Miaka mitano baada ya kumaliza chuo, hatimaye naenda kwenye mshahara wa Milioni 6, bado siamini, nawaza sana

KALINZI NYUMBANI

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2015
Posts
1,797
Reaction score
1,594
Wameniconferm jana, niende kituo cha kazi huko Geita ,mwezi ujao, hapa nilipo nahisi kama naota vile.

Naona siku kama haziendi niende nikalipoti, nahisi kama jamaa wanaweza ahirisha vile, nawaza namna gani maisha yangu yanaenda kubadilika, nawaza namna gani naenda kuitoa familia yangu kwenye umasikini baada yakufanya biashara ndogondogo nikiwa chuo, nahatimae baadae zikaja kuanguka. Nawaza miradi gani Nije nifanye hapo baadae, nawaza usafiri gani ntakuja kununua.

Nawaza zile haso zakwenda Dodoma Kila mara kwenye interview ndio zimeisha au, nawaza safari zakwenda nje ya nchi kwenye training mbalimbali kama walivyoniahidi.

Nawaza Dem wangu niliekua nampenda nakujitoa Kwa Kila kitu kwake ambae tulikua tunakaribiana mshahara yeye akiwa anapokea mil 1. Mie nikiwa napokea mil 1.2 alivyonipiga chini nakwenda kuolewa najamaa mwenye mwenye maisha mazuri kuliko Mimi, atanionaje nakile kigari Cha Jamaa yake kilichochoka choka.

Nawaza sana aisee hivi ndio naondoka kwenye kundi la MAKAPUKU au vipi?

Aisee wakuu tuendelee kumuomba Mungu Sana, maana hii kazi niloomba tu huko LINKEDIN bila kujuana na mtu yeyote.

Bado nawaza Sana na nahisi kama ndoto.

Wapiganaji wenzangu tusichoke tuendelee kupambana.
 
Kwanza hongera ila cha kukushauri tu, usianze kununua nepi kabla mtoto hajazaliwa maana anaweza kufa pia.

Kufanikiwa kwako kuna wengine inawauma na jicho la husda lipo. Pambana kimya kimya na umshukuru Mungu sana wala usiwabeze makanjibai kwani nao walikulipa mshahara kwa makubaliano.

Hujapasua bado kwani binadamu hatupangi maisha ila yanakuja yenyewe la mwisho ni Confirm msomi.
 
Nakubali mkuu.
 
Sababu kubwa ya wazee kuendelea kulamba teuzi huku wamestaafu ni vijana kushindwa kuwa na vifua vya kuhifadhi mambo.. pia vijana kushangilia ushindi wakati mechi bado haijaisha. Hebu kijana tuliza hizo hisia zako... subiri hadi uanze kazi kwanza. Halafu kingine huo mshahara kama utapata utumie vizuri kwa ajili yako na familia yako. Mambo ya kuwaza kumuoshea Ex ni upumbavu mtupu. NINASISITIZA TENA uwe mkimya na msiri. Kitendo cha kutuanikia mishahara yako kinaashiria wewe ni kijana wa hovyo.
 
Punguza makasiriko atakua excited, jambo kubwa hajataja kampuni, kwahio muacheni afurahie.
 
Mkuu Hongera Sana, Kwa kumbukumbu zangu huko Kwa makanjibai mie ndio nilikuambia utume CV humu humu jamiiforum, tukumbukane mkuu. Namba yako bado ninayo.
 
Hongera Sana mwanetu..kawakilishe vizur usije ukapagawa na ml 6..ukaanza mambo ya Ajabu
 
Hongera, Ila kawe mtu mwema pesa hisikubadilishe tabia njema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…