Michango ya Rambirambi za Misiba kwenye makundi ya Whassap imegeuka mzigo kwa wachangiaji

Michango ya Rambirambi za Misiba kwenye makundi ya Whassap imegeuka mzigo kwa wachangiaji

Kama nmna utaratibu wa kusaidiana sio mbaya.

Msiba usikie kwa jirani
 
Waafrika kazi yetu kugawana umaskini. Vimichango michango tu kila kukicha kila mahali. Kupata maendeleo ni ndoto
 
Kama hutaki pesa zako zitumike kwenye misiba ya watu wengine hakikisha akaunti yako iwe fixed na uweke pesa za kutosha na uwaachie ndugu zako maelekezo ukifa watumie vipi.
Sijawahi kuona kutoa rambirambi kama ni mzigo.
labda huwa unatoa jerojero kwenye ile misiba ya mitaani. Usiombe ukutane na misiba yenye bajeti ghali maji utayaita ma
 
Dah! Mleta uzi inaonekana unakereka sana watu wanavyofiwa. Kama hutaki kuchangia hata msiba wewe ni mtu wa hovyo. Pia kulikuwa hakuna haja ya kuleta huu uzi wa kipumbavu hapa... ukiona grupu linakuboa unajitoa tu. Mimi nilijitoa magrupu yote ya watsapp hadi la familia. Ila niliwaambia mkinihitaji nipo mnicheki.
Mkuu,

Mazungumzo haya yana levels nyingi sana na kuchukua tafsiri moja ya chini kabisa hakuyafanyii haki.

Umeweka option ya kama hataki kuchangia bila hata ya kuangalia kama anaweza kuchangia!

Unaelewa kuwa hayo ni mambo mawili tofauti?

Ushawahi kukosa chochote mpaka ikakubidi utembee kwa mguu umbali mrefu kwa sababu huna hata nauli?
 
Mimi ndo maana nilijitoa kote huko.Nikabaki kwenye kundi la familia tu.Binafsi nilijiuliza kuna vitu vingike mfano tuliomaliza wote mashuleni,bila technolojia kutuweka karibu maana yake kila mtu na.hamsini zake.Basi sasa mimi nikaamua kusema niishi kama wale wa zamani kulipokuwa hakuna WhatsApp. Mtu umesoma nae A level mkamaliza kila mtu kivyake.
 
Hivi mtu akikataa kuchangia inakuwaje?
Ingawa nimesoma juu juu, nivyojua hivi vya kijamii husani misiba, siyo lazima, kinachofnyika ni kujiweka karibu na jamii, husani kwa mtu mwenye familia.
Ili pale linapokupata juu ya mwafamilia wako usiwe peke yako, maana usipojihusisha nao hawatahusika.
 
Mimi najua michango ya misiba anayestahili kuchangiwa ni mtu aliyefiwa na baba, mama, mke au mme na mtoto Sasa inakuaje kile au hata mtu akifiwa na mdogoake na shemeji anaitisha michango?
Umasikini
 
Kama hutaki pesa zako zitumike kwenye misiba ya watu wengine hakikisha akaunti yako iwe fixed na uweke pesa za kutosha na uwaachie ndugu zako maelekezo ukifa watumie vipi.
Sijawahi kuona kutoa rambirambi kama ni mzigo.
Haujaelewa hata kidogo mleta mada anaongelea tatizo gani. Hajasema kwamba kutoa rambirambi au kuchangia harusi ni jambo baya. Ila tatizo siku hizi ni kama watu hawana utaratibu mzuri katika kuomba hii michango.

Michango huwa maudhui yake ni iombwe pale wahusika wanaopatwa na majanga wanakuwa hawana hali nzuri.

Kwa mfano harusi, wewe una milioni zako 30 