Miaka 97 ya Mzee Mwinyi na amani ya moyoni pasipo nongwa na visasi

Some people are really blessed
 
Umeandika vizuri sana lakini mwishoni kabisa usingemalizia vile ingewaachia watu watafakari wenyewe.
Hata hivyo staili ya mwinyi kimaisha ni nzuri sana watu wema wanaweza kuiga hiyo staili
 
Ukiishi ukiwa unafikiria kuumiza wengine mchana kweupe maana yake na wewe uliumizwa sana utotoni. Kule kuumizwa hakuishi kuwa ni tukio la kivitendo tu, bali kunaingia ndani kabisa ya ubongo wako.
Sidhani malezi ya utotobi yatakuwa ndio factor kuu. Kuna hulka na maumbile pia

Mfano akina Mandela mbona wamekulia kwenye msoto lakini wakasamehe

Kuna watoto wa marais na wanasiasa wakubwa huko nchi za DRC Burkina Faso n k sijui walikuwa nao marais na wakawa makatili tu
 
Ni kweli 100% kuhusu family history, shida na suluba za utotoni na hata za makuzi zinavyoathiri mwelekeo wa fikra za mtu na jinsi atakavyotenda ukubwani akitapata madaraka. Mifano ipo mingi, lakini mfano wa wazi kabisa na unaodhihirisha vyema hali hii ni wa Adolf Hitler. Soma historia yake kodogo tu utayaona yote hayo.
 
Mandela hakukulia kwenye msoto. Mandela alikuwa wa ukoo wa kichifu, na hadi anaingia gerezani 1963 alikuwa tayari na degree ya chuo kikuu, fursa adimu sana kwa watoto weusi miaka hiyo. Mandela alifungwa akiwa na umri wa miaka 45, kwahiyo kama ni msoto hasa ulianza akiwa na umri huo, kabla ya hapo alikuwa kiongozi mwenye kuungwa mkono na umma na hata mataifa mengine, alipambana lakini hakusota, alianzia msoto gerezani at 45.
Historia inaonesha kuwa watu wenye disturbed childhood wanaishia kuwa watu wa visasi vya kudumu dhidi ya watu ambao hata hawahusiki na kilichowasotesha. Soma habari za Adolf Hitler, ni mfano halisi.
 
Mandela aliesamehe ni wa mchongo Mandela HALISI asingekubali utumwa wa kiuchumi walionao wa sauz Hadi leo
 
Hukutoa ufafanuzi wa swali uliloulizwa. Uchaguzi na ubinafsishaji wapi na wapi?
Mimi nilitaka ufafanuzi wa para hii
"Mrema alipambana akamshinda kwenye uchaguzi. Nyerere alimuunga mkono Mrema kugombea, kui -challenge CCM."
Fafanua unataka nifafanue nini?

Mrema alikuwa jembe hashwa. Majambazi yote yalikaa nyumbani. Panya Road angewaua wote. Wasingethubutu kujitokeza. Alikuwa kama JPM. Zaidi ya JPM. Chuma.

Watz wengi wanataka amani, usalama, ajira, ,mazingira mazuri ya kufanya biashara. Sio taarabu, ngojera, maneno mengi.

Majaliwa anaweza kutufaa ni mchapakazi, anatatua matatizo ya sisi walalahoi.

Watz wanataka kiongozi imara sio legelege, kurembue macho.
 
Huyo Ahmed Hassan Diria, balozi na waziri, usituchefue wengine tuna ndugu waliumia sababu yake. Nyumba ya Upanga jirani na hekalu la wahindu, niseme zaidi? Dogo amesota sana jela kwa kubebeshwa ngada na huyo mzee. Na alimtaja lakini hola.
 
Asante. Wakumbushe pia kuwa yule afande wa Mutukula Gen David Musuguri ametimiza miaka 102 mwezi January. Na katika mahojiano yake siku alipotimiza miaka 100 alisema ameishi na ugonjwa wa kisukari tangu alipotimiza miaka 60, yaani amedumu na kisukari for 40 years!
 
Aliachiwa nchi maskini sana na Nyerere. Tulikuwa tumetoka vitani mwaka 1978 madhara yake yakiwa dhahiri kwa kila sekta.

Ndio miaka ya mwanzoni ile, tofauti na hawa kina Samia na hayati JPM waliokuta kuna wasomi wa kila aina.
Ukiwa Nchi maskini haimaanishi uuze kila kitu. Kuna vitu vya msingi vinavyoisaidia jamii, Taifa. Vibaki mikononi ya serikali (Wananchi).
 
Umenikumbusha kifo cha mwandishi wa habari wa gazeti la Mfanyakazi enzi hizo anaitwa Francis Katabalo, alikua anaandika sana habari za Uchunguzi, gazeti la Mfanyakazi those years lilikua gazeti la habari za Kiuchunguzi. RIP Francis Katabalo
Rekebisha jina. Aliitwa Stanslaus Katabaro, kwa kifupi Stan Katabaro.
Tuliokuwepo tulimjua personally.
 
Hivi ukimwondoa mzee wa Msoga, Getrude Mongela, Anna Makinda na Msuya Kuna waziri wa mzee Mwinyi ambaye bado Yuko hai?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…