Miaka 55 ya BAKWATA: Tujikumbushe Historia Yake na Yaliyotokea October - December 1968

Tunaweza kupata source nyingine tofauti na mtazamo wa wenzio.
Kwamba serikali izuie taasisi kujenga chuo?
Kweli?
Nan...
Kupata chanzo kingine cha kwa nini EAMWS ilivunjwa na kwa nini serikali ilikataa kutoa kibali OIC kujenga Chuo Kikuu Tanzania ni lazima sasa serikali yenyewe itoe majibu.

Wakati Jopo la Prof, Shivji wanaandika historia ya Mwalimu Nyerere walikuja nyumbani kwangu mara mbili kunihoji.

Waliniuliza mengi kuhusu Mwalimu Nyerere na mimi niliwaeleza kila kitu.

Kilipotoka kitabu ikaandikwa kuwa EAMWS haikuwa inajenga Chuo Kikuu bali walikuwa wanajenga Islamic Centre.

Na yako mengine mengi nimewaeleza hivi wakaandika vile.

1703590865133.png

Kulia: Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Yahya Othman na Dr.
Ng'waza Kamata

Stux...
Hakuna sababu ya kunitukana.
Hivyo utavuruga mjadala.

Tunaweza tukafanya mjadala wa heshima na adabu.

Huu mkutano wa Aga Khan haukuwa kati yake na EAMWS na BAKWATA.

Kikao hichi kilikuwa kati ya Aga Khan na BAKWATA.

Rejea ondoa ghadhabu katika kifua chako na usome upya.

EAMWS ilishapigwa marufuku na Tewa Said Tewa alialikwa kama kiongozi wa zamani wa EAMWS.
Tofauti iko wapi sasa? Kama Tewa Said Tewa alihudhuria kuwakilisha iliyokuwa EAMWS?

Ndiyo maana nakuambia wewe ni mwanaharakati wa Kiislamu. Haya mambo hatuyataki Tanzania, nenda Somalia au Afghanistan ukajipime nao
 
Stux...
Cambridge Journal of African History haichapi mapitio ya vitabu vya riwaya.

Inawezekana wewe unataabika na ukweli lakini walimu wa historia ya Afrika vyuo vingi wanaposomesha historia ya utaifa wa Tanganyika huanza na Kleist Sykes na Dr. Kwegyr Aggrey mwaka wa 1924.

Hapa huwaelekeza wanafunzi kusoma maisha ya wazalendo hawa wawili katika Dictionary of African Biography (Oxford University Press New York 2011) kisha huwaelekeza pia kusoma, Modern Tanzanians, (Tanzania Publishing House, Dar es Salaam 1973) kitabu alichohariri John Iliffe wasome, ''The Townsman Kleist Sykes,'' mwandishi Aisha ''Daisy'' Sykes.

(Unaweza kusoma historia hii Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam East Africana: ''The Life of Kleist Sykes,'' Ref. No. JAN/HIST/143/15).

KIsha anawapa rejea ya kitabu cha Abdul Sykes (1998) wasome.

Hakuna mwalimu atakaegusa Historia ya TANU ya Kivukoni na vitabu vingine labda kwa kupita kuwaonyesha wanafunzi umuhimu wa kuandika ''Corrective History.''

Kuna mengine unayoandika nayanyamazia kwa kuwa si maudhui ya mjadala wetu.

Kwa hiyo hivyo vitabu viko kwenye mtaala wa elimu wa Tanzania?
 
Wacha jazba mzee wangu.Historia ya Tanzania imeandikwa na iko sahihi.Tatizo lako ni kutazama.kila kitu katika miwani ya Uislamu.
Unataka kuwa na hati miliki ya ukweli kuhusu Uhuru wa nchi yetu.Acha ushamba
Nan...
Hapana sina hamaki.
Ushahidi kuwa sighadhibiki unao hala mbele ya macho yako.

Ninaetukanwa ni mimi mimi situkani mtu.
Ukiniuliza swali nitakujibu kadri ya ufahamu wangu.

Umesema kweli naandika historia ya Waislam katika uhuru wa Tanganyika.

Ikiwa nisingefanya hivyo leo tungekuwa hakuna historia ya kweli si ya Julius Nyerere wala ya chama cha TANU.

Mimi nitakuwaje mshamba ilhali nimezaliwa Mtaa wa Kipata?

