Miaka 55 ya BAKWATA: Tujikumbushe Historia Yake na Yaliyotokea October - December 1968

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
TUJIKUMBUSHE HISTORIA YA BAKWATA OCTOBER HADI DECEMBER 1968 SEHEMU YA KWANZA

"... ikadhihirika kuwa serikali ilikuwa imepania kuivunja EAMWS kwa kuwatumia Waislam wachache walioteuliwa kwa kazi hiyo.

Lengo likiwa ni kuanzisha taasisi mpya ambayo serikali itaweza kuiamuru.

Ieleweke hapa kuwa kama tulivyokwisha eleza hapo nyuma, serikali nzima ya Tanzania ilikuwa mikononi mwa Wakristo na watendaji hawa walikuwa wapo chini ya Kanisa.

Hii ilikuwa na maana kuwa kilichotakiwa kuwepo ilikuwa taasisi ya Kiislam ambayo Kanisa itaweza kuiamuru.

Hii ilikuwa ni jambo lazima lifanyike ili kuwadhibiti Waislam kama nguvu inayoweza kuleta mabadiliko ya siasa.

Baada ya kuelewa hali hii ndipo sasa tunaweza kuuangalia kile kilichoitwa ‘’mgogoro’’ wa EAMWS’’ ambao ulidumu kwa miezi mitatu ya mwisho ya mwaka wa 1968.

Ilituweze kuuelewa vyema kisa kizima cha ‘’mgogoro’’ ni muhimu kwanza kuelewa chanzo chake, hadhi za wahusika wakuu na nafasi zao katika ‘’mgogoro’’ ule.

Mwisho, ni muhimu kuweka bayana na kuchambua nafasi ya Julius Nyerere, serikali yake, chama cha TANU na vyombo vya dola katika ‘’mgogoro’’ ule.

Hii itasaidia kuelewa kama kweli ulikuwepo ‘’mgogoro’’ katika EAMWS, au ‘’mgogoro’’ ulibambikizwa na watu katika TANU, serikali na ndani ya Waislam wenyewe ili kuwadhoofisha Waislam kwa nia ya kuwa usije Uislam ukawa na nguvu katika Tanzania hivyo kuwawezesha Waislam kushika madaraka ya nchi."

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes 1998).

1702871878997.png
 
Kila La Heri Sana Bakwata Ikiwapendeza Ivunjwe Kiundwe Chombo Kipya Kitakachoondoa Mivutano
 
Kwahiyo mlitaka muiamuru serikali,we mzee kubwa jinga kabisa,
Ndugu yangu siyo vizuri hivi. Huyu mzee anaweza kuwa babako mzazi kabisa. Kuna ulazima gani kumtukana hivi? Ni kosa gani kafanya hapo mbali na kupigania Uislamu wake ambalo hasa huwa ndiyo lengo kuu la asilimia 99.99 ya maandishi yake humu? Hatujuani humu ndiyo lakini tujitahidi sana tuwe na utu na ubinadamu. Umenisikitisha sana!
 
Ndugu yangu siyo vizuri hivi. Huyu mzee anaweza kuwa babako mzazi kabisa. Kuna ulazima gani kumtukana hivi? Ni kosa gani kafanya hapo?Hatujuani humu ndiyo lakini tujitahidi sana tuwe na utu na ubinadamu. Umenisikitisha sana!

Mkuu hoja za mzee zimejaa aibu na matusi dhidi ya umoja na amani ya nchi hii,hujui ni madhara gani au ni malengo gani makubwa aliyonayo huyu mzee dhidi ya umoja na amani ya nchi hii,anataka kuleta utengano na chuki za kidini baina ya watanzania.

Sio wa kuvumilia wala wa kuchekea,tunamjibu mpumbafu sawa na upumbafu wake

Hata hekima na maarifa sio umri,kuna wazee wajinga na wapumbafu pia.
 
