Michango ya harusi imekwama, nawezaje kufanya sherehe kwa bajeti ndogo isiyozidi milioni 5?

Michango ya harusi imekwama, nawezaje kufanya sherehe kwa bajeti ndogo isiyozidi milioni 5?

Watu 250 ndio wamechanga ikafika 6M? 😁
Kila mmoja kachanga ngapi sasa?

Budget isiyo rasmi

Watu 250 tafuta wapishi wale wanauza plate moja 10K
So 10K×250 = 2.5M
Vinywaji 500K (soda na maji)

Mziki - Chukua nyumbani kwako, DJ awe mdogo wako huyu itakuwa ni bure
MC - Chukua mwanao sana utampoza hata 100K
Usafiri - Haiwezi kuzidi 200K
Cake - 300K
Mapambo - 1M
Ukumbi tafuta garden simple - 1M

3M+100K+200K+300K+1M+1M = 5.6M
400K ilobaki utafanya kama dharula
You deserve a medal.
Birthday yako lini ?
 
Acha kujistress,jikune mkono unapofika,hii mambo ya kuchanga harusi inapitwa wakati,wengi wamekushauri vizuri,hakuna haja uumie halafu ujikute kwenye madeni.
Madam itabidi aelewe tu.

Nchi nyingi sa hivi story na sherehe ni wewe na watu wa kwenu ,hata kukupa muda tu kuhudhuria ni kipengele juu watu hawana time.

So siku zikikaribia ulichonacho ndio tumia, kila la heri Mkuu.
 
Usd 3000 x 2650 = 7,950,000/= mkuu hela ilikutoka bado
Ungeuliza ilikua mwaka gani kiongozi.
Na hapo ni pesa ambayo nilipanga isizidi hicho kiasi.

Akiamua, anawezakuandaa hata maandazi na chai, ibada ikiisha, watu wanatawanyika kuwahi taarifa ya habari nyumbani.
Kwa hio suti halo lazima ilikua 2010 kurudi nyuma kipindi hicho dola moja ni buku jero hadi buku mia nane
 
Harusi ni mwanzoni wa Septemba, wageni ni 250, lakini 80% bado hawajachanga. Hao 20% waliomaliza wachache ila wengi wamepunguza michango.

Nataka kufanya sherehe ndogo nzuri bila presha kwa bajeti isiyozidi tsh milioni 5-6.

Naomba ushauri wenu wakuu.
Harusi ni nyingi sana kipindi hiki.
Utapata hela wiki 2-4 za mwishoni. Wabongo ni watu wa dakika za mwishooooni!!!!!
 
Back
Top Bottom