1703591363646.png

Trafalgar Square, London
 
Tofauti iko wapi sasa? Kama Tewa Said Tewa alihudhuria kuwakilisha iliyokuwa EAMWS?

Ndiyo maana nakuambia wewe ni mwanaharakati wa Kiislamu. Haya mambo hatuyataki Tanzania, nenda Somalia au Afghanistan ukajipime nao
Stux...
Ikiwa hizo ni fikra zako mimi lazima nikubali kughitilafiana na wewe.

Isemee nafsi yako kuwa hupendi historia hii niandikayo usiwesemee wengine.

Hapa nina wasomaji wengi na nimepewa hadi cheti kwa Uandishi Bora katika Jukwaa la Historia:

1703591671510.png

1703591728914.jpeg
 
Kwa hiyo hivyo vitabu viko kwenye mtaala wa elimu wa Tanzania?
Stux...
Hapana haviko katika mtaala.

Kitabu hicho hapo chini: ''The Torch on Kilimanjaro,'' kilichapwa na Oxford Unversity Press, Nairobi 2007 wakitegemea kitawekwa katika mtaala wa kusomesha historia na Kiingereza katika shule za msingi Tanzania.

Hili halikuwa.

Kitabu hiki kinasomeshwa Kenya, Uganda na kwengineko ila hapa nyumbani.

Kinakwenda toleo la tatu In Shaa Allah.

1703592389945.png

Toleo la Pili

Stux...
Ikiwa hizo ni fikra zako mimi lazima nikubali kughitilafiana na wewe.
Isemee nafsi yako kuwa hupendi historia hii niandikayo usiwesemee wengine.

Hapa nina wasomaji wengi na nimepewa hadi cheti kwa Uandishi Bora katika Jukwaa la Historia:

JF imetambua uandishi wako tu. Usipotoshe!! JF haijasema kuwa unayoandika ni ya kweli.

Hata hivyo policy ya JF ni "user generated ckntent". Haiwahusu whether kuna uwongo
 
Mkuu hoja za mzee zimejaa aibu na matusi dhidi ya umoja na amani ya nchi hii,hujui ni madhara gani au ni malengo gani makubwa aliyonayo huyu mzee dhidi ya umoja na amani ya nchi hii,anataka kuleta utengano na chuki za kidini baina ya watanzania.

Sio wa kuvumilia wala wa kuchekea,tunamjibu mpumbafu sawa na upumbafu wake

Hata hekima na maarifa sio umri,kuna wazee wajinga na wapumbafu pia.
huyu mzee ana mawazo ya kuigawa nchi kidini na vta ya kidini ni mbaya sana huyu mzee ni gadi tu anapandikiza chuki mda wte
 
Tofauti iko wapi sasa? Kama Tewa Said Tewa alihudhuria kuwakilisha iliyokuwa EAMWS?

Ndiyo maana nakuambia wewe ni mwanaharakati wa Kiislamu. Haya mambo hatuyataki Tanzania, nenda Somalia au Afghanistan ukajipime nao
mwambie mkuu.watu km hawa wakipita balabalan wakaona watu wana aman wanajiskia vbaya wanataman wachinje mtu huku wakisema allah akbar
 
Stunex,
Mimi silalamiki na laiti ningekuwa hivyo ningepata sifa ya ulalamishi.

Mimi nina heshima yangu katika utafiti wa historia ya Tanzania.

Kitabu nilichoandika cha Abdul Sykes kimebadilisha historia ya Julius Nyerere na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Utafiti wa tatizo la elimu kwa Waislam limeonyesha yale ambayo waliokuwa wakifanya hujuma wamefahamika.

Nimeweka Research Papers hapa nilizowasilisha vyuo vikuu ndani na nje ya mipaka yetu bahati mbaya hajatokea mtu kati yenu aliyetaka kujadili paper hizi.

Kilicho chepesi kwenu ni uandishi wa jeuri na kejeli.

Stunex,
Mohamed Said kalamu yake haijadhalilisha Uislam.

Picha kutoka Maktaba yake zimethibitisha ukweli wa aandikayo.

Nimekuwekeeni hapa video clips mtazame.

Jukwaa zima likawa kimya.

Nimekuwekeeni clip hapa nazungumza Ikwiriri katika Bibi Titi Festival mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa naeleza yaliyotokea nyumbani kwa Ally Sykes Mtaa wa Kipata Nyerere alipokwenda kutoa taarifa kuwa Waingereza wamekataa kusajili TANU kwa kisingizio kuwa chama hakina wanachama.