TUJIKUMBUSHE HISTORIA YA BAKWATA OCTOBER HADI DECEMBER 1968 SEHEMU YA KWANZA

"... ikadhihirika kuwa serikali ilikuwa imepania kuivunja EAMWS kwa kuwatumia Waislam wachache walioteuliwa kwa kazi hiyo.

Lengo likiwa ni kuanzisha taasisi mpya ambayo serikali itaweza kuiamuru.

Ieleweke hapa kuwa kama tulivyokwisha eleza hapo nyuma, serikali nzima ya Tanzania ilikuwa mikononi mwa Wakristo na watendaji hawa walikuwa wapo chini ya Kanisa.

Hii ilikuwa na maana kuwa kilichotakiwa kuwepo ilikuwa taasisi ya Kiislam ambayo Kanisa itaweza kuiamuru.

Hii ilikuwa ni jambo lazima lifanyike ili kuwadhibiti Waislam kama nguvu inayoweza kuleta mabadiliko ya siasa.

Baada ya kuelewa hali hii ndipo sasa tunaweza kuuangalia kile kilichoitwa ‘’mgogoro’’ wa EAMWS’’ ambao ulidumu kwa miezi mitatu ya mwisho ya mwaka wa 1968.

Ilituweze kuuelewa vyema kisa kizima cha ‘’mgogoro’’ ni muhimu kwanza kuelewa chanzo chake, hadhi za wahusika wakuu na nafasi zao katika ‘’mgogoro’’ ule.

Mwisho, ni muhimu kuweka bayana na kuchambua nafasi ya Julius Nyerere, serikali yake, chama cha TANU na vyombo vya dola katika ‘’mgogoro’’ ule.

Hii itasaidia kuelewa kama kweli ulikuwepo ‘’mgogoro’’ katika EAMWS, au ‘’mgogoro’’ ulibambikizwa na watu katika TANU, serikali na ndani ya Waislam wenyewe ili kuwadhoofisha Waislam kwa nia ya kuwa usije Uislam ukawa na nguvu katika Tanzania hivyo kuwawezesha Waislam kushika madaraka ya nchi."

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes 1998).

waislamu huwa hawana asili ya amani wala msijali tunajua harakati zenu mwisho mnataka Tz pawe syria ili mtimize maandiko ya hayati muarabu muamedi

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo mlitaka muiamuru serikali,we mzee kubwa jinga kabisa,
hii Sio sawa hata Kidogo na haikubaliki kwa Kaka Yangu Mohamedi said
Mkuu hoja za mzee zimejaa aibu na matusi dhidi ya umoja na amani ya nchi hii,hujui ni madhara gani au ni malengo gani makubwa aliyonayo huyu mzee dhidi ya umoja na amani ya nchi hii,anataka kuleta utengano na chuki za kidini baina ya watanzania.

Sio wa kuvumilia wala wa kuchekea,tunamjibu mpumbafu sawa na upumbafu wake

Hata hekima na maarifa sio umri,kuna wazee wajinga na wapumbafu pia.
Mkuu Jiwe angavu!
samahani sana!
Ila kwa ulivyoandika tu najua kuwa Mzee Said sio tu anaweza kuwa baba ako ila kwa umri wako huyo ni babu yako..

Sijaona kosa lake hata moja ila naona makosa yako kumkosoa wakati ambapo anaeleza Ukweli uliokuwepo..

Kuna wakati Tuwe na uvumilivu wa kusikia Yale yanayotuumiza Na ndiyo nchi zenye maendeleo hufanya hivyo kuna wakati huamua hata mambo wasiyoyapenda ili tu..Wananchi wao wapate ustawi...

Alethophobia naona inakua sana kwa kasi kwa kizazi hichi watu wengi sana wanaogopa kuupokea Ukweli,Maana wanahisi ukweli unawaumiza..

Lakini hawajui kuwa ukweli sio kuumiza tu bali unaponya Jitahidi kuwa na Ustahimilivu kwenye hoja za mwenzako utakuwa Bora zaidi..
 
