Nilichafanya harusi yangu miaka 6 iliyopita. Sikutaka changisha watu, hivyo nilitoa taarifa kwa magroup ya primary, o-level, a-level na chuo, hawa niliwapa taarifa ya harusi siku nliyotoka toa mahari. Nlituma picha na kuomba michango yao.
Sikuwahi mkumbusha mtu yoyote juu ya mchango wa harusi. Ila wale marafiki wa kweli walinitafuta wenyewe walivyoona tarehe zinakaribia. Hivyo michango nlipata ya wale tu wachache bila bughudha yoyote.
Week kabla ya harusi, nlitoa offer kwa kila group card double 2 kwa angeyeweza fika.
Harusi iligharimu chini ya 6.5mil (total budget) hii ilikuwa ni ukumbi, mapambo, vinywaji, chakula na MC. Mc alikuwepo wa bei ya jioni, alikuja na mziki na cameraman wake, mwendo wa picha tu, hakuna video.
Nadhani ningekuwa nao leo budget yangu isingefika 5.5 mil.
Ningeenda hotel kubwa, ningeomba buffee ya watu 100, budget ya buffee ingekuwa 50k kwa kwichwa, vinywaji average 50k kwa kichwa. Sherehe ingechukua dakika 90. Ni mwendo wa utambulisho, chakula, kuagana. Ukitaka toa zawadi, tuma boda ataleta. 500k ingeenda kwa camera man.
Shughuli imeisha.