TANZIA Michael Ngaleku Shirima mmiliki wa Precision Air afariki dunia

TANZIA Michael Ngaleku Shirima mmiliki wa Precision Air afariki dunia

Shirima wizi wake nauunga mkono ingawa sipendi wezi, unajua hata Nyerere kuna siku alisifia wezi wa mbolea. Kuna mbolea ilikuwa inatolewa kwa ruzuku wanaopewa wanalima hovyo jamaa mmoja akaiba akalima kwa usahihi akapata mavuno mengi na kukidhi haja ya serikali ya uzalishaji wa chakula.

Tuseme mzee Shirima aliibia shirika la Afrika Mashariki, ila hata asingeiba ndege za hilo shirika ziko wapi leo hii? Badala yake asingeiba tusingekuwa na Precision Air na hilo shirika lingevunjwa vilevile tukaambulia historia.
Wizi huu hata maandiko matakatifu yanaubariki
 
Mtoto wake ndiye alikuwa msaidiz wake, shirima ni mmiliki CRDB kwa hisa nyingi sana, wachagga wanatuacha sisi WAGOGO tukikumbatia li-CHAMA lisilo na huruma zaidi ya kutuuza kwa wakoloni wetu wa zamani.
Na NMB pia ni mwanahisa. Na mwaka huu dividends za NMB ni pesa kubwa per share. Na mashirika mengine anazo hisa. Kifupi alikuwa mwekezaji. Rest in Eternal Life M.N Shirima
 
Moja, sijazaliwa familia maskini. Sijui kwa upande wako.
Mbili, mimi sio mjinga na nina hakika nina akili kukuzidi, kama unabisha hili niko tiyari nikupe evidence.

Mchukue mfanyakazi wa Air Tanzania au Kenya Airways auze mbao na kahawa naye awe founder wa shirika la ndege.

Shirima alikuwa na uwezo mkubwa kibiashara, experience ya kazi pamoja na passion ambayo hii ni muhimu mno kwenye biashara hii. Ila kwenye mtaji hapo jifanye aliuza mbao ili usije jiona mchawi na ndio ujione una IQ kubwa
Huwezi kusema tu hakuuza mbao wakati hujaonyesha kwa ushahidi alifanya ufisadi gani! Hii ndiyo point yangu. Point yangu ime-base kwenye utamaduni ulio kwenye jamii yetu (kwa taarifa yako jamii yetu ni maskini hata kama wewe ni tajiri) kuwa kila tajiri ni fisadi. Kuhusu kuwa na akili kunizidi, well, that is how you think, and it is not necessarily how it is! Unafikiri kuna mjinga anayejitapa kwa ujinga? Mara nyingi wajinga ndiyo hujitapa wana akili.
 
Back
Top Bottom