Dr. Mambo,
Ahsante sana.

Nimeongeza uzi mwingine kuhusu historia ya BAKWATA.
Hiyo ni sehemu ya pili.

Ahsante kwa kunifunza somo jipya: "Alethophobia."
A fear or dislike of the truth

Noun. alethophobia (uncountable) (psychology) A fear or dislike of the truth; an unwillingness to come to terms with truth or facts.
 
Shukrani pia kaka kwa bandiko zako nazipenda sana!
 
Maalim tuendelee, leta nondo kuhusu EAMWS na hicho kibakwata.
Jabulani,

BAKWATA imekataliwa toka siku ya kwanza 1968.

Kote serikali ilipopita katika majimbo kujaribu kufufua ofisi za EAMWS ziwe za BAKWATA serikali ilifanikiwa baada ya matumizi ya fedha nyingi (siwezi kuandika neno lenyewe).

Kazi hii ikifanywa na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Geoffrey Sawaya.

Tabora viongozi wa BAKWATA wamezomewa katika mkutano wa hadhara mbele ya Mkuu wa Mkoa.

Hii ndiyo historia ya BAKWATA.

Waislam wameikataa BAKWATA hadi Rais Ali Hassan Mwinyi alipowaruhusu Waislam kusajili taasisi zao kwa maendeleo yao.

Haya yote yamo katika kitabu cha Abdul Sykes na mpasha habari wangu ni marehemu Bilal Rehani Waikela aliyekuwa Katibu wa EAMWS, Western Province.

Historia hii nimeieleza kwenye kitabu cha Abdul Sykes.

BAKWATA haina heshima machoni mwa Waislam wengi.

Sioni vipi Islamic Foundation Morogoro au Ansar Muslim Youth Tanga ikiwa chini ya BAKWATA.

Huu ni muhali mkubwa sana.

Mzee Waikela anasema kama si kutaka kujenga Chuo Kikuu EAMWS ingekuwapo hadi leo.

BAKWATA haijapata hata siku moja kusema kuwa EAMWS ilikuwa inajenga Chuo Kikuu.

BAKWATA hata siku moja haijapata kueleza historia ya Mufti Sheikh Hassan bin Ameir katika medani ya siasa kupigania uhuru wa Tanganyika au katika kuutangaza Uislam Tanganyika, Nyasaland, Rwanda, Burundi na Congo.

BAKWATA inaogopa historia ya Sheikh Hassan bin Ameir.
 
BAKWATA ndio taasisi ya kiislamu yenye nguvu na umoja kuppita zote. Hizo taasisi nyingine ziko kwa maslahi ya watu wachache
Laki...

Nakuwekea makala hapo chini huenda ikakusaidia katika kuujua ukweli:

Tarehe 28 Aprili, 1993 tukio la ajabu lilifanyika.

Katika hali ya kukata tamaa na katika jitihada zake za kuinusuru BAKWATA Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Naibu Waziri Mkuu Augustine Mrema aliitisha kikao kati ya Waislamu na Wakristo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Ajenda haikuelezwa.

Kanisa lilituma ujumbe wenye nguvu.

Viongozi wa Waislamu nje ya BAKWATA hawakuitikia huu mwito ila BAKWATA wenyewe.

Waislamu wachache waliojitokeza walikuwa pale kwa udadisi hawakuwa na imani kwamba mkutano huo ungezaa matunda.

Wakati wa kutambulishwa kati ya pande hizo mbili ulipofika, Waislamu hawakuwa na viongozi wa kupeana mkono na viongozi wa Kanisa.

Mrema alihutubia mkutano huo akabainisha kuwa uchaguzi wa BAKWATA ulikuwa umepitwa na wakati na hauwezi kufanyika kwa sababu ya BAKWATA haina fedha.

Kanisa lilijitolea kutoa fedha kuipa BAKWATA ili iweze kuitisha wajumbe wake na kufanya uchaguzi.

