bongo dili
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 12,350
- 25,180
Mimi mzima kiroho na kimwili ndugu
Unaweza ukawa ushakufa huwezi ishi ukiwa hujui maana ya kuishi upo upo tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaweza ukawa ushakufa huwezi ishi ukiwa hujui maana ya kuishi upo upo tu
Chanzo ni Kodi zetu kupitia mkono wa Mramba alizokwapua akiwa waziri wa fedha kisha akapewa adhabu ya kwenda kupiga picha akifanya usafi hospital ya mwananyamala,kisha akawa waziri wa ujenzi na usafirishaji akaua reli na Air Tanzania ili Precious ikue,na malori na mabus yapate biashara.Mi nasubiri za kuona chanzo cha utajiri wake ni nini? Maana kama Mzee Edwin Mtei aliiba pale BOT etc, huyu lazima kuna chanzo ambacho siyo sahihi
Chanzo ni ufisadi kupitia Kodi zetu kupitia mkono wa Mramba alizokwapua akiwa waziri wa fedha kisha akapewa adhabu ya kwenda kupiga picha akifanya usafi hospital ya mwananyamala,kisha akawa waziri wa ujenzi na usafirishaji akaua reli na Air Tanzania ili Precious ikue,na malori na mabus yapate biashara.Huwezi kusema tu hakuuza mbao wakati hujaonyesha kwa ushahidi alifanya ufisadi gani! Hii ndiyo point yangu. Point yangu ime-base kwenye utamaduni ulio kwenye jamii yetu (kwa taarifa yako jamii yetu ni maskini hata kama wewe ni tajiri) kuwa kila tajiri ni fisadi. Kuhusu kuwa na akili kunizidi, well, that is how you think, and it is not necessarily how it is! Unafikiri kuna mjinga anayejitapa kwa ujinga? Mara nyingi wajinga ndiyo hujitapa wana akili.
Yupo kwenye Miaka yake ya kiblibliaInasikitisha sana, lakini inatukumbusha ya kuwa maisha ya hapa duniani yana mwisho na wote tutaondoka; tuishi kwa kumpendeza allah
Siyo wote Mkuu. Wengine tuna vyanzo clean kabisa. Kuna Yule MTU wetu alikuwa anataka matajiri wageuke mashetani. Sasa akamtaka jamaa mmoja aweke vyanzo vya utajiri na awasilishe statement za bank zote. Jamaa alipeleka vyanzo vyote na mwenye wivu akabana ngenge. Kisa tu kumbe ni kwa vile tajiri alikuwa mchaga na yeye ilikuwa damu kunguni kwao. Mungu fundi.Alale mahali pema anapostahili.
NOTE: Hakuna tajiri anayeweza kukueleza kiini cha utajiri wake hata siku moja.
Nimeona kagusia kuhusu kuuza kahawa, udereva wa malori n.k ilikuwa hatua nzuri pia
IPP bado ipoNina Imani kamapuni itaendelea kuwepo,
Maana wamatumbi akifa mmiliki na kampuni lazima ipate misuko misuko.
RIP
Bado Late Shirima ni majority shareholder maana anamiliki 42% plus na nyingine zilizobaki zinamilikiwa na minority waliojigawa ikiwemo Kenya Airways 41%, wafanyakazi 2% Precision na Public 14%. Muwe mnafanya kautafiti kidogo ili ukisema Jambo usionekane ni chuki. Pamoja sanaIlishamilikiwa na watu wengine kitambo alibaki na share kidogo sana.
Kweli. Utasikia kamtoa kafara fulani, Freemason.Tatizo la kuzaliwa kwenye umaskini na ujinga. Angalia sana hata vijiji vyenye watu maskini na wasio na elimu. Kila anayefanikiwa wanasema ni chinjachinja au lazima apewe jina baya
Mkuu waambie kuwa wachaga wengi biashara zao zinaendelea kwa kuwa wanaweka misimgi imara ya succession ( Wana succession plan). Wajifunze kwa Marehemu Mengi. Pamoja na ufala wa Gold Digger aliyetaka aifilisi IPP Holding ili akaishi Dubai na yule Banake lakini IPP ilisimama imara na walioachwa ambao ni watoto na Management imara. Mengi aliwekeza kwa warithi na alikuwa mjaja Sana hakumuweka Jack na Warithi. Hata ule Wosia kama kweli Mengi alihusika kuuandika basi aliandika kiufundi Sana akijua Jack hatatoboa nao. Chezea Mangi wewe.IPP bado ipo
Huyu mwamba hakuwahi kuandika kitabu cha historia yake?View attachment 2652129
Mmiliki wa Shirika la Ndege Nchini Tanzania la Precision Air, Michael Ngaleku Shirima, ameaga dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya AgaKhan, Jijini Dar es Salaam
===========
Mfahamu zaidi Michael Ngaleku Shirima
Michael Ngaleku Shirima CEO wa Shirika la Ndege za Precision Air alianza kufahamika zaidi na watu baada ya ndege za shirika kukumbwa na tafrani za hapa na pale zikihusisha ajali iliyotokea jijini Mwanza ambapo ndege ya shirika hilo ilishindwa kutua katika uwanja wa ndege Bukoba na kulazimika kugeuka Mwanza ambapo rubani aliona ni vyema kuishusha ndege hiyo kweye maji ya ziwa Victoria.
