Miaka ya 2000's nlifungua Internet Cafe. Ndipo nlipoanzia kupiga bingo na kupasua mioyo

Aisee miaka hiyo kuangalia matokeo ni mpaka mbandikiwe shuleni au mmpigie mtu aliyeko Necta tofauti na hapo hamna lkn siku hiz,enzi hizo mwendo wa barua tu na zinapitia posta......tumetoka mbali kwa kweli

Ila mzee ulipiga hela si utani
Nakumbuka ndugu walikuwa wakija kijijini kutoka Dar.
Tunajipinda kuandika Barua wawapelekee ndugu wengine wa Dar.
 
Unasema ulikuwa na hela na internet cafe? Unatupanga. Wenye hela walikuwa kina mpakanjia, na kina ndama mtoto wa ng'ombe, muzamil yang millionea na papaa msoffee.
 
Unasema ulikuwa na hela na internet cafe? Unatupanga. Wenye hela walikuwa kina mpakanjia, na kina ndama mtoto wa ng'ombe, muzamil yang millionea na papaa msoffee.
Hao nyie mateja ndo mlikuwa mnawafahamu sana. Sisi tulikuwa tunafahamika na watoto wa kidosi na walioenda shule.... 🤣
 
Wazee wa Java tulikuwa tukijifungia ndani kusaka magemu kwenye Waptrick. 😆

Nashangaa watoto wa Android na IOS wanavimba!
 
Kaka unanikumbusha mbali ila kwa kipindi kile km ulikuwa na ofisi hizo aisee ww ni mkongwe [emoji1][emoji1][emoji2].

Mlikula sana ela zetu unanikumbusha Magomeni mapipa seaboys pale wana tulikuwa tunaenda kuangalia pilau ujana maji ya moto sana aisee.

Aisee unanikumbusha Steven Kanumba kipindi hicho yuko Kaole hana hili wa lile kipindi hicho ndo anaanza kuigiza ilikuwa ikifika week end anakuja kushinda kwenye messenger kwenye ofisi za internet seaboys. Daah kweli mda haurudi nyuma aisee.
 
Umenikumbusha ndugu yangu mmoja ni marehemu Sasa.....alikuwa anaishi maisha ya kipedeshee kwa kuuza CD za ngono......alikuwa anaheshimika Sana Kwa wateja wake.... alikuwa anawauzia mpaka wabunge na mawaziri.......
 

Seaboyz chini juu rasi simba ana fundisha kila mtu kwa wakati wake yeye mwenyewe.usipo jua anakurudishia pesa yako,jamaa muongo sana yule
 
Ila miaka 90 mpaka 2003 kila eneo lilijulika lina watu waina gani na makuzi gani.
Ukienda TMK ni watu wa kuzamia na mabaharia
ukienda Magomeni ni wauza unga na mashangingi
Ukienda sinza ni wakishua na watafutaji
ukienda mazenzese,buruguni na tandika ni sehemu
za waswahili
ukienda ubungo,gongo lamboto,tabata,airport na mwenge ni wazee wastaafu wa jeshi na waliochelewa kuja mjini kumiliki katikati mjini
ukienda ilala,msimbazi,kinondoni na magomeni kidogo wenye mji wao Mzizima na wajanja wa Dar
 
Ha ha ha... Tulikula pesa zenu na dada zenu sana miaka hiyo.... Hongera nawe umeanza ujanja kitambo sana miaka hiyo wengi wapo SITIMBI AU SANVULA CHOLE huko....
 
Umazaliwa mwaka gani !. ao unawowataja wameanza kuwika miaka 2004
Madogo hawa wakishavuta vipisi vya bangi za kugongea basi wanaona wanajua some stuff ...katakuwa katoto ka miaka ya 2000 au 1990s mwishoni. Subiri kaje kukujibu.
 
Mara ya kwanza naanza kuwa na simu ya android zikianzia HTC watu walikuwa wanazikataa kipindi hiko hipo NoKia ,samsung,moto na BB
😆 HTC ilikuwa ni simu ya heshima mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…