji hawa walikuwa wapo chini ya Kanisa.
Hii ilikuwa na maana kuwa kilichotakiwa kuwepo ilikuwa taasisi ya Kiislam ambayo Kanisa itaweza kuiamuru.
Hii ilikuwa ni jambo lazima lifanyike ili kuwadhibiti Waislam kama nguvu inayoweza kuleta mabadiliko ya siasa.
Baada ya kuelewa hali hii ndipo sasa tunaweza kuuangalia kile kilichoitwa ‘’mgogoro’’ wa EAMWS’’ ambao ulidumu kwa miezi mitatu ya mwisho ya mwaka wa 1968.
Ilituweze kuuelewa vyema kisa kizima cha ‘’mgogoro’’ ni muhimu kwanza kuelewa chanzo chake, hadhi za wahusika wakuu na nafasi zao katika ‘’mgogoro’’ ule.
Mwisho, ni muhimu kuweka bayana na kuchambua nafasi ya Julius Nyerere, serikali yake, chama cha TANU na vyombo vya dola katika ‘’mgogoro’’ ule.
Hii itasaidia kuelewa kama kweli ulikuwepo ‘’mgogoro’’ katika EAMWS, au ‘’mgogoro’’ ulibambikizwa na watu katika TANU, serikali na ndani ya Waislam wenyewe ili kuwadhoofisha Waislam kwa nia ya kuwa usije Uislam ukawa na nguvu katika Tanzania hivyo kuwawezesha Waislam kushika madaraka ya nchi."
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes 1998).