Anko...
Alizamia miaka 18 kwenda kuchimba madini, walikua wawili na Jirani ambaye walikua marafiki sana tangu utoto.
Mwenzake alikaa miaka 12 akarudi kusalimia kwao, akaulizwa mwenzako vipi? Akaseme yupo hataki kuja mpka Afikie malengo yake, japo mpka hapo alikua tayari ameshayapatia maisha vizuri ila kwa malengo yake akaona bado..
Yule Rafiki yake akawa hivyo hivyo anakuja na kuondoka, akimsisitiza mjomba aje, anakataa,
Upepo ukabadilika, mali zikaanza kupukutikaa, Mwenzake yeye alikua na maisha tu ya chini, akaamua kabisa kurudi kwao, Mjomba ndio mambo yakazidi kua magumuu, mama yake(bibi) akawa anaumwa yule rafiki yake akatafuta marafiki wengine kule mgodini ili wamuunganishe na mjomba, ikafanikiwa akamwambia Mama yako Anaumwa sana, furaha yake akuone,
Mjomba akakubali kurudi, alikua hana hata simuu, Ilibidi mawasiliano ya maendeleo ya safari yafaywe baina yetu na konda, watu wakaenda ubungo kumpokea(ilibidi yule rafiki yake naye awepo maana alisema ikitokea mkapotezana na konda hamwezi kumkumbuka) ...
Waliooenda ubungo kumpokea hawakuamini Jamaa alivyochokaa,
Hana simu, nauli alitumiwa, Nguo kaweka kwenya rambo, Yaani kwa ufupi hana hili wala lile,
Safari ya kuja kaskazini ikaanza, huo mpango wa kumrudisha ulifanywa kimya kimya bila mama yake kujua, Maana usije ukabuma sababu ilishatokea hivyo akaumia sanaa, na kati ya wanae huyo alikua akimpenda sanaa, Miaka yote amekua akiota ujio wake na kumsubiria, basi watu wakaona awamu hii wafanye kimya kimya.
Hakuna mtu ambaye alimtambua,
Mama ni mama tuuu, Bibi kusikia tuu sauti ya Hodi Akahamaki kilunga "......... Huyu ni....."
Kuingia ndani, watu hawakuelewa zile nguvu bibi aliziapata wapi za kuamka na kumkumbatia mwanae,
Yeye hakujali amedhoofu wala nini alichofurahi ni kumwona mwanae.....
Aliondoka kwa malengo ya kuja kufunika ukoo kwa utajiri, akarudi akiwa ndio maskini zaidi, akatafutiwa kijimtaji akaanza upya ila kwa shart, lazima abaki kijijini amuangalie mama na mali nyingine mana hakuna mtu, Mama yake alipona wakaishi pamoja kwa furaha miaka mitatu zaidi, Bibi akafariki, yule rafiki yake naye akafariki, ndani ya siku mbili Anko naye akafariki, ilikua mwaka huu, Alinipenda Sana mpaka nikawa najiuliza kwa nini, hata wakati wanawasiliana na yeye kuja alikua ananiulizia, na mimi nilikua simfahamu mana nilikua mdogo na sikua kijijini.. na rafiki yake mkubwa kwenye familia yake alikua mama...
Anko Amefariki na umaskini wake na hata bila mtoto, Japo ameacha kiwanja kikubwa tuu kule.
Kama kuna Ndugu, jirani au rafiki anayejua huu mkasa, Basi tunafahamiana.