Unachanganya mambo, miaka hiyo ilikuwa ni English monarchy kwa hiyo ni english monarchy ndiyo iliyokuwa sawa au zaidi ya Korea lkn siyo sisi, sisi hatujawahi kuwa sawa au kumzidi yoyote yule kiuchumi, …
Mkuu, inaelekea hujamwelewa mtoa mada! Au wewe hukuangalia taarifa ya habari?
Unailinganisha nchi yetu na Korea? Haujui tulivyowaacha mbali kiuchumi? Tukoo mbali sana kimaendeleo, Korea hawatufikii hata kidogo. Au niseme hawatukaribii hata kwa mbaaali!!!
Sisi tuna viwanda vikubwa vya kutengeneza magari. Nitajie alau hata kimoja cha South Korea, kitaje kama kipo. Hawana kiwanda cha magari, bado unatulingamisha nao?
Sisi tuna maviwanda ya maana ya electronics, shipbuilding, telecommunications, chemicals, steel etc. Wao Wana vinavyotambulika dunianai? Wana viwanda gani vinavyoheshimika Kimataifa? Labda vyerehani vinne?
Unajua cherehani? Ile ya kushonea nguo. Zikiwa nne, zinaitwa kiwanda kwa huko kwake! Unajua Wakorea wanachekesha sana ee!!! Vyerehani vinne ni kiwanda? Sijui maajabu yataisha lini Korea! Si waje kwetu kujifunza uchapa kazi?
Kama Wakorea wamekutuma uje kuwapigia debe kuwa wameendelea kama sisi, waambie hatudanganyiki. Sisi tupo level nyingine. Wawatafute "watoto wenzao", watuache sisi na wakubwa wenzetu!
Unataka wa kutulinganisha nao? Nakutakia wachache: Japan, Singapore, Malaysia, Srilanka, alau kidoogo, japo naye bado ni kabwana mdogo, lakini alau afadhali kidogo, South Africa. Bora utulinganishe hata na "dogo" South Africa kuliko katoto kadogo kama Korea.
Umenipata kiongozi? Namaanisha, mtoa uzi hajakosea!