Miaka, toka kuumbwa kwa adamu hadi kufa kwa Abrahamu. Umeona nini?

Nimekupata vema mkuu Tena sana tu umeeleweka na nimeongeza kitu pia,Hilo kuhusu gharika wayahudi walikopi kwenye maandiko ya Mesopotamia hasa kutoka katika Epic of Girgamesh
Hayo masimulizi yana utata kidogo maana wengine tuaamini hiyo gaharika ilitokea katika ukanda wa mto Euprates ambapo ndio hizo miji za Accient civilization zilikuwepo so kutokana na kutojua Kwa wayahudi kwamba Dunia kubwa wao wakadhani lile bonde la mto lilipojaa maji na kumeza miji wakajua Dunia nzima ndio imekua flood's!
Halafu nakuunga mkono hiyo vita ya nuclear weapons kupigwa Duniani miaka maelfu nyingi huko nyuma maana hata chanzo cha majangwa tunayoyajua ni hizo vita na ndio maana middle east yote imekua kame sababu ya pale ilikua base ya viumbe wengi na miji mikubwa enzi hizo Hivyo missiles nyingi zilielekezwa pale na kusababisha jangwa,na pia huko Gabon Kuna sehemu iligunduliwa mabaki ya Nuclear reactors ambayo Ina mamillion ya miaka so inawezekana hapa hii Dunia imekaliwa na viumbe wengi kabla yetu na sisi pia ni Alliens wa wa zamu kuikalia ila sio mwisho wa Alliens wengine kuja tokea watakuja na wengine pia labda supanorva itake place!
 

kinachofanya niamini kuwa garikani ni tukio la kweli na lilitukia na kufunika Dunia mzima ni kitendo cha Baadhi ya mabaki ya viumbe Bahari kupatikana jangwani.
nje na maandiko ya Bible hii ni moja fact muhimu kwangu ya kuamini kuwa garika sio ngano bali ni kitu halisi.
jambo la muhimu tunaeendelee kunifunza.
ila kwangu mimi hakuna maktaba nzuri kama biblia.
 
Dunia ina siri nyingi ndugu zangu ukiwa huru kifikra na akili utajifunza mengi ya kustaajabisha.
 
Pia ushahidi unaonyesha kuwa jangwa la sahara zamani lilikuwa na maziwa, nyasi na wanyama kibao. Bila shaka ni baada ya gharika japo wanasayansi wanaexplanations zao.
 
lazima iwaongelee maana masimulizi mengi Kwenye bible verses wamecopy Kwenye Accient writings za Mesopotamian!
ACHA UZUSHI BIBLIA INAJITETEA, NA MIAKA NA MIAKA INAZIDI KUDHIHIRIKA BIBLIA NI NENO LA MUNGU ,

NAKUPA MFANO

katika mwaka wa 1868 kule Diboni, Yordani Kulipatikana jiwe lifaamikalo kama MOABITE STONE lililogunduliwa na mwana akiolojia na mmishionari wa ujerumani Klein,

Jiwe hili linathibitisha vita ya wa moabu dhidi ya Israeli kama ilivyoandikwa katika 2Fal 2 na 3.

Kati ya shuhuda za kiakiolojia za kabila hili la wa moabu ni Jiwe la Mesha, linaloeleza ushindi wao dhidi ya mwana wa mfalme Omri wa Israeli.

JIWE HILI LILIKUTWA LIMEANDIKWA MANENO HAYA

“Mimi ni Mesha […] mfalme wa moabub […] Omri alikuwa mfalme wa Israeli, na akawatesa moabu Moabu […]Nilichukua kutoka humo vyombo vya Yehova […] ilihali nyumba ya Daudi ilimiliki Horonaimu


Jiwe la moabu ni maelezo ya matukio yanayofanana na 2 Wafalme sura ya 3. Watu kadhaa wa bibilia na mahali hutajwa



Jiwe la MOABU Lilikuwa na umri unaokaribia miaka 3,000. Ni kipande cha jiwe la basalti jeusi lililosuguliwa likiwa na upande wa juu ulioviringishwa vizuri, lilikuwa na kimo cha karibu meta 1.2 likipita kidogo tu upana wa meta 0.6, na likiwa na unene unaokaribia meta 0.6.
 
