Miaka Tisa (9) ndani ya JF: Kumbukizi nilivyojiunga na kuishi JF nikiwa kama Mwanafunzi wa Sekondari

Mungu wangu! Hii ni maajabu. Adriz unakubali kuwa mtoto wa 2000!!? Mi nilijuaga ni jibaba fulani hivi lenye madevu kila pembe, jitu lenye heshima yake na familia kwa ujumla

Unaweza kuta members wote wa humu JF tu watoto wa 2000 isipokuwa mimi, wewe unaesoma hii comment and staff ya JF
 
Hongera sana adriz Kwa kutimiza Miaka 9..

Mimi leo nilikuwa Nitimize miaka 14 Jf kwa Id yangu ya Zamani Ila walinilima BAN ya Maisha 😅😅😅 mwaka 2012 sitasahau 🤣🤣🤣

Mpaka leo nimekuwa Mtu mwema Nafurahia Miaka 12 Bila Kulimwa BAN 🤣🤣🤣

Jilinde na BAN mkuu Hiyo inaumiza Sana
 
H
Hee kosa gani hilo la ban ya maisha??
 
Hamna mkuu usiogope , kipindi najiunga kuanzia mtaani mpaka shuleni sijapata mtu wala rafiki anayeijua Jf labda wajiunge kipindi Cha sasa maana utandawazi umekua na madogo wengi wanachimba mitandaoni.

Watu wengi wanastaajabu hilo haswa wale ambao tumezoeana na kupeana namba za simu tukawa na tukawa Marafiki nje ya Jf hawakuweza kuamini kunikuta Mimi dogo tu.
 
H

Hee kosa gani hilo la ban ya maisha??
Zamani sheria Zilikuwa Ngumu sana Tofauti na Siku hizi kulikuwa na Zimwi moja la kuitwa Invicible huyu jamaa Ukiingia kwenye 18 Unakula BAN yaani kulikuwa hakuna Cha Msalia Mtume, Sheria ilikuwa sheria kweli..
Na JF ilikuwa Jf Kweli..

Nakumbuka kama sijasahau sana Tulikuwa Tunabishana Kuhusu Premium Member, Tanzanite member,Platinum member,Gold member Na title zingine Kuhusu Kuruhusiwa na Ziwepo kulingana na Malipo ya Watu wanavyochangia Pesa..

Yaani Member atajulikana Kwa title yake kulingana na Pesa Atakazochangia Mimi ilikuwa ni mmoja wa wanaopinga hizo sheria kwamba Title kulingana na Pesa utakayotoa..

Nakumbuka Kuna mwamba Alijipendekeza akanikejeli unajua Kipindi hicho Damu ilikuwa inachemka Kijana Shababi nikamporomoshea Matusi hadi leo sijui mwenyewe Niliyatoa wapi 🤣🤣🤣..
 
Acha tuu kaka hata mm nilikua naporomoshaga matusi ila kwakweli nimegundua hayana maana kabisaa..unaweza mtukana baba yako humu...ukapata laana invisible..😃😃😃😃
 

adriz

JF-Expert Member · From Buza Dar es Salaam
Joined Sep 2, 2017 😂😂😂 hiyo miaka 9 inakujaje mkuu?
 
2015 uko form one 😅😅😅😅😅😅😅

unisalimie
 
2015 form 1
Madogo ina bid muanze kutoa shikamoo kwa mabraza zenu sasa
CC
The Mongolian Savage
 
Mambo yamebadilika kweli lakin bado jf kwa Tanzania hii ndio mtandao wa wenye akili, na ukitulia unaokotea okotea madini sio kama facebook, Ig, tiktok


All in all hongera Mr adriz mtaani vijana wenye maarifa ni wa kuokoteza kwelikweli lkn kupitia jf we met with u and others and we sharing views
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…