TANZIA Michael Ngaleku Shirima mmiliki wa Precision Air afariki dunia

TANZIA Michael Ngaleku Shirima mmiliki wa Precision Air afariki dunia

Rombo. Wakati jamii ikiomboleza kifo cha mwanzilishi na mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya Shirika la Precision Air, Michael Shirima, imeelezwa namna alivyothubutu kujiuzulu kazi na kwenda kuchoma nyama.

Shirima (80), mzaliwa wa Rombo mkoani Kilimanjaro, alifariki dunia Juni 9, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa tangu Juni 8, mwaka huu.
Msemaji wa familia, Abdallah Singano alisema mwili wa Shirima utasafirishwa kutoka Dar es Salaam Jumatatu kwenda Arusha, utaagwa Jumanne na kusafirishwa kwenda Rombo kwenye maziko yatakayofanyika Jumatano.
Mbunge wa Rombo, Profesa Adolf Mkenda, akizungumzia maisha ya Shirima alisema ameacha historia nzuri kwa Taifa kwa kuwa alikuwa mtu asiyekata tamaa, licha ya changamoto alizopitia.
Profesa Mkenda ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, alisema kitabu alichoandika Shirima na kukizindua mwaka 2022 'On my father's wings' kinaelezea historia ya maisha yake na uamuzi mgumu aliochukua wa kujiuzulu Shirika la Ndege la Tanzania mwaka 1979.
"Niliwahi kumuuliza ni kwa nini aliacha kazi Air Tanzania, aliniletea barua zake kwa nini alitaka kujiuzulu na mpaka leo nina nakala yake, alivyoona shirika linayumba na kuwatahadharisha kwamba litakufa wakiendelea vivyo hivyo, hawakumsikiliza, hivyo akaamua kujiuzulu.
"Alipofika nyumbani mke wake alishtuka sana, lakini wakati huo walikuwa wanakaa nyumba ya Serikali, alikuwa hana kazi, ikabidi aondoke akatafute mahali pa kujishikiza yeye na familia yake, baadaye alianza kufanya biashara ya kuuza nyama choma kidogo kidogo,” alisema Mkenda.
“Alitafuta mkopo akaanza kununua mafuta ya pamba na alipata lori akaanza kuchukua mafuta kutoka Mwanza kuja kuuza Moshi. Wakati anafanya biashara hiyo akagundua Mwanza kuna ujenzi mwingi, lakini mbao zipo upande wa Moshi, akawa anachukua mbao Moshi na kupeleka Mwanza na kurudi na mafuta, alifanya kazi ngumu."
Alisema kwa kushirikiana na mtu mwingine aliyemtaja kwa jina la Kisinani walianza biashara ya kupeleka kahawa nje ya nchi na siku moja rafiki yake huyo alimwambia kuna mtu anahitaji ndege ndogo kwa ajili ya kufanya kazi shambani.
"Hivyo akaanza na ndege ndogo ya kukodi, baadaye akanunua nyingine, ndivyo alivyoendelea mpaka alipofikia leo," alisema Profesa Mkenda.
Alisema atamkumbuka Shirima kwa namna alivyokuwa mtu wa dini na hata alipofikwa na changamoto za biashara alikuwa akifunga novena siku tisa akiomba.
Rais aomboleza
Rais Samia Suluhu Hassan, kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ameandika, “Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Michael Ngaleku Shirima, mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Precision Air.
“Baada ya utumishi wake kwa umma kwa zaidi ya miaka 30 amekuwa sehemu muhimu katika biashara ya anga na shughuli za kijamii katika nchi yetu. Natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki.” Mwenyezi Mungu amweke mahali pema. Amina.”

CREDIT: MWANANCHI
Huyu jamaa alikuwa ni hatari na nusu anamiliki maize flour,5% shares za i&m bank ambayo ndio one of largest bank in Kenya naipo Tanzania pia ana rombo millers anauza kahawa na matunda ulaya,maktau safari lodge ipo tarekea,shares tbl,sanlam insurance, tol,shamba kubwa la kahawa na vitenga uchumi kibao across east africa.
 
Chanzo ni ufisadi kupitia Kodi zetu kupitia mkono wa Mramba alizokwapua akiwa waziri wa fedha kisha akapewa adhabu ya kwenda kupiga picha akifanya usafi hospital ya mwananyamala,kisha akawa waziri wa ujenzi na usafirishaji akaua reli na Air Tanzania ili Precious ikue,na malori na mabus yapate biashara.
Ujinga na umaskini vinakusumbua
 