Hiki kilikuwa kikao cha watu wanne siku ile: Mama mwenye nyumba Bi. Zainab mke wa Ally Sykes. Huyu Ally Sykes kadi yake ya TANU No. 2, Abdul Sykes kadi ya TANU No. 3 na Julius Nyerere kadi ya TANU No. 1 ya Territorial President wa TANU.

Katika kikao hiki cha kujadili usajili wa TANU nikamleta Said Chamwenyewe.

Huyu ndiye Mohamed Said.

Waziri Mkuu alipozungumza kufunga Bibi Titi Festival alisema historia ya kweli isomeshwe wanafunzi wawajue wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Shida yako ni kutaka kuuaminisha umma kuwa uli chokitafiti wewe kuhusu historia ya Tanganyika ni cha kweli kuliko cha watafiti wengine
 
JF imetambua uandishi wako tu. Usipotoshe!! JF haijasema kuwa unayoandika ni ya kweli.

Hata hivyo policy ya JF ni "user generated ckntent". Haiwahusu whether kuna uwongo
Stux...
Hakika JF haithibitishi ukweli wa niandikayo ila wametambua uzito wa makala zangu.

Kwa miaka mingi watu walisomeshwa historia isiyokuwa na ukweli na wakaiamini.

Mimi nimekuleteeni historia ya Mwalimu Nyerere na harakati za kuunda TANU kutoka Nyaraka za Sykes zinazokwenda nyuma hadi 1924 Kwegyir Aggrey alipokutana na Kleist akamshauri aunde African Association.

Kleist baba muasisi wa African Association watoto Abdul, Ally na Abbas viongozi wa TAA na waasisi wa TANU 1954.
 
Shida yako ni kutaka kuuaminisha umma kuwa uli chokitafiti wewe kuhusu historia ya Tanganyika ni cha kweli kuliko cha watafiti wengine
Nan...
Ukweli wa niliyoandika utaamuliwa na nyie wasomaji.

Lakini kaa ukijua kuwa kitabu changu kimevunja rekodi ya kitabu cha Chuo Cha CCM Kivukoni na kitabu cha Abubakar Ulotu kuhusu historia ya TANU.

Vitabu hivyo vyote vimekufa.
Kitabu changu kinakwenda toleo la tano.

Elewa hakuna mtafiti yeyote hadi leo aliyefunuliwa Nyaraka za Sykes ila mimi.
 
huyu mzee ana mawazo ya kuigawa nchi kidini na vta ya kidini ni mbaya sana huyu mzee ni gadi tu anapandikiza chuki mda wte

TUJIKUMBUSHE

Waislam wa Tanzania na Tatizo la Udini Katika Wizara ya Elimu.

Ndugu Waziri,
Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na maswali mengi wakijiuliza Waislamu, moja likiwa inakuwaje katika maeneo yenye Waislamu wengi ambapo idadi ya wanafunzi Waislamu inakuwa zaidi ya asilimia 70, lakini wanapochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya watoto wa Kiislamu huporomoka na kuwa chini ya asilimia 20.

Swali na kitendawili hiki kimekuwepo kwa muda mrefu bila kupatiwa majibu.

Hata lilipofikishwa Bungeni mwaka 1999 na aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni, Mzee Kitwana Selemani Kondo, bado halikupatiwa jibu.

Akihoji juu hali hiyo, Mzee Kitwana Kondo alitoa mfano jinsi hali ilivyokuwa katika shule ya Pembamnazi iliyokuwa na Waislamu watupu na kwa miaka mingi mfululizo kulikuwa hakuna hata mtoto mmoja aliyekuwa akichaguliwa kwenda sekondari kutoka katika shule hiyo.

Aidha alisema kuwa, katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watoto wa Kiislamu katika shule za msingi ilikuwa zaidi ya asilimia 70 lakini inapokuja kuchaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Waislamu iliporomoka na kuwa chini ya asilimia 20.

Akizungumza Bungeni tarehe 2 Februari, 1999 alisema kuwa katika watoto waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka 1998, idadi ya Waislamu ilikuwa asilimia 71 na Wakristo 29%. Hata hivyo akasema, ilipotoka orodha ya waliochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Wakristo ikawa asilimia 79 (79%) na Waislamu 21%.

Je, hiyo ilikuwa na maana kuwa watoto wa Kiislamu kwa asili yao hawana akili?