Michael Shirima ni moja kati ya wapambanaji ambao wamepambana kutoka chini hadi kufikia mafanikio ya juu kwa kuwa alikuweka ujasiri na kutokata tamaa. Michael alizaliwa mwaka 1943 huko Usseri Rombo Mkoani Kilimanjaro, baada ya kumaliza shule na kila kitu aliamua kuingia katika ulimwengu wa wachakarikaji kukimbiza ndoto zake ambazo alizigeuza kuwa mipango na baadaye utekelezaji.
Michael aliajiriwa kwa muda kidogo na hapa anasema “Nilipokuwa naanzisha Shirika la ndege la Precision Air haikuwa kama lilivyo sasa hivi lilianza kidogo, likakuwa. Nimekulia kwenye Taasisi ya usafiri wa anga. Nilipofikisha miaka 18 ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia kwenye mambo ya ndege (ilikuwa ndege ndogo). Ndipo ilipoingia kwenye damu na ijapokuwa nilibadilisha mawazo mara kwa mara lakini nilirudi kwenye wazo langu. Sikuanzisha Precision Air moja kwa moja lakini nilifanya kazi kwenye Shirika la ndege ya East African Airways kwa miaka 12 Jijini Nairobi. Lilikuwa ni Shirika la Afrika Mashariki Tanzania, Kenya na Uganda”
“Mtaji wa kuanzisha Kampuni ya Precision Air niliutoa kwenye Kahawa. Ni kazi ambayo ilikuwa haifanywi na watu wengi. Na pia nilikuwa dereva wa malori. Nilikuwa napeleka mizigo Mwanza kutoka Moshi. Nilikuwa napeleka mbao kule. Pia nilikuwa nanunua mafuta ya pamba naleta Moshi” Mzee Michael Shirima, Founder wa Precision Air na Mwandishi wa kitabu cha On My Father Wings
“Tuna wafanyakazi 300. Hii kazi ni ngumu Sana, sio watu wengi wanaweza kuifanya. Kuna Mtaalamu aliandika kwamba ukitaka kuwa Milionea (Dola kwa mfano) uwe Bilionea halafu uingie kwenye kazi ya kuendesha Shirika la ndege ndio utakuwa Milionea. Na huingii kwenye kazi hii ili uwe tajiri au utengeneze fedha hapana unaingia kwenye kazi kwa sababu ya kupenda passion. Na Mimi sifanyi kazi kwa maono nafanya kazi iliyopo sasa hivi”
Ameuza 49% ya Hisa Kwa KQMtu akishauza hisa za kampuni Kwa watu wengine...hawi tena 'mmiliki"..anabaki kuwa founder...kichwa kingepaswa kusema "muasisi wa Precision air"..
Hana tena majority shares..
Kula 10 Mkuu. Yaani watu tunapambana halafu jinga Moja linawaza tu kuwa ukiwa tajiri ni mwizi. Najitolea mfano Mimi nikiwa kijana mdogo kabisa nilianza kuweka bank fixed account Ile pesa napewa kwenda shule I e sehemu ya pocket money. Na nilikuwa siyo Mtumiaji wa pesa hovyo. Nikirudi likizo June na FDR ina mature naongezea na nyingine narudishia. By the time namalizia form 4 nilikuwa na pesa nzuri. Nikiwa nasubiri kuingia F5 nikajipinda kazi mahali miezi kadhaa nikapata pesa nikaongeza FDR. Niliingia chuo nikiwa na millions kadhaa. Nikaongeza na boom FDR ikawa inakuwa kwa speed ya radi. Kwa sabanu ya uchapakazi mzuri lecturers wakaniona hivyo nikawa napewa research assistant tasks na za pesa nzuri Sana. I made millions nikarejesha kwenye FDR. I graduated well nikapata free scholarship na madola ya ukweli. Hapo sasa ndiyo utajua FDR ilikuwa kwa Kasi ipi. By the time namalizia scholarship na degree kadhas unafikiri nilkuwa na millions ngapi? Baadaye nikaingia biashara za Shareholding na biashara nyinginezo clean. Hivi utaniitaje mwizi ukisoma figure za pesa niliyokuwa nayo? Halafu biashara ni akili kubwa. Kwa umri wangu huu situmikii pesa bali pesa Inatitumikia na nimeachana na biashara za kuibiwa. Nafanya biashara za kupigiwa simu au automatic SMS kuwa biashara ime mature njoo tuongee biashara mpya. Katika biashara kila mmoja anachagua inayolipa na Mimi nilichangua stress free businesses na zinazolipa na ambazo hata nikizeeka bado zitaendelea na watoto wanazijua na sharti waziendeleze maana zitakuwa kwenye Foundation. Na nyingi ni silent businesses maana hutasikia Zogwale akitajwa waziwazi kama wengine. Hivyo inabidi kuheshimu struggle za watu japo pia mijizi IPO.Hizi akili za kila aliyefanikiwa Tz ni mwizi Kuna kiongozi mmoja mshamba amewahi kutuongoza ndiye aliyeturithisha haya mawazo! Tumekuwa na taifa la kishamba sana, yaani badala ya kupambana tuwe na matajiri wengi watz halisi (achana na hao wenye uraia wa nchi nyingine), tunawapiga vita kwa kuwaita wezi! Tz tuna takrinan watu 40m walio ktk umri wa kufanya kazi, serikali imeajiri watu almost 1m (hii ni kuanzia Katibu mkuu kiongozi Hadi mtendaji wa Kijiji)! Wengine wote wameajiriwa na sekta binafsi, alafu anatokea mpuuzi mmoja anapambana na sekta binafsi! Puuzi kabisa
41%Ameuza 49% ya Hisa Kwa KQ
Mbona una hasira Sana halafu matusi ya aibu ukubwani?Hawa wana ukabila wa kisenge nasemaje, wachagga tunabaki juu daima.
