Mimi nilifanya hiviiiiii
Kila kitu kiliishis kanisani, namaanisha ibada ya ndoa hadi chakula cha mchana.
Hapakua na kukodi gari wala dereva, niliendesha mwenyewe, nikapakia wife, tukawapitia wadhamini haooo kanisani.
Watu walivyomaliza ibada ya kawaida, tukaingia ibada ya ndoa, wakati huo catering services zinaendelea nje. Juice za ceres mabox ya kutosha na soda.
Hapakua na kadi za mwaliko wala michango.
Waliokuwepo ibadani, ndugu na marafiki ndio tuliwapa taarifa wajumuike na waumini wengine.
Baada ya ibada na chakula, utambulisho wa ndugu pande za familia zote mbili, tukarudi zetu horelini kuendelea na honey moon.
Hapakua na kelele wala lawama yoyote, wachache wanasema kwanini amefanya hivi wengine wakasema hii ni style nzuri.
Hapo bajeti ilikua watu 200 caterer alifanya 25k kwa sahani. Vinywaji na mambo madogo madogo, ilitumika kama usd 3000 tu.
Zingatia hapo hakuna gharama za ukumbi, MC, sijui mapambo, kukodi magari na makorokoro mengine.
Hiyo pesa inajumuisha na siku tatu za kulala hotelini maeneo ya Ramada, walikua na offer ya Pasaka.
Usifanye jambo kufurahisha watu.