lazima iwaongelee maana masimulizi mengi Kwenye bible verses wamecopy Kwenye Accient writings za Mesopotamian!
SIKWELI BIBLIA ITAENDELEA KUJITETEA SIKU ZOTE , HATA MUICHAFUE VIPI, SIR ISACK NEWTON ALIICHUNGUZA NA KUTHIBITISHA NI NENO LA KWELI LA MUNGU AKIKISOMA NA KUKICHAMBUA KITABU CHA DANIELI KULIKO HATA CALCULUS
 
UMEDANGANYWA NA UNAENDELEA KUDANGANYA WATU...... BIBLIA NI NENO LA KWELI NA LINAENDELEA KUDHIHIRIKA KILA SIKU

Mji wa ninawi uliukuwa ngome na mji mkuu wa waashuru na uliotukuka kati ya 933-612 B.C, uliangamizwa na majeshi ya wakaldayo na waajemi mnamo mwaka wa 612 B.C .

Kati ya miaka 1800 mabingwa wa elimu ya mambo na nyaraka za kale (ARCHEOLOGIST)walifanikiwa kuchimbua sehemu ulipojengwa mji huu na kugundua maktaba kuu ya mfalme Assurbanipal(669-626B.C) iliyokuwa na nyaraka nyingi za kale. Ingawa habari hizi za NINAWI zimetajwa katika biblia AGANO LA KALE,

waandishi wa historia wa kiyunani na kirumi hawakujua lolote kuhusu mji huu wa WAASHURU na historia yake. Jemedari na mwanahistoria ,na mwandishi wa kiyunani Zehnohifani(Xenophon,434-355 B.C) alipofika mahali hapo akiwa na kikosi cha mamluki wa kiyunani 10,000 mnamo mwaka 401 B.C hakuna mtu aliyeweza kumwambia jina la mji huo .

Mambo ya namna hiyo ndiyo yaliyomfanya Voltaire(1694-1778 B.C) na watu wengine walidhihaki BIBLIA na kuiona kama kitabu cha hadithi za kubuni.

Lakini miaka ya 1800 mabingwa wa elimu ya mambo ya kale walichimbua na kufanikiwa kugundua kiwanja ulipokuwa umejengwa mji wa ninawi pamoja maktaba kuu ya mfalme Assurbanipal, mlimokuwa nyaraka na hati mbalimbali zilizoithibitisha biblia kuwa ya kweli katika ulimwengu wenye mashaka.

Mfaransa Paul Emile Botta na mwingereza Austin Henry Layard wanastahili sifa kwa kazi ya kuchimbua na kugundua magofu ya ninawi yaliyokuwa yamefunikwa na udongo wa karne nyingi na kuwa chungu kubwa na hivyo kuthibitisha kuwako kwa mji wa kale wa ninawi.Penye chungu la mji wa kale khorsabad, Botta aligundua jumba la mfalme SARGONI,aliyetawala ASHURU mnamo mwaka 722-705B.C.

Wapinzani wa BIBLIA walikuwa wamedai hakuna mtu aliyejulikana kwa jina la SARGONI, acha ya kuwa mfalme wa ASHURU, hii kwasababu jina lake halikujulikana na waandishi wa historia ya kale ya Waashuru ila tu lilikuwa limetajwa mara moja tu katika BIBLIA ( Isaya 20:1).

Austin Henry Layard aliyefanya uchunguzi wa kuchimba katika MESOPOTAMIA kutoka 1845 hadi 1854 aligundua vyungu vya mji huo ambavyo vilikuwa vimegawanyika na kuwa vilima viwili vya magofu .Chini ya kilima kimoja ,Nabi Yunus ,