Alitaka kujua Mzee Kitwana Kondo. Lakini hakuweza kupata jibu.

Mheshimiwa Waziri,
Ni wazi kuwa Waziri wa Elimu au Waziri Mkuu ambaye ndiye msimamizi wa mambo ya serikali Bungeni asingeweza kutoa majibu ya uhakika kwa sababu swali lilihitaji kufanyika uchunguzi huru wa kina na makini kwanza.

Mheshimiwa Waziri,
Mwaka 1987 aliyekuwa Waziri wa Elimu, Profesa Kighoma Ali Malima, aliweka utaratibu mpya wa ufanyaji wa mtihani wa darasa la saba ambapo namba zilitumika toka kufanya mtihani, kusahihisha na kuchagua wanafunzi wa kwenda kidato cha kwanza.

Namba zilivishwa majina baada ya taratibu zote hizo kukamilika. Mwaka huo idadi ya watoto wa Kiislamu waliokwenda kidato cha kwanza iliongezeka kwa asilimia 40 ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Hata hivyo, mara aliondolewa Waziri Malima katika wizara hiyo na utaratibu wa zamani ukarejeshwa ambapo yalikuwa yakichaguliwa majina na idadi ya Waislamu ikaporomoka na kurudi chini ya asilimia 20.

Mheshimiwa Waziri,
Hali kama hii hapana shaka inazua maswali mengi ambayo yanahitaji majibu na majibu hayo hayawezi kupatikana bila ya kufanyika uchunguzi.

Labda tuongeze mifano ili kuliweka wazi zaidi jambo hili.

Mwaka 1983 mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Kopa Abdallah akisoma katika shule ya msingi Kichangani, Kilosa, alikosa kuchaguliwa kwenda sekondari.

Yeye binafsi, wazazi wake na hata walimu wake hawakuamini matokeo yale kutokana na alivyokuwa akifanya vizuri kuliko wanafunzi wote.

Baadae ilikuja kugundulika kuwa nafasi yake alipewa mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Antoni Samirani ambaye alikuwa na uwezo mdogo sana ikilinganiswa na Abdallah.

Kilichofanyika ni kuwa jina la Abdallah lilifichwa na baadae Antoni akapewa jina hilo kimya kimya na kwenda kusoma sekondari akitumia jina Abdallah wakati yeye ni Antoni.

Taarifa zinasema kuwa Kopa Abdallah alipogundua hakuweza kufanya kitu akaishia kuwa dereva.

Hali kama hiyo ilimkuta pia Adam Ramadhani aliyekuwa akisoma shule ya msingi Rutihinda jijini Dar es Salaam na kumaliza darasa la saba mwaka 1999. Yalipotoka matokeo ya mtihani wa darasa la saba na kuonekana kuwa Adam hakuchaguliwa, baba yake hakuamini kuwa mtoto wake anaweza kufeli kutokana na uwezo aliokuwa nao na zaidi akitizama walivyochaguliwa watoto ambao Adam alikuwa mwalimu wao shuleni na mitaani.

Katika kufuatilia suala hilo wizarani, ilikuwa aibu kwa wizara baada ya kuonekana kuwa walichaguliwa watoto wa Kikristo wenye alama za chini kabisa huku akiachwa Adam Ramadhani aliyekuwa na alama za juu kuliko wote.

Mheshimiwa Waziri,
Mifano kama hii ni mingi mno na ipo katika ngazi zote kwa maana kutoka elimu ya msingi kwenda sekondari, kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano na kutoka kidato cha sita kwenda Chuo Kikuu.

Kwamba hata kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano, wapo watu waliopata kushuhudia majina ya wanafunzi wa Kiislamu yakiwekwa pembeni japo walikuwa na sifa za kuchaguliwa.

Mheshimiwa Waziri,
Ukiacha hujuma katika kuwaacha wanafunzi Waislamu wenye sifa kuendelea na masomo, matatizo huanzia kwenye kuamua nani amefaulu na nani kafeli.

Tuhuma zilizopo ni kuwa wapo wanafunzi wanapewa madaraja ya juu wakati alama zao ni za chini na wapo wanaopewa madaraja ya chini wakati alama zao ni za juu.

Na hii ni kwa masomo yote.

Mheshimiwa Waziri,
Kumekuwa na utamaduni katika nchi hii wa kukataa ukweli.

