Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Ukiwa member wa makundi ya Whassap, ya kifamilia, ukoo, mliosoma wote primary, O-Level, High School, Chuo, Kazini, Mtaani Kuna mzigo mzito sana wa michango ya rambirambi inakungoja.
Kila kundi unakuta lina wastani wa watu 20 mpaka 50 na mengine yanafika watu 100. Katika makundi haya, ndani ya miezi miwili unakuta angalau kuna msiba katika kundi mojawapo. Wakati mwingine unakuta zaidi ya makundi 3 kuna msiba na unahitajika mchango!.
Michango ya misiba imekuwa ni kitanzi kizito sana kwa members ila wanaugulia kimyakimya ili wasionekane wabaya.
Na Michango ya Rambirambi kimsingi imetengenezwa in such a way siyo ya hiyari kivile japo hakuna kulazimishwa kwa nguvu bali kuna kulazimishwa kisaikolojia na pia jinsi hiyo michango ilivyo haiko kwa namna ya kuonyesha upendo au kuguswa na msiba, bali imegeuka kuwa kama VIKOBA kuwa Ukichanga basi na wewe utachangiwa!. Usipochanga basi hakuna hata kuitisha rambirambi kwenye kundi ili kila mtu atoe kwa hiyari yake bila kujali policy ya kundi!.
Katika maisha haya ambayo uchumi unazidi kuwa mgumu, Hii michango ya rambirambi katika makundi ya Whassap imegeuka shubiri kwelikweli.