Michango ya harusi imekwama, nawezaje kufanya sherehe kwa bajeti ndogo isiyozidi milioni 5?

Michango ya harusi imekwama, nawezaje kufanya sherehe kwa bajeti ndogo isiyozidi milioni 5?

Wewe andaa misosi hapo home, watu waje wale, tafuta MC na DJ wa kawaida, toka kanisani rudi home. Watu wale misosi, watoe zawadi, sepa zako na bi harusi mkale honeymoon, waache wanasherehekea hapo.

Usipoangalia hapo utaishia kwenye madeni.
Nyumba zetu zenyewe uswazi zimebana hata watu 30 kuwahost majanga
 
Bajeti ya harusi ya watu 100- 150
1.Tafuta ukumbi wa gharama nafuu............500,000-1,000,000
2.Tafuta mpishi wa kumlipa kupika, nunua kila kitu yeye apike.........mpishi 300,000...vifaa 900,000.......................1,200,000
3.MC wa 500,000 500,000
4.Video /Picha Music......................................................................................................................................................................................................600,000
5.Vinywaji watu 150(bia 3,soda 2,juice box 1kila meza)......................................................................................................................1,000,000
6.Mineral water..................................................................................................................................................................................................................300,000
7.Usafiri....................................................................................................................................................................................................................................400,000
8.Mengineyo. kadi za mwaliko..................................................................................................................................................................................................................................100,000
9.Keki........................................................................................................................................................................................................................................200,000
10.dharura.............................................................................................................................................................................................................................200,000
11.Mapambo.........................................................................................................................................................................................................................600,000
Jumla ....................................................................................................................................................................................................................................6,100,000

NB:Kama kuna ndugu wenye magari hakikisha mnayatumia kwa ajili ya Maharusi, usafiri mtakaoingia gharama ni wa kuwafuata wakwe.
Bajeti nzuri, hapo bado mapambo na yenyewe yana gharama kubwa sana
 
Sasa mkuu kosa langu kuomba ushauri 😎
Unaomba ushauri wa kijinga, unatakaje kufanya sherehe na pesa huna?? Eti unasema kabisa watu hawajatoa, sherehe Yako wewe jambo la anasa kwanin kama hela huna usiachane nalo? Au ni lazima?

Hiyo hela iliyopo Fanyia jambo la maana achana na huo utoto, kama umeoa mzaramo au mmakonde hapo sasa utajua wewe

Nyie ndio wale mnalazimisha watu wachangie, wasipotoa MNANUNA.

Achana na mambo ya kuridhisha watu kama hela huna achana na huo UTOTO, Kuna safari ndefu sana inakuja mbele Yako hiyo hela ya akiba ya kufanyia sherehe Fanyia mambo yatakayokulipa.
 
Andaa laki ya kukutahiri govi
Laki ya mshenga
Na laki ya sheikh udadu
Tunamaliza mchezo ndani ya dakika tano


1785936001188.png
 
Usikodi ukumbi angalia baa ya kawaida yenye eneo zuri, siku hyo wasiuze nunua vinywaji kwao, wakupe jiko Kodi vyombo na mpishi nunua vya kupika mwenyew mziki wa kwao bar mc tafuta mshkaj wako alicechangamk mwenye experience ya kuongea mbele za watu, Kodi video shuter wa kawaida tu, wageni waalikwa wape kadi ya mwaliko waliotoa 50 kwenda mbele tu, gari omba kwa Wana weka mafuta, ingekua Mimi hyo 6m nakurudishia chenji na upare wangu huu, usije ukajiingiza kwenye madeni mpk ndoa inaisha una madeni makubwa na ukifk ndani mwanamke anaanza kukupandisha sukari tena fanya simple
 
Back
Top Bottom