Adam hakuwa binadamu wa kwanza kuishi duniani,hizi habari sijuwi mnazitoa wapi na mnazisambaza kwa malengo gani.
Hakuna ushahidi wa kihistoria ya kuwa Adam alikuwa binadamu wa kwanza kuishi.
Wakati huyo Adam anaishi miaka 3000-4000bc iliyopita huku Africa Jamii ya Homo ilishaishi miaka million 2-3 iliyopita na walishasambaa hadi maeneo ya mbali sana.
Ukiyachunguza vyema maandiko matakatifu, hasa simulizi kutoka Kitabu cha Mwanzo kama vile kilivyoandikwa na Nabii Musa, hakuna maelezo yoyote yale kuhusu historia ya kuumbwa kwa sayari ya dunia. Bali kimeanza na simulizi kuhusu kazi ya Mungu ya kutengeneza mazingira ambayo yatakuwa ni makazi ya kudumu kwa viumbe ambavyo alipenda kuviumba kwa utashi wake Yeye mwenyewe.
Nukuu ya maandiko hayo hutupa mazingira ya aina tatu ambayo Mungu aliyafanya. Kwa kuwa dunia ilikuwepo kabla ya uumbaji wa mwanadamu, nayo dunia ilikuwa imezingirwa na sura ya maji, basi Mungu aliyatenga maji hayo ili ikapate kuwepo kwa eneo nchi kavu. Eneo la nchi kavu na maji na eneo la juu akaliita mbingu ambapo aliweka jua na mwezi kwa ajili ya kuwepo kwa usiku na mchana pamoja na majira tofauti ya mwaka.
Kwa hiyo basi maandiko matakatifu hayazungumzii kabisa kuhusu mwanzo halisi wa sayari yetu, "solar system" ama "galaxy" bali huzungumzia kuhusu mwanzo wa viumbe hai vilivyopo juu yake.
Labda ni vyema tupitie kwa pamoja nukuu ya maandiko ili tupate zaidi ufahamu na mantiki ya msimulizi kama ifuatavyo;
Kitabu cha Mwanzo
1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.
5 Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.
6 Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji.
7 Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.
8 Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.
9 Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.
10 Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Kwa hiyo basi, hakuna ubishi wowote ule kuhusu uwepo wa uhai kabla ya Adam, kwa kuwa malaika wa nuru, shetani na malaika wengine walikuwapo kabla yake, lakini wao walikuwa na miili yenye maumbile ya kiroho, ndiyo maana makazi yao yalikuwa juu ya nchi ama mbinguni. Tofauti yao na Adam, yeye aliumbwa pia kwa roho bali mwili wake uliumbwa kupitia udongo ili aweze kuishi katika nchi kavu.
Kwa kuwa Mungu ni wa milele, basi hata hizo simulizi za mamilioni ya miaka ya uwepo wa dunia huenda zikawa ni za kweli. Lakini zinapatika kutoka katika chanzo kipi cha kuaminika cha habari?
Ni kweli kabisa pengine shetani na malaika wengine waovu waliishi katika sayari ya Mars. Lakini pale walipoasi walitupwa katika sayari yetu ya dunia, na kuwekwa chini ya nchi iliyokuwa imezungukwa na vilindi vya maji.
Na ukweli huu unapatika kuhusu simulizi za uwepo wa kuzimu. Maandiko matakatifu hituambia kuzimu ni chini ya nchi ambapo ni makazi ya muda ya malaika waovu kabla ya hukumu yao ya kutupwa Jehanamu.
Sent from my Nokia 2.3 using
JamiiForums mobile app