Asee nimeufuatilia huu Uzi kimya kimya tangia mwanzo na sikutaka kuchangia chochote but nimejikuta nalazimika tu.
Anyways, nianze kwa kutangaza interests zangu kwamba Mimi Shabiki mkubwa wa wote hawa hivyo sitegemei maandishi kuwa na upendeleo wa upande wowote.
Nikianza na MJ who was considered to be "The instrument of the world" in case of entertainment.. mj alikuwa the best entertainer to ever walk in this world...alikuwa anajua kucompose mziki wa kuburudisha na kuinspire watu kwa namna ya ajabu sana. Michael Jackson is truly definition of a musical genius..anajua kucheza, anajua kuimba, anajua kuprovoke hisia za hadhira yake ndio maana akiwa mtoto kabisa alikweza kuwa star wa band ya nyumbani kwao ya Jackson 5, Kuna kitu hatuwezi kumnyanganya Michael he was a musical genius and natural talented.. aliekulia Kwenye spotlight na platform kubwa, world class music facilities, great producers and directors akina Quincy Jones e.t.c kutoboa kwake kulikuwa hakuepukiki.
But Bob Marley was beyond musical genius, alikuwa na kipawa cha unabii ndani yake kama nyongeza yake..mazingira aliyozaliwa na kukulia walikuwa magumu na hatari..alizaliwa baada ya mama yake kubakwa na mkoloni mzungu Sinclair Marley then akatelekeza yeye na mama yake pale Kingston Jamaica wasijue la kufanya hapa ndipo "No woman no cry" ikatengenezewa.. He was born fatherless. Akawa Fundi welding na baadae msoma viganja vya watu then akaachana navyo na kujiunga na Peter tosh na Bunny wailer kufanya music then yaliyofuata ni history tamu ya kazi nzuri zisizosahaulika milele.
Bob alikuwa na charismatic ya kuongea jambo likapokelewa kwa nguvu ya ajabu na watu..rejea aliweza kusimamisha vita iliyokuwa inataka kuibuka Jamaica then akaitisha concert ya one love maadui wa kisiasa wakawambia wafuasi wao waweke silaha chini wakaja pamoja jukwaani na kuanza safari mpya ya amani na Upendo..likapigwa riddim la love and prosperity all day long.. That's was huge success ya reggae na Marley kwa ujumla.
Nyimbo ya Bob natural mystic ilipewa tuzo ya kuwa song of the century kutokana na mashairi yake kutabiri ujio wa ugonjwa wa ajabu utakaotesa watu na kuua mamilion Duniani soon baada ya ngoma kutoka Ukimwi ukagundulika Afrika na kuanza kuua maelfu ya watu. Nitajadili nyimbo hii kwenye reply inayofuata hapo chini.
Then nyimbo zake nyingi zinatumika katika vyuo mbalimbali kucites cross cutting ishu za philosophy and musicology.
Mwl Nyerere alishawai kumdharau Bob kutokana na muonekano wake kama sisi tunavyomdharau hapa ila Kwenye tamasha la Uhuru wa Zimbabwe Bob alipopanda jukwaani kufanya Sanaa zake Mwl alimwomba aje Tanzania maana kuna Mengi alikuwa anataka kuyasema lakini alikuwa hana lugha nyepesi na ya kueleweka kirahisi kwa watu ila Bob alikuwa anajua hii namna then na kipindi hicho agenda kuu ya Nyerere, Nkurumah, Kaunda e.t.c na afrika yote ilikuwa ni "Africa unite" na Bob ndio ilikuwa dhumuni lake...siku hiyo Mwl Nyerere alishangaa hadi akaenda kumsimulia mwanae makongoro na akaanza kuwa anakula reggae tu za Marley akiwa magogoni..but sina hakika kama alikuwa anakula na sacrament ya akina Marley.. (Weed)...sina hakika.
Bob ana mengi sana tutajaza serve za Max bure.
But wote ni musical genius in their own way but Bob Marley alikuwa na some touch za unabii anaongea jambo then linatokea na amefanya mziki katika mazingira magumu sana ya kutaka kuuwawa na CIA because he was musical powerful. Na walifanikiwa kumpachika cancer kidoleni na aliemuua alikiri last month nadhani akiwa death bed kwamba I killed Bob Marley.
Bob and MJ are truly definition of musical genius