Kula 10 Mkuu. Yaani watu tunapambana halafu jinga Moja linawaza tu kuwa ukiwa tajiri ni mwizi. Najitolea mfano Mimi nikiwa kijana mdogo kabisa nilianza kuweka bank fixed account Ile pesa napewa kwenda shule I e sehemu ya pocket money. Na nilikuwa siyo Mtumiaji wa pesa hovyo. Nikirudi likizo June na FDR ina mature naongezea na nyingine narudishia. By the time namalizia form 4 nilikuwa na pesa nzuri. Nikiwa nasubiri kuingia F5 nikajipinda kazi mahali miezi kadhaa nikapata pesa nikaongeza FDR. Niliingia chuo nikiwa na millions kadhaa. Nikaongeza na boom FDR ikawa inakuwa kwa speed ya radi. Kwa sabanu ya uchapakazi mzuri lecturers wakaniona hivyo nikawa napewa research assistant tasks na za pesa nzuri Sana. I made millions nikarejesha kwenye FDR. I graduated well nikapata free scholarship na madola ya ukweli. Hapo sasa ndiyo utajua FDR ilikuwa kwa Kasi ipi. By the time namalizia scholarship na degree kadhas unafikiri nilkuwa na millions ngapi? Baadaye nikaingia biashara za Shareholding na biashara nyinginezo clean. Hivi utaniitaje mwizi ukisoma figure za pesa niliyokuwa nayo? Halafu biashara ni akili kubwa. Kwa umri wangu huu situmikii pesa bali pesa Inatitumikia na nimeachana na biashara za kuibiwa. Nafanya biashara za kupigiwa simu au automatic SMS kuwa biashara ime mature njoo tuongee biashara mpya. Katika biashara kila mmoja anachagua inayolipa na Mimi nilichangua stress free businesses na zinazolipa na ambazo hata nikizeeka bado zitaendelea na watoto wanazijua na sharti waziendeleze maana zitakuwa kwenye Foundation. Na nyingi ni silent businesses maana hutasikia Zogwale akitajwa waziwazi kama wengine. Hivyo inabidi kuheshimu struggle za watu japo pia mijizi IPO.
Well said mkuu! Hongera kwa kuwa na financial discipline
 
Mkuu waambie kuwa wachaga wengi biashara zao zinaendelea kwa kuwa wanaweka misimgi imara ya succession ( Wana succession plan). Wajifunze kwa Marehemu Mengi. Pamoja na ufala wa Gold Digger aliyetaka aifilisi IPP Holding ili akaishi Dubai na yule Banake lakini IPP ilisimama imara na walioachwa ambao ni watoto na Management imara. Mengi aliwekeza kwa warithi na alikuwa mjaja Sana hakumuweka Jack na Warithi. Hata ule Wosia kama kweli Mengi alihusika kuuandika basi aliandika kiufundi Sana akijua Jack hatatoboa nao. Chezea Mangi wewe.
Thubutu, mengi kwa jack hakupindua mzee
 
Mtu akishauza hisa za kampuni Kwa watu wengine...hawi tena 'mmiliki"..anabaki kuwa founder...kichwa kingepaswa kusema "muasisi wa Precision air"..
Hana tena majority shares..
He hold 51% vs. 49% holdings by KQ. Therefore he still exercise control on decision making. In this regard he is still the major shareholder, hence the owner.
 
Thubutu, mengi kwa jack hakupindua mzee
Hahaha Mkuu. Daah ndiyo akapinduliwa jumla. Tumepata fundisho kuwa age differences matter a lot. Tusidanganyane age just a number. Not practical kwa mambo mengine so it can't be a universal set but rather a union.
 
Well said mkuu! Hongera kwa kuwa na financial discipline
Sure mkuu. Yaani ninatumaini Sana ujanani tuanze kuwaza maisha ya uzee na unforeseen kwa Afya na uhai. Yaani hapo tungewekeza Sana. Ikifika 40s unakuwa financially stable. Yaani kuna pesa iko mahali haitumiki kwa Jambo lolote lile zaidi ya kuzalisha. Lakini tunapoteza Sana rasilimali fedha na muda ujanani.
 
Matajiri wengi tu wameanzia chini hata huyo marehemu kwahio usiwadharau bruh
Mimi nilianza na Fixed Account ya Sh. 600 nikiwa form One miaka hiyo (over 50 years). Nikawa naongeza kila June nkifunga shule. Je nilijifunzia wapi? Ni maoni na matokeo ya zile hesabu za Darasa la Saba za Principal na interest. Hahaha. Yaani mambo ya fixed and compounded interests. Froma a very poor family I made it. Hivyo waliojitajidi waheshimiwe na mali zao ziheshimiwe. Na kifupi sijawahi kuiba hata kipindi nimeajiriwa nilikuwa narudisha excess Imprest Ofisini na kila Mtu alikuwa anashangaa. Mafanikio yanawezekana bila wizi. Ni kuamua na kuweka jitihada tu. I am not a billionaire but I supper live a financially stress free life. Hicho ndiyo cha misingi.
 
Mimi nilianza na Fixed Account ya Sh. 600 nikiwa form One miaka hiyo (over 50 years). Nikawa naongeza kila June nkifunga shule. Je nilijifunzia wapi? Ni maoni na matokeo ya zile hesabu za Darasa la Saba za Principal na interest. Hahaha. Yaani mambo ya fixed and compounded interests. Froma a very poor family I made it. Hivyo waliojitajidi waheshimiwe na mali zao ziheshimiwe. Na kifupi sijawahi kuiba hata kipindi nimeajiriwa nilikuwa narudisha excess Imprest Ofisini na kila Mtu alikuwa anashangaa. Mafanikio yanawezekana bila wizi. Ni kuamua na kuweka jitihada tu. I am not a billionaire but I supper live a financially stress free life. Hicho ndiyo cha misingi.
Unavutia kukufatilia, naweza kukuona ama kuwasiliana na wewe kwa private message?
 
Back
Top Bottom