Miaka 63 baba mdogo hajawahi kurudi nyumbani

Hii habari yako ni questionable! Mjombake mama aliondoka 1980's mama akiwa mdogo akaja kurudishwa 2000's wewe umshamaliza sekondari. Hebu eleza vizuri.
 
Very sad ....pole sana ndugu yangu ...huenda kuna siku tutamwona tena.
Unyanyasaji na unyanyapaa wa aina hii upo sana kwa kweli .
... aliondoka 1963 baada ya kujifungua; let's assume she was 20. Today she would be 77. Ngumu sana kuonana naye tena Mkuu; tuombe basi japo katika Ufalme wa Mbinguni.
 
Babu yangu hata kabla hajamzaa baba, kaka zake wanne,waliondoka kwenda Zambia (Kitwe kwenye machimbo ya shaba, baadae watatu wakaenda ''KuJhoni''(Joharnesburg) Africa kusini kwenye machimbo ya dhahabu, mpaka leo hawajawahi kuonekana, Ni zaidi ya miaka 70 iliyopita...hii ni kutoka Mbeya Rungwe Tukuyu...........
 
Inauma Sana. Hata sisi shangazi yetu alijifungua mwaka 1963! Naskia akawa anatoka kinyesi. Jamii ikamtenga, akaona isiwe kesi. Ndo hii sasa tunaita "fistula!

Tunajiulizaga sijui alipona au alikufa! Aliondoka na mwanaye😭😭
Nimesikitika sana. Miaka ya zamani kuna watu walipata shida sana na wengine kufa vifo vya mateso makubwa kwa sababu tu ya ujinga, mila na desturi zilizokuwepo kwenye jamii. Hasa wanawake waliathirika sana. Mimi nimezaliwa kwenye jamii ambayo miaka ya nyuma mfumo dume ulikuwa umetamalaki na mwanamke alikuwa anaonekana kama mtumwa wa kufanya kazi. Sitaacha kuwaheshimu kinamama katika maisha yangu nikikumbuka wengi walivyonyanyaswa kwa sababu ambazo ziko nje yauwezo wao.
 
Anko...
Alizamia miaka 18 kwenda kuchimba madini, walikua wawili na Jirani ambaye walikua marafiki sana tangu utoto.
Mwenzake alikaa miaka 12 akarudi kusalimia kwao, akaulizwa mwenzako vipi? Akaseme yupo hataki kuja mpka Afikie malengo yake, japo mpka hapo alikua tayari ameshayapatia maisha vizuri ila kwa malengo yake akaona bado..

Yule Rafiki yake akawa hivyo hivyo anakuja na kuondoka, akimsisitiza mjomba aje, anakataa,
Upepo ukabadilika, mali zikaanza kupukutikaa, Mwenzake yeye alikua na maisha tu ya chini, akaamua kabisa kurudi kwao, Mjomba ndio mambo yakazidi kua magumuu, mama yake(bibi) akawa anaumwa yule rafiki yake akatafuta marafiki wengine kule mgodini ili wamuunganishe na mjomba, ikafanikiwa akamwambia Mama yako Anaumwa sana, furaha yake akuone,

Mjomba akakubali kurudi, alikua hana hata simuu, Ilibidi mawasiliano ya maendeleo ya safari yafaywe baina yetu na konda, watu wakaenda ubungo kumpokea(ilibidi yule rafiki yake naye awepo maana alisema ikitokea mkapotezana na konda hamwezi kumkumbuka) ...

Waliooenda ubungo kumpokea hawakuamini Jamaa alivyochokaa,

Hana simu, nauli alitumiwa, Nguo kaweka kwenya rambo, Yaani kwa ufupi hana hili wala lile,

Safari ya kuja kaskazini ikaanza, huo mpango wa kumrudisha ulifanywa kimya kimya bila mama yake kujua, Maana usije ukabuma sababu ilishatokea hivyo akaumia sanaa, na kati ya wanae huyo alikua akimpenda sanaa, Miaka yote amekua akiota ujio wake na kumsubiria, basi watu wakaona awamu hii wafanye kimya kimya.

Hakuna mtu ambaye alimtambua,
Mama ni mama tuuu, Bibi kusikia tuu sauti ya Hodi Akahamaki kilunga "......... Huyu ni....."
Kuingia ndani, watu hawakuelewa zile nguvu bibi aliziapata wapi za kuamka na kumkumbatia mwanae,
Yeye hakujali amedhoofu wala nini alichofurahi ni kumwona mwanae.....

Aliondoka kwa malengo ya kuja kufunika ukoo kwa utajiri, akarudi akiwa ndio maskini zaidi, akatafutiwa kijimtaji akaanza upya ila kwa shart, lazima abaki kijijini amuangalie mama na mali nyingine mana hakuna mtu, Mama yake alipona wakaishi pamoja kwa furaha miaka mitatu zaidi, Bibi akafariki, yule rafiki yake naye akafariki, ndani ya siku mbili Anko naye akafariki, ilikua mwaka huu, Alinipenda Sana mpaka nikawa najiuliza kwa nini, hata wakati wanawasiliana na yeye kuja alikua ananiulizia, na mimi nilikua simfahamu mana nilikua mdogo na sikua kijijini.. na rafiki yake mkubwa kwenye familia yake alikua mama...

Anko Amefariki na umaskini wake na hata bila mtoto, Japo ameacha kiwanja kikubwa tuu kule.

Kama kuna Ndugu, jirani au rafiki anayejua huu mkasa, Basi tunafahamiana.
 

Mkuu unawezaje kukumbuka hadi tarehe na mwezi.?
Na wewe hiyo ‘wizakale’ ni ‘umekuja zamani’, usharudi ulikotoka.?
 
Ila Mkali umetisha wale watumwa ndio tunaowambia Black lives matter ...hao walilazimishwa bana
Ha ha ha; warudi basi. Afrika ardhi imejaa tele. Kwa Tanzania under special arrangements hekta kadhaa zinaweza kutengwa maeneo ya Bahi na Manyoni kwa ajili ya Black Lives walio tayari kurudi ila ndio hawataki kurudi home.
 

Mkuu unakwama wapi.?

Mama yako yupo hai, na unajua kwao ni Shinyanga... ukimuuliza uende hataki kukuelekeza au unasubiri akupeleke.!
 
Hiyo ndio basi tena
 
Pole ndugu. Wazaliwa wa kwanza sometimes wanakuwa na issues sijui kwanini. Anyway, hata maandiko yanasema ni malango shetani huwachezea kweli kweli. Mvumilie tu kaka mkubwa Bwana atakulipa.
 
Yaani hata Babu akawa anamwambia wewe ushakuwa mkosi...hapo dingi yuko bwiru anasoma..anarudi hom hakumkuta sisy ake ...Kuna makabila mpk leo wanaendekeza hizo mila za ajabu na mamfumo dime....nikibarikiwa kupata mtoto wa kike sitaruhusu aolewe kabila langu... Sitaki kbs
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…