Michae Maluwe kumbe na wewe hujui Kingereza?

Michae Maluwe kumbe na wewe hujui Kingereza?

Huu ni ulimbukeni wetu tu, wenzetu wanaamini katika lugja yako ya kwanza/lugha mama. Angekosea Kiswahili kama lugha yake ya kwanza ningeelewa vyema. Kingereza kama lugha ya pili siyo suala la kutengenezea ujumbe wa kumsimanga mtu kwani kujua lugha husika si kuwa maarifa husika kwenye fani.

Hata hiyo uliyotoa wewe wajuvi wa mambo wanaweza kutohoa ukajikuta bado uko mbali na ukweli.
Angeongea kiswahili tu,ulimbukeni ni kujifanya unajua kitu kumbe hujui
 
Una Mawazo Kama Majirani zetu Wakenya.....!

Inaitwa assimilation..! Wenyewe wanatuona WaTz tuko nyuuuuma eti hatujui Kiingereza...teh teh..!

Sasa Nenda Kwa Wenye kujiamini na Lugha zao kama India,China n.k ..Hawa hawashobokei Lugha za Watu..!

Ifike Mahali tujiamini na Lugha zetu.
Hao sio lugha tu hata utamaduni wa kigeni hawataki lakini sisi waafrika ndio wa kupapatikia tamaduni za kigeni labda kuliko hata wenye tamaduni zenyewe. Waafrika bure kabisa.
 
Anaweza akawa sahihi kwa sisi tunaojua kingereza usitafisiri neno kwa neno mkuu yeye hajaongelea tukio ameongea uwalisia wa jambo mfano " unatengeneza nafasi ila magoli hakuna" kutokana na muda uliopo hakuongelea tukio la mpila kaongelea kwa uwalisia wa jambo, present tense always he, she , it creates, ila kutokana ni i, you , they ndo maana katumia creat present continues tense
 
Captain Michael Maluwe sioni sababu ya kumponda as long as Kocha alilielewa swali mbona Wazungu huwa wanaongea kiswahili cha kuchekesha hatuwajaji ?
Kwan wazungu wanajua au hawakosei kiswahili wacheni upumbavu
 
Mechi ya KenGold inaisha
Mtangazaji Michael Maluwe anamuuliza kocha mzungu
""You create the chance.......
Badala ya ''you created some chances.....

Kweli lugha ngumu
Mbna mnaabudu sana kiingereza... hizo grammar error mnazikomaliaaaa... kweli ukoloni mambo leoooo hautaishi
 
mimi kingereza najua , ila sio kile cha maongezi ya kawaida ni technical english, ukinisikia utadhani unasoma kitabu cha chemistry na broken kama kawaida, hata gamond anachapiaga , for me we are playing like we train,
 
Ulishawahi kumsikiliza Gamondi anavyoongea? Broken English kibao ila hasemwi kwasababu yeye ni mzungu...
 
unamshangaa huyo...Lamine yamal alikua anauma meno kwenye usiku wa tuzo....kila mtu na lugha yake buana
habari gani?
 
Mechi ya KenGold inaisha
Mtangazaji Michael Maluwe anamuuliza kocha mzungu
""You create the chance.......
Badala ya ''you created some chances.....

Kweli lugha ngumu
Sasa hapo unashangaa nini? Kwani kiingreza ni lugha yake? Kwani muingreza akikosea kiswahili naye utamcheka? Wakati wa ukoloni kulikuwa na watu wanaitwa manyapala, walikuwa wakijua kuongea kiingreza hata cha kuombea maji wakajiona wazungu wakatumika na wazungu kunyanyasa wasiojua kizungu! Naona na wewe uanajiona mzungu kwa kujua kizungu! Pole sana kwa utumwa huo!!!
 
Sasa hapo unashangaa nini? Kwani kiingreza ni lugha yake? Kwani muingreza akikosea kiswahili naye utamcheka? Wakati wa ukoloni kulikuwa na watu wanaitwa manyapala, walikuwa wakijua kuongea kiingreza hata cha kuombea maji wakajiona wazungu wakatumika na wazungu kunyanyasa wasiojua kizungu! Naona na wewe uanajiona mzungu kwa kujua kizungu! Pole sana kwa utumwa huo!!!
Angeongea kiswahili,acheni kutetea ujinga
 
Ujinga hapo ni upi? Kutokujua kiingreza au kutokuongea kiswahili?
Kuongea lugha usiyoijua vizuri mubashara,dunia nzima inakushangaa,TV ni chombo rasmi cha mawasiliano sio.
 
Huyu Michael Maluwe wa zamani Sana. Nilianza kumuona anatangaza kipindi Cha michezo ITV 1999/2000 miaka Kama 24 iliyopita
Alikuwa ananikera kipindi hicho, kila kipindi zaidi ya nusu ni basketball tu
 
Back
Top Bottom