Miaka 63 baba mdogo hajawahi kurudi nyumbani

Kila mtu anawajibika kwa maisha yake, hao uliowaacha kijijini nao waendelee na maisha yao, tatizo letu ni fikra za ujamaa ndio bado zinatufanya hata kuondoka nyumbani tulikozaliwa kuona ni tatizo.
Hata wanyama hulea watoto, lakini wakikua basi huwaacha wajitegemee.
Ndugu sio jukumu lako, ni fikra tu.
 
Mleta mada umesababisha nimemkumbuka marehemu mama yangu, nimeumia sana.

Mama alikua anamuongelea sana mdogo wake alieondoka mwaka 1980, alielekea Arusha toka hapo ikawa ni habari za kusikia tu yuko Mirerani ila hakuwahi kurudi.

Nimewahi kwenda Mirerani kumtafta mara kadhaa sijawahi kumpata. Kuna kipindi nilipewa clue zilizoonyesha kama ni yeye huko Mbuguni lakini nikaambulia patupu.

Ilikua kila nikienda Arusha mama anasema kamuulizie mjomba wako, anajaribu kumuelezea alivyo. Jamaa hajawahi kupatikana hadi mama amefariki. Bibi alifariki 1995 wala jamaa hakutokea.

Mshikaji alikua mwanajeshi, baada ya vita ya Uganda aliporudi tu mwaka 1980 kutoka kampala akaacha jeshi kisha akaenda home kuwasalimia ndugu na jamaa, akaaga anaenda kutafta maisha Arusha jeshi hataki hakurudi tena hadi leo.
 
Unaonekana wewe unawadharau sana wachungaji. Kwa hiyo unajiona maisha umeyapatia sana siyo ?
 
... take care mzee; your freedom of speech is assured BUT freedom after speech is not guaranteed! Yalikuwa maneno ya Idd Amin Dada kwa waandishi wa habari enzi hizo.
 
Sema baadhi ya wanaume sio wote,halafu ukoo/familia yenu ndio inaonekana inashida,hakuna wasukuma wenye tabia kama hiyo
 
Na mimi nasema kweli siku zote, wanawake wa kisukuma waliokuwa wanasifiwa kwa tabia nzuri hata na makabila mengine wamekwisha
 
Kuna msemo usamao wanawake wote ni wapumbavu lakini akina mama wote ni walevu..nadhani hakuna mtu ambae atakubali mamake aitwe mpumbavu.
 
Mtoto wa dada yangu anamiaka 7 anapoteaga, tunamtafuta mji mzimaa hapatikani, ila mda wa chakula kikiletwa mezani tu na yeye anaibuka kama mzimu
Duuu hili n pepo Mkuu mlikemee tu.. n mawazo yanawajia kwa sababu huenda alikuwa profitable hapo nyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…