Miaka miwili ya Rais Samia, Hakuna jambo la maana linaloonekana!

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
2,754
Reaction score
4,975
Ni miaka miwili sasa imetimia tangu kiongozi wa awamu ya sita kuingia madarakani, Lakini utafiti unaonyesha na hata unapojaribu kuuliza, Je, kuna jambo lolote la msingi na la maana unaloweza kupoint out kwamba jambo hili limegusa maisha ya watanzania wa hali zote? Je, kuna nia ya dhati na mikakati madhubuti ya kutokomeza maadui wa taifa (umasikini, ujinga na maradhi)? Je, Walau kuna miundombinu ya maana katika level za kimataifa na project kubwa zotakazotiinua kiuchumi zime/zinafanyika? Je, Kuna nia ya dhati ya kudhibiti matumizi na kuziba mianya ya rushwa na kuelekeza nguvu katika matumizi ya maendeleo?

Asilimia kubwa ya watanzania watakupatia jibu moja tu, HAPANA.

Kwa tathmini hii ni wazi kwamba huenda Tanzania tusiifikie safari yetu ya kujikomboa kiuchumi na kuondokana na maradhi na ujinga, Au itatuchukua muda mrefu sana kuweza kuondokana na umasikini.
 
Hakuna wanaotekwa..
Hakuna wanaopigwa risasi .
Hakuna anekamatwa Kwa kupinga serikali watsap gruop..
Hakuna Kesi ya wamiliki wa JF..
Hakuna mfanyabiashara alieporwa hela..
Hakuna plea bargain...
Hakuna kabila moja kupewa teuzi..
Hakuna upumbavu mwingi...

Miaka miwili ya mafanikio
 
mama anapendwa na wafanyakazi maana dili sasa hivi ni kama kawa

ila wanyonge wanamwona aliye feri
 
Ni kweli ila sio kweli saaana
 
Mama amefanya mengi sana amejenga madarasa mengi sana haijawahi kutokea tangu tupate uhuru ,amepandisha madaraja watumishi ,ameleta mariziano ,miradi yote ya kimkakati anaiendeleza, kilimo kimeimarika sana ,ametoa ajira nyingi
Madarasa ya UVIKO?? .
 

Ni rahisi sana kusema rais Samia hajafanya kitu sababu hujui

Sasa hebu tuambie kwanza wewe hii miaka miwili umefanya nini🤣🤣
 
samia she's misfit to the position!
 
Yaani ngosha huoni reli ya SGR inayojengwa Mwanza kuja Tabora na Tabora kuja Singida, Singida kuja Dodoma na Dodoma kuja Morogoro?
Alafu Tabora kwenda Kigoma?

Akimalizia ile aliyejenga Mwendazake Dar kwenda Morogoro na Morogoro kwenda Dodoma?
 
Mama amefanya mengi sana amejenga madarasa mengi sana haijawahi kutokea tangu tupate uhuru ,amepandisha madaraja watumishi ,ameleta mariziano ,miradi yote ya kimkakati anaiendeleza, kilimo kimeimarika sana ,ametoa ajira nyingi
Ripoti ya CAG inasema kwenye ujenzi wa Yale madarasa Kuna pesa nyingi imetafunwa,madarasa mengine hatajajengwa (hewa) na Kuna yaliyojengwa chini ya kiwango(yamechakachuliwa).

Pia ile hela ya covid iliyojenga hayo madarasa Kuna ambayo yaliagizwa magari. Hadi Leo pesa yenye thamani ya tsh bilioni 18 haijulikani ilipo maana magari yenye thamani hiyo pesa hayajaonekana popote hapa nchini. Magari yaliagizwa kutoka Japan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…