Layard alivumbua jumba la mfalme Esar-hadoni ALIYETAWALA MWAKA 681-669 B.C .( Soma 2 wafalme 19:37)na chini ya kilima cha pili Koyyunjik, aligundua jumba la kifalme la Senakeribu mfalme wa Ashuru (705-681 B.C) Soma 2 wafalme 18:13…

 
hahahahaha Aisee wewe jamaa unanifurahisha sana hivi unadhani Mimi siyajui haya?
Nayajua kiundani sana na hunidanganyi kitu kuhusu Accient Mesopotamia na miji yake,mwanzo wa mwingiliano wa jamii za Annunaki,ustaarabu wote wa Assyrian, Sumerian, Babylon, Egyptian, Kush, Aztec, Maya, Peru, Indus valley nk
Sasa unakuja kunambia Eti Kuna kina nani walikua hawajui kua Kuna miji na wafalme kadhaa huko nyuma na biblia imesema inawatambua na wanasayansi wamegundua juzi hapa kua ni kweli hiyo hainifanyi nione biblia ni ya kushangaza wakati baadhi ya maandiko imeyakopi kutoka katika maandiko ya kale ya MESOPOTAMIAN
Sasa nikuulize kitu mkuu ulitaka hayo mambo yasiandikwe Kwenye Abrahamic religion verses wakati mwanzolishi wa hizo Dini Mzee Abram alitoka Kwenye jamii za Waashuru wa kale?
Huoni hapo ilikua rahisi kujua historia za mababu zake na kuyanakili Kwenye hiyo old bible?

Kitu kingine unajua dhana ya mungu El
Abraham aliipata wapi?
Unaijua historia ya Merchizedec mtawala wa Salem ambaye ndie kiumbe aliempa huyo baba wa Imani wa wayahudi ujuzi na maarifa ya kumjua mungu
El Murduc?
Bado bado sana ndugu yangu nenda kasome kiundani kuhusu miungu ANNUNAKI
Walitie kina Anu,Murduc,Enki nk halafu njoo hapa tuchambue haya maswala kiundani ndio utapata mwanga Acha kukalili Bible kuona Kama ndio source ya yote kumbe nayo ni copy and paste ya Accient writings of Accient civilization!

You are welcome!
 
Si rahisi kwa asili ya Taifa hili la Wayahudi kupenda na kuiga mila na desturi dhaifu za wasio wayahudi (Goyim).
Ilikuwa ni mwiko kwa Wayahudi kujifunza Mila na hadithi za wageni iwe wawe ugenini ( Walipochukuliwa mateka) au katika nchi yao(Yuda). Na ilikuwa ikitokea hivyo basi Mungu aliwapiga kwa adhabu kali sana!

Hivyo Tunapoongelea Habari za Biblia tunaongelea habari za Taifa lisilochanganyikana na mataifa mengine! Wala lisilo na shirika katika mila na desturi za wengine! (Hakika walipojisahau katika hili walipigwa sana).

Muundo wa Kuandika Historia yao na Tarehe zao na Miezi yao na Miaka yao ni tofauti na Mataifa yote ya Mashariki ya Kati! Hivyo kwa urahisi tu - Haijawahi kuwa vyepesi kwao kuiga na Kufuata hadithi za Watu wengine( kama jinsi ulivyoorodesha hapo katika mada yako).

Labda niseme hivi! Wayahudi kwa Asili wanadharau za Kihaya! They are too proud not to imitate any fairy Tale, it doesn't matter how funny and unique that story is.( To the Haya if you were not educated at Makerere! you are nothing at that time).

Hata Katika Agano Jipya sasa! Unaona shida inayojitokeza! Ni wakati ambapo Ustaarabu wa Kigiriki/Kiyunani unafifia na Kuupa Nafasi Ustaarabu wa Kirumi. Unaona wazi kuna mabishano ya Wayahudi na Wasio wayahudi wanaotahiriwa(Wayahudi) na wasio tahiriwa?wenye Govi (Wagiriki na Warumi). Inafikia hata kutaka kushindwa kula pamoja! Je inawezekana watu hawa wanao tahiriwa kunakiri na Kuandika historia yawasio tahiriwa?

Biblia inaeleza historia na habari ya Taifa la Wayahudi juu ya Matendo Makuu ya Mungu wao YEHOVA dhidi ya Mataifa yote ya ulimwengu wa wakati ule na sasa!
 
Bibilia haijacopy popote.
ila mambo ambayo bibilia imeyaandika bila kujali yaliandikwa lini yalikuwepo au yalijulikana hata kipindi ambacho hao jamaa wanacompile historia yao. hapo ndipo watu wanashindwa kuunganisha dots.

