Miaka 97 ya Mzee Mwinyi na amani ya moyoni pasipo nongwa na visasi

Mzee ana ukwasi wa kutosha
1960 alikuwa Mkuu wa Chuo cha Ualimu Znz cha Lumumba tangu hapo akaanza kuwa na mshahara mkubwa

1966 Balozi, kaja kuwa Waziri wa Jamhuri tangu 1972

kaja kuwa Rais wa Znz

kaja kuwa Rais wa Muungano

binti yake mmoja kaolewa na mtoto wa Mfalme wa Abudhabi

Mtoto wake Rais wa Znz

mtoto wake mwingine Mbunge wa Bunge la Jamhuri

Ma binti zake ni Wafanyabiashara wakubwa wanaoshiriki kwny kandarasi kubwa kubwa za nje na ndani ya nchi

Vijana wake wa kiume ni ma Tycoon kwny biashara ta Utalii Afrika mashariki

wengine ni Wafanyakazi wa Taasisi kubwa kubwa za kimataifa

sasa hapo akiwa na Ukwasi ni jambo la kushangaa kweli ?

mwenzangu na mie kamshara ka TGSD hata shangazi akidondoka kwny bodaboda kijijini lazima utafutwe utume elf 5 ya kumbeba kwny bodaboda utachomokaje kwny lindi la umskini?
 
Sahihi kabisa

umri na Afya havina uhusiano na dini wala uchamungu

 
😄😄😄😄😄😁
 
HV mzee huyu kashakabidhiwa ile nyumba ambayo jiwe amemjengea pale kawe huku akiwa Bado Ana nyumba pale mikocheni
 
na mtoto wake mwingine ni rais wa JMT ila sijaandika mie
 
Mzee Mwinyi angekuwa na fikra na mawazo kama yako nahisi asingekuwa na afya yenye nguvu alionayo sasa, hapa sizungumzii kuwa na umri mkubwa.

Nachoamimi mimi kufa mapema ni mipango yaungu mwnyewe. Roho mbaya husababisha kudhohofu kwa afya ya mwili pia.
 
Wewe mjinga tu wazee wa kislam wanaokufa mapema wote ni waovu? Vipi wakristo wazee wapo wengi tu! Udini ndo shida yenu wavaa madera! Vipi akina warioba huwaoni?Pia akina Butiku, Samwel Marechera!
Ni Malecela sio Marechera. Ukifika wakati wao watazungumziwa kwa uzoefu wao tofauti na huu wa Mwinyi.
 
Mzee Mwinyi ameishi miaka mingi kwa vile sera yake ya RUKSA ilimuondolea nafasi ya kufikiri.
Kila mtu alifanya lake.
Economic Hitmen wakamwambia uza na kuua TIPER ili biashara iwe huru, yeye akasema RUKSA!
Matokeo tunayaona miaka mingi baada ya utawala wake na kabla hajafa.
 
Matunzo Mazuri katika Uraisi wake
Matibabu mazuri
Chakula Kizuri
Hewa Nzuri
Nyumba Nzuri
Mtoto wake Ni Raisi
Hana Shida na Pesa

Hata Papa,Mapadri..Askofu..Masista wakubwa wakubwa Wanaishi maisha Marefu.
 
Mada ni Mzee Mwinyi na ukosefu wake wa nongwa zenye kuongeza maadui na hasira,Hayo ya watoto na wakwe zake yanamhusu binafsi.
 
Kama hiyo unahisi ndio sababu ya mzee Mwinyi kuwa hivyo, wewe ujui kuna watoto wa Mwl na Dr Magufuli walikufa mapema tu ilhali walikulia kwenye maisha ya starehe na raha kuliko wewe.
 
Hapo wewe ni kula , kuswali na kuuliza…….saa ngapi vile?
 

Alimuuzia mwarabu eneo la Loliondo pia, sehemu ambayo ni mapito ya wanyama wanapohama. Waarabu wamehamisha wanyama hai kwenda uarabuni na kutengeneza mbuga ya wanyama.
 
Ukiishi ukiwa unafikiria kuumiza wengine mchana kweupe maana yake na wewe uliumizwa sana utotoni. Kule kuumizwa hakuishi kuwa ni tukio la kivitendo tu, bali kunaingia ndani kabisa ya ubongo wako.
Kwa hiyo unaamaanisha JPM ndio alikuwa ana "nongwa na visasi"! Sawa. Endeleeni kumkana enyi wafuasi uchwara.
 
Hizo ni akili zinazofikiriwa na watu wavivu, mfumo wa Nyerere alisababisha wengi kuwa mafukara wa hali ya juu sana, watu wazama wanajua kuwa kipindi cha Nyerere watu walivaa makaniki tu na viatu vya magogo ya miti na magome yake, watu walikuwa wanaishi kwenye nyumba ambazo hazikuwa bora, ilikuwa mtu ukijenga nyumba ya bati tu mwaka mzima unakuwa mahabusu kuhojiwa hata kama ulidunduliza kulima ufuta na mbaazi ndipo ukapata hiyo pesa.

Magufuli nae alikuwa mchoyo sana kuliko mlivyokuwa mnafikiria, mapato yote ya serikali asilimia kubwa alipanga yaende kanda ya ziwa. Kwa manufaa ya watu wa kanda hile. Alijawa na nepotism na ukabilarism, na kwa akili ya kawaida tu inaonekana mfumo wa urais angeubadilisha ili aweze kukaa muda mrefu madarakani.
 
Wewe mjinga tu wazee wa kislam wanaokufa mapema wote ni waovu? Vipi wakristo wazee wapo wengi tu! Udini ndo shida yenu wavaa madera! Vipi akina warioba huwaoni?Pia akina Butiku, Samwel Marechera!
Unapaniki Bure tu, uwaoni waislamu walio-criticize hilo bandiko, hio ilikuwa fikra zake katika ufahamu wake.
 
Matunzo Mazuri katika Uraisi wake
Matibabu mazuri
Chakula Kizuri
Hewa Nzuri
Nyumba Nzuri
Mtoto wake Ni Raisi
Hana Shida na Pesa

Hata Papa,Mapadri..Askofu..Masista wakubwa wakubwa Wanaishi maisha Marefu.
Na wao wana watoto marais??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…