Augustine Mrema pia alisaidia kukusanya fedha kutoka kwa wafanyabiashara ili kufadhili uchaguzi huu wa BAKWATA.

BAKWATA ikakutana Dodoma kuanzia tarehe 10-12 Mei mgeni rasmi akiwa Augustine Mrema.

Badala ya kufanya uchaguzi BAKWATA ilipitisha baadhi ya mabadiliko ya katiba ili kumpa Mufti Mkuu Sheikh Hemed bin Hemed mamlaka kamili ya kumfukuza mtendaji yeyote wa BAKWATA bila kuwajibika kwa mtu yeyote.

Wakati haya yakiendelea Waislam walikuwa wanafutilia usajili wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania.

Serikali ilisajili Baraza Kuu hili bila kupenda na kwa shingo upande.

Ingawa Baraza hili linaungwa mkono na Waislamu walio wengi, serikali bado inakataa kulitambua na inaendelea kuweka kuunga mkono BAKWATA.

Katika kukabiliana na hili Waislamu kwa upande wao wamekataa kuitambua BAKWATA.

Kwa miaka 55 sasa tangu BAKWATA ilipoundwa na serikali mwaka 1968 msuguano kati ya Waislamu kwa upande mmoja na BAKWATA na serikali kwa upande mwingine unaendelea.
 
Bado hauko sahihi, waislamu wengi wana iunga mkono BAKWATA, nenda kwenye ofisi za BAKWATA Temeke uone zilivyofurika waislsmu kwa ajili ya matatizo yao ya ndoa na mirathi, hakuna taasisi ya waislamu yenye nguvu zaidi ya BAKWATA, usipindishe ukweli
 
TUJIKUMBUSHE HISTORIA YA BAKWATA OCTOBER HADI DECEMBER 1968 SEHEMU YA KWANZA

"... ikadhihirika kuwa serikali ilikuwa imepania kuivunja EAMWS kwa kuwatumia Waislam wachache walioteuliwa kwa kazi hiyo.

Lengo likiwa ni kuanzisha taasisi mpya ambayo serikali itaweza kuiamuru.

Ieleweke hapa kuwa kama tulivyokwisha eleza hapo nyuma, serikali nzima ya Tanzania ilikuwa mikononi mwa Wakristo na watendaji hawa walikuwa wapo chini ya Kanisa.

Hii ilikuwa na maana kuwa kilichotakiwa kuwepo ilikuwa taasisi ya Kiislam ambayo Kanisa itaweza kuiamuru.

Hii ilikuwa ni jambo lazima lifanyike ili kuwadhibiti Waislam kama nguvu inayoweza kuleta mabadiliko ya siasa.

Baada ya kuelewa hali hii ndipo sasa tunaweza kuuangalia kile kilichoitwa ‘’mgogoro’’ wa EAMWS’’ ambao ulidumu kwa miezi mitatu ya mwisho ya mwaka wa 1968.

Ilituweze kuuelewa vyema kisa kizima cha ‘’mgogoro’’ ni muhimu kwanza kuelewa chanzo chake, hadhi za wahusika wakuu na nafasi zao katika ‘’mgogoro’’ ule.

Mwisho, ni muhimu kuweka bayana na kuchambua nafasi ya Julius Nyerere, serikali yake, chama cha TANU na vyombo vya dola katika ‘’mgogoro’’ ule.

Hii itasaidia kuelewa kama kweli ulikuwepo ‘’mgogoro’’ katika EAMWS, au ‘’mgogoro’’ ulibambikizwa na watu katika TANU, serikali na ndani ya Waislam wenyewe ili kuwadhoofisha Waislam kwa nia ya kuwa usije Uislam ukawa na nguvu katika Tanzania hivyo kuwawezesha Waislam kushika madaraka ya nchi."

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes 1998).

Balukta ndio suluhisho la matatizo ya Waislamu
 
Back
Top Bottom