Michango ya Harusi Single 100,000 na Dabo 150,000, watu wanaumia kimoyomoyo!

Hayo mamichango ya harusi sijui maujinga gani sitoi pesa yangu yaaan !

Msiba, ugonjwa ndo nachangia tu !

Starehe yako uje usumbue watu, mtu eti kisa mmesoma wote, mmepotezana 10+yrs anakuadd kwenye grp anataka mchango..... ujinga huu
Anakupigia , anajichekesha kisha anakuunga kwa group, dah!
 
Unalalamikaje wakati kuchanga ni jambo la hiari

Ukisoma comment unapata picha flani huku JF watu wengi ni masikini sana.

150,000/- sio hela ya kulalamika wala kuja kuitolea maelezo mtandaoni

TUtafute hela
 
Wilayani mikoani, single 30,000/=, double 50,000/=. Harusi za mitaani mchango kuanzia 5,000/=. Plegde kubwa sana haizidi 20,000/=. Kupanga ni kuchagua
 
Tatizo si michango ya harusi.

Tatizo ni unafiki wa Watanzania wengi ambao wanailalamikia michango pembeni, wakati hawawezi kuwaambia wanaochangisha kuwa hatuwezi au hatutaki kuchangia harusi.

Kwanza nchi ya watu wenye matatizo mengi sana yanayohitaji kipaumbele kumalizwa haihitaji harusi kubwa za watu wengi.
 
Ukihoji utaambiwa huna hela ni kapuku, utaambulia matusi ya rejareja. Huu upuuzi wa michango ya harusi ni fasheni tu, huko nyuma haikuwepo na watu waliooa bila kuchangisha watu. Kwa nini unaoa kwa kutegemea mifuko ya watu? Huu ni usumbufu, kwani bila michango ndoa haifunwi? Fanya harusi kwa bajeji yako
 
Kumambuzi, kwenye michango ya harusi kumekuwa na visa, vitimbi na vioja vingi sana *****! Kuna watu wameigeuza ni sehemu ya kupigia kujipatia fedha kufanyia mambo yao mengine. Wanakamati si watu wazuri nao huambulia mgao kama bakshishi yao wakati wanavunja kamati. Kuna dogo alikuwa mtunza fedha huku yeye ndiye muoaji, alipoo michango imenona akaghairi kufunga ndoa kanisani akaenda kufungia bomani kukwepa matumizi makubwa ya fedha. Michango akaigeuza kuwa mtaji wa kuanzisha duka. Kuna bodaboda mmoja yeye kakabidhiwa michango ya harusi yake akaichezea kamari na sasa anapigiwa simu aeleze mpango wa harusi yake hapokei simu. Mwingine aligawa kadi achangiwe na akachangiwa, harusi ilipokaribia akapiga kimya na kudai michango haikufikia lengo kwa bajeti yake, hajarudisha hela za watu, akaanzisha mradi wa kukopesha watu. Anakopesha kwa riba kuanzia buku tano, buku ten, mbau, hamsini, laki na sasa kaanzisha kakikundi chake cha VICOBA
 
Hizi harusi za michango waachiwe matajiri wachangiane kufanya sherehe zao za kifahari. Makapuku kuigaiga utamaduni huu ni vituko na vioja. Cha ajabu ndoa zenyewe hazidumu kwa makapuku huku umewakwangua wenzako visenti vyao. Peleka ndoa kwa mchungaji kanisani/kwa sheikh msikitini hakatai kufunga, rudi homu na mkeo bila mwembwe na nderemo kula ugali wako lala, kesho nenda kwenye mishe zako maisha yaendelee
 
Unalalamikaje wakati kuchanga ni jambo la hiari

Ukisoma comment unapata picha flani huku JF watu wengi ni masikini sana.

150,000/- sio hela ya kulalamika wala kuja kuitolea maelezo mtandaoni

TUtafute hela
usidharau watu, wana hela zao. Michango ni mbwembwe tu na vibe la kula bata, kwani bila michango ndoa haiwezekani kufungwa?
 
usidharau watu, wana hela zao. Michango ni mbwembwe tu na vibe la kula bata, kwani bila michango ndoa haiwezekani kufungwa?
Sijadharau
Watu wanahonga hela bila kufikiri

Watu wanatoa sadaka na zaka

Watu wanatoa bila kutegemea chochote

Ushindwe kutoa 150,000/- kwa jamaa yako siku ya furaha yake

Mimi binafsi huwa natoa kwa mtu ambaye niko karibu nae, kwa sababu una maamuzi ya kutoa au kutokutoa

Si swala ka kelele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…