Kufuatia uchunguzi uliofanywa na Kamati za Bunge, tumeshuhudia wizi na ufisadi wa kutisha ukifichuliwa Bungeni hivi karibuni hali iliyopelekea mpaka Mheshimiwa Rais kubadili Baraza lake la Mawaziri.

Sasa baada ya kuyasema yote hayo, tunasema kuwa Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likilalamikiwa kwa zaidi ya miaka 30, lakini malalamiko hayo yamekuwa yakipokewa kwa sikio la uziwi.

Imefikia mahali tunasema kuwa hatuna tena imani na Baraza hilo.

Mheshimiwa Waziri,
Ili kupata ukweli wa malalamiko na shutuma hizi, na ili kujibu lile swali juu ya watoto wa Kiislamu ambalo halikupata jibu Bungeni, tunaitaka serikali kufanya yafuatayo:

1. Tume huru iundwe kuchunguza Baraza la Mitihani la Tanzania na utendaji wake kazi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.

2. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA) ajiuzulu mara moja ili kulinda heshima ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaani na Baraza la Mitihani.

Watendaji wakuu wa kitengo cha mitihani na wanaohusika na mfumo wa Kumputa ya Baraza la Mitihani nao wawajibishwe mara moja.

3. Hatua za kisheria na kibinadamu zichukuliwe dhidi ya watumishi wa Baraza la Mitihani watakaothibitika kuhusika na kashfa hii.

4. Muundo wa Baraza la Mitihani uzingatie uwiano wa kidini, kitendo cha chombo nyeti kama hiki kujazana watu wa dini moja kunaliondolea Baraza la Mitihani sura ya kitaifa, kwani takwimu zinaonyesha Makatibu Wakuu Watendaji na Manaibu Katibu Wakuu wamekuwa Wakristo na Wenyeviti wa Baraza hilo ni Wakristo tangu lilipoanzishwa mwaka 1973, mpaka hii leo na takwimu tunazo.

Mheshimiwa Waziri,
Tunaomba ieleweke kuwa tunachotaka ni kupatikana haki na kufanyika uadilifu kwa watu wote.

Hatudai wala hatutaki upendeleo kwa Waislamu na wala hatutaki kuona mtu yeyote anaonewa au kuporwa haki yake, awe Mwislamu au mtu wa dini nyingine.

Tunachoamini ni kuwa kama Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haina cha kuficha, basi itaunda Tume hiyo kwa haraka na kuhakikisha kuwa ni Tume ya kuaminika itakayofanya kazi yake kwa umakini, kwa kina na kwa uadilifu wa hali ya juu kabisa.

Lakini kama Wizara yako itaona kuwa haiwezi kuunda Tume ya uchunguzi, tunacho kuhakikishia ni kuwa sisi tutafanya kila liwezekanalo na kwa namna yoyote kuhakikisha kuwa Tume hiyo inaundwa.

Na ikigundulika kuwa kuna hujuma zinafanyika katika utendaji wa Baraza, basi itabidi uwajibikaji uanze kwenye Wizara kabla ya kuwawajibisha watendaji wa Baraza la Mitihani.

Ni imani yetu kuwa utayapokea madai ya Waislamu na kuyafanyia kazi kwa umakini na kwa haraka ili kujenga mustakbali mwema wa nchi hii na watu wake.

Tunaomba kuwasilisha,

Mwenyekiti,
Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
 
Shida yako ni kutaka kuuaminisha umma kuwa uli chokitafiti wewe kuhusu historia ya Tanganyika ni cha kweli kuliko cha watafiti wengine
Nan...
Sina shida ya hilo.

Kitabu changu kimechapwa mara nne kuanzia 1998 kilipotoka hadi leo.

Kitabu hiki kwa miaka 25 kinajadiliwa na hapa JF tunakijadili toka mwaka 2008.

Nimealikwa vyuo vingi kuzungumza kuhusu historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Sijaona hivyo vitabu vya watafiti wengine.

Hebu nifahamishe hivyo vitabu.
 
Kuna sababu gani ya kuchanganya serikali na dini?
Tuiache serikali isimame yenyewe bila dini na watu wake ndiyo wahangaike na dini zao kwa ustawi wa taifa
Mzee anamix sana mambo,maandikl yake mazuri tu katika historia,
Udini sasa
 
Babu...
Tulia usome hayo hapo chini kisha rejea unifahamishe fikra zako katika hili suala la udini:

Back
Top Bottom