Kosa Yule jaji kuamua vile,IPP ingeenda kwa yule dada aliyeshindwa kuendesha biashara ya FenichaIPP bado ipo
Ni sawa na kusema taarifa ya CAG ya kupotea kwa zaidi ya trilioni 2 ni ya uongo kwa sababu haijadhibitika hela zilizopotea zilichukuliwa na kina nani. Hela ikipotea njia hii kuna njia nyingine inaingia, kutojulikana imeenda wapi haimaanishi haijapotea.Huwezi kusema tu hakuuza mbao wakati hujaonyesha kwa ushahidi alifanya ufisadi gani! Hii ndiyo point yangu. Point yangu ime-base kwenye utamaduni ulio kwenye jamii yetu (kwa taarifa yako jamii yetu ni maskini hata kama wewe ni tajiri) kuwa kila tajiri ni fisadi. Kuhusu kuwa na akili kunizidi, well, that is how you think, and it is not necessarily how it is! Unafikiri kuna mjinga anayejitapa kwa ujinga? Mara nyingi wajinga ndiyo hujitapa wana akili.
Na kweli yule dada kichwa chake hakina akiliKosa Yule jaji kuamua vile,IPP ingeenda kwa yule dada aliyeshindwa kuendesha biashara ya Fenicha
Ukibahatika kusoma riwaya ya the godfather ya Mario puzo , ukurasa wa kwanza kabisa mwandishi anaanza na nukuu inasema kwamba " behind every great fortune there's crime" . Upo sahihi kwa hiki ulichokisema hapa.Ni sawa na kusema taarifa ya CAG ya kupotea kwa zaidi ya trilioni 2 ni ya uongo kwa sababu haijadhibitika hela zilizopotea zilichukuliwa na kina nani. Hela ikipotea njia hii kuna njia nyingine inaingia, kutojulikana imeenda wapi haimaanishi haijapotea.
Vilevile kwenye biashara kuna vitu wazi kabisa, kuna mfanyabiashara mmoja mkubwa bongo ni co-owner wa viwanda viwili vya bidhaa moja muhimu, pamoja na biashara nyingine. Kwenye story yake hakuna sehemu atataja jinsi anavyofanya kazi kwa mgongo wa kiongozi mkubwa serikali ya awamu ya tatu na ndio maana akamiliki usimamizi wa viwanda, sanasana atakwambia alivyokuwa fundi magari sijui gereji ghafla story inaruka unakuja kwenye kumiliki viwanda na hapo katikati kuna nafasi wazi.
Umeona kiongozi mmoja mkubwa awamu ya 6 anaenda zindua hoteli uko kwao eti "anachochea uwekezaji" wa mkulima mmoja aliyejenga hoteli. Kiongozi mwingine awamu ya nne alienda zindua shule binafsi ambayo inafanya vizuri sana kwenye matokeo na mmiliki wa hiyo shule eti alikuwa mvuvi na kaishia darasa la saba, na huyo kiongozi hajawahi zindua sio shule tu ya binafsi nyingine, hata vyuo binafsi hajawahi.
Au nawewe ni wale mliokubali Masanja Mkandamizaji alivyoonyesha mali kisha akasema analima mpunga na ana mashine za kulimia ndio anakopata hela, miaka michache tunamuona mkulima wa mpunga kaanzisha kanisa akatumie muda wake kukusanya waumini, mwaka huu akaanza kurusha vipindi studio kwa kulipwa.
Tunarudi palepale kwa Honoré de Balzac, kama mtu hawezi elezea maelezo ya kueleweka kuhusu mali zake ujue kuna jinai nyuma. Huu sio uchawi wala ujinga, huu ndio msingi wa accountability duniani na ndio msingi wa auditing.
Ila kwetu sisi Shabiby akisema alinunua basi at the age of 19 kwa kuuza karanga akiwa shule watu wanakubali, hakuna anayetaka kujua kule Gairo biashara gani ya siri ilitendeka because it was a well executed crime.