Leo asubuhi nilikuwa naangalia tv moja ya Korea kusini nilishangazwa na maendeleo hafifu ya hawa jamaa na nilipoangalia historia nikakuta kumbe miaka ya Uhuru tulikuwa karibu sawa.
Wakati Tanzania tumepiga hatua kubwa kiasi hiki wao bado wamelala usingizi mzito.
Sisi tunatengeneza Magari, electronics, kilimo uhakika wao bado wanajivuta.
Wataalamu wa uchumi,shida ni Nini kwa hawa ndugu zetu?
1. Ni wavivu sana. Wanapenda sherehe na starehe kuliko kazi
2. Hawakuipa Elimu kipaumbele. Ndiyo maana mpaka Sasa kuna raia huko wasiokuwa kusoma na kuandika. Katika Moja ya ziara zangu huko, nilibaini kuna baadhi ya vijiji vyake ambako wazazi huwashawishi watoto wao, hasa wa kike, kuandika majibu ya uongo kwenye mitihani ya darasa la saba ili wasichaguliwe kwenda Sekondari. Kwao, watoto wao kusoma kujicheleweshea mahari.
3. Mfumo wao wa uchumi walioukumbatia muda mfupi baada ya uhuru ulichangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha kasi ya Maendeleo.
4. Mipango ya kukurupuka. Kila Rais anayeingia madarakani anaingia na Mipango yake na kupelekea baadhi ya iliyoanzishwa na watangulizi wake kutupiliwa mbali au kuwekwa kando kwa muda.
5. Watu wake wengi hawana exposure na mambo ya mataifa mengine. Katika ukanda wake, inaweza ikawa ndiyo nchi inayoongoza kwa watu wake kutokwenda nchi zingine. Hata utoaji tu wa passport ni nongwa haswa. Hawatoi passport mpaka kusudi la safari lithibitishwe. Wakati mwingine, huweza kutakiwa hata kuonesha tiketi ya ndege kabla ya kupewa passport.
6. Ubinafsi nao umetawala. Hiyo imepelekea rushwa kutamalaki. Wakati fulani, ilishawahi kupewa na jina lililopunguza makali, badala ya rushwa, ilibatizwa jina la takrima.
7. Hawaamini katika uwajibikaji. Kwao, kiongozi wa umma ni bosi, siyo kama kwetu ambako kiongozi ni mtumishi wa umma. Viongozi wetu wanajitahidi sana kutumika kwa uaminifu kwa sababu wanajua wakizembea tutawawajibisha.