Kuzaliwa kwa yesu, gharika,uumbaji, ni vitu ambavyo mipango na taarifa zake zilikuwepo kabla hata matukio hayo hayajaandikwa. Na sisi watu wa imani hizo story hazitusumbui kabisa mkuu kwa sababu tunaamini Shetani anaknowledge ya mambo hayo, hata kabla hayajaandikwa. Na kazi yake siku zote zaidi ya kudanganya ni kufanya counterfeit ya ukweli.
ndio maana pamoja na matukio hayo ya kale kuendana lakini hayafanani 100% na kile cha bibilia.
mfano;
Sababu ya gharika ya Nuhu ilikuwa ni suala la maadili na ilikuwa wafe wote isipokuwa nuhu na familia yake.
lkn matukio hayahaya yaliingizwa kwenye historia za wamistri, wamesopotamia ili yakidhi culture zao.
Mfano sababu ya gharika kwenye moja ya hizo story ni miungu kulia njama na kutaka kumfitini mwanadamu wao.
hata wengine walilalamika sana kuona jamaa aliponyoka kwenye gharika.
ndio maana watu wengi wafuasi wa hizo myth huwa ni wale wenye stress na misongo ya mawazo. maana huwezi kupinga ukweli ukabaki salama.
 
1:maandiko ya bibilia yanajithibitisha yenyewe kuwa sio copy and paste kutoka popote(2tim3:16, 2peter 1:21,zaburi 119:160) kwa tunaoamini hilo huwa tunaishia hapo.
2:ukifuatilia geneology ya bibilia utagundua dunia inakama takribani miaka 6000 na ushee, na mafuriko yalitokea miaka zaidi ya 4360 iliyopita.hao jamaa waliotawanyika dunia nzima waliondoka na mwangwi wa ukweli huo japo Mungu aliamua kufanya kazi na Israel ili kupitia wao dunia nzima ibarikiwe. Binafsi kuona hayo kunaniongezea imani kwa Mungu zaidi.

3:sio egypt tu, wala huko babeli karibu kila kona ya dunia na desturi zao hata kijijini kwenu utakutana na matukio au desturi zinazofanana na za kwenye bibilia mfano ' kafara' hata kabla bibilia haijawafikia. hiyo inaonyesha fact moja kuu kwamba wote tu ndugu, na tuna chanzo kimoja na matukio yote ya kwenye bibilia ni sahihi. achilia mbali kaanani ambao walikuwa hadi na hema ya kukutania kama ile Mungu aliyowaambia waisrael. Sababu kubwa ni kwamba walitawanywa pale babeli(mesopotamia) muda mfupi baada ya garika na miaka kadhaa baada ya uumbaji. nenda china, nenda nigeria yoruba people, nenda america kaskazini, nenda kusini, nenda ufilipino,india,kote huko watakuelezea stori za mafuriko kama ya nuhu. hiyo kwetu sisi ni uthibitisho bibilia ni halisi na zote hizo ni uthibitisho kuwa baada ya nuhu watu walisambaa dunia nzima kama inavyoelezwa na bibilia
 
kunastory kama za noah zaidi ya miatano duniani kila kona mfano hapo juu. hadi tanzania zipo kabla ya hata ukristo.
huoni huu ni ushahidi wa grobal flood.
lkn pia huoni hizo timing zinaweza kuwa doctored kufavour hao wakosoaji wa bibili



Mwanafalsafa Plato aliirejea biblia wakati anaandika Moral issue kuhusu Mji wa Athens akiita "Hebrew bible" so bible ime exited kwa karne nyingi kuliko dini nyingi
 
Unaweza kujadili yaliyomo katika kitabu bila kuyaamini.
Biblia si kitabu tu cha dini bali pia cha historia, sheria nk. Lakini kama vitabu vingine(vya hesabu, afya nk) unatakiwa ukiamini kwanza ndipo unaweza kwenda mbele. Usipoamini yaliyoandikwa kwenye kitabu cha afya hamuwezi anza kujadili yaliyomo.
 
hivi Wewe jamaa utawatenganisha vipi wayahudi na Mila za kale za waashuru?
Tatizo lako wewe umekomaa na historia nusu ya Wayahudi bila kuona chanzo Cha mwanzilishi wa Imani hiyo Yaani Mzee abrahamu na Jamii alizotokea Mimi nimeanza kuchimbua historia ya Abraham kabla hajahama na baba yake Mzee Terra kutoka uru ya wakaldayo mpaka kwenye marago ya kaanani na kuweka makazi pale,
Sasa utamtenganishaje babu ya Wayahudi na Mila za Mesopotamian?
Kwanza huyo Mzee mwenyewe alikua anaabudu miungu ya waashuru mpaka pale Merchizedec mtawala wa Salem alipompa ujuzi wa Mungu El Murduc hapo ndipo jamaa akachange akaanza Jenga madhabahu za Mungu El na kumwabudu
Sasa turudi kwenye source ya huyo mungu wa Merchizedec alikua Mungu Gani katika Aina ya Ile miungu ya ANNUNAKI?

Utapiga chenga weeeeee ila utarudi pale pale kwenye kwenye chanzo Cha miungu napokazia Mimi!
 
Historia ya binadamu kwenye biblia haizidi miaka 6000.
Kunao ushahidi wa kuwepo Kwa binadamu kati ya 200,000yrs - 300,000,000yrs.
Na mbona Mungu awafiche binadamu mambo kadhaa ilhali ndiye muweza yote na mwenye yote?

Siku ambayo Mwafrika ataondokea huu upuzi wa Kanisa na dini za kizungu/kiarabu, hata sisi wenyewe tutafika kwenye sayari zingine na kumaliza umasikini.
 
Biblia imetaja pia watu kuwepo kabla ya Adam, hilo fungu lipo. Tatizo ninalosema hapa ni kuwa watu hawsomi Maandiko Matakatifu kwa umakini unaostahili, wanapita tu WAWAWAWAWA utafikiri nyuki wamepigwa jiwe wakiwa ndani ya mzinga
 
Kwa mujibu wa biblia,kutoka adam mpk sasa ni takribani miaka 6000

Ila dunia kama dunia ina umri wa miaka mingi sana.

Katika biblia ukisoma kwa makini, uumbaji ulivokua, inasema roho wa Mungu ilitulia juu ya uso wa maji kwenye giza totoro.

Ndipo Mungu akaanza kusema iwe NURU,Nuru ikawa,kisha maji yajitenge na nchi kavu,ikawa.
hii inamaanisha wakati Mungu anasema hivo maana yake giza lilikuwepo,maji yalikuwepo, na dunia ilikuwepo.
pia hii inamaanisha wakati Mungu anasema hivo sio kwamba ndio alikua anaumba ulimwengu kwa mara ya kwanza,bali alikua anarejesha vitu vilivyokuwepo.yaani dunia iliumbwa miaka mingi sana kabla ya kuumbwa Adam.


Hii pia inamaanisha kua Wakati roho wa Mungu ipo juu ya uso maji, maana yake kabla ya kusema iwe nuru, maana yake giza lilikuwepo, maji yalikuwepo ila yamefunika dunia nzima,maana yake Ardhi/nchi ambayo maji yapo juu yake ilikuwepo kabla.

Hii inamaanisha kuna viumbe vilikuwepo kabla ya uumbaji wa adam ila Mungu aliviadhibu kwa Kuvipiga na Maji na giza totoro vikapotea, ndipo baadae Mungu akaona aumbe viumbe vingine kwa mfano wake hii inamaanisha kabla ya uumbaji wa adam.Kuna viumbe vilikuwepo katika hii dunia ila havikufanana na Mungu,Vikaasi Mungu akavikatilia Mbali kwa kuvipiga na Maji na giza.
Ndio maana baadae kabisa utaona Mungu alikiari hata iangamiza dunia tena kwa maji akaweka agano na binadamu. Maana yake ilikua ni tabia ya Mungu hapo kabla kuadhibu dunia kwa maji pale inapomuasi.

Maana yake kabla ya kuumbwa binadamu kabla yetu kuna viumbe walishaikalia hii dunia,ndio maana leo hii kuna baadhi ya miji inapatikana baharini ikiwa imefunikwa na maji.
yaani kuna civilisation ilikuwepo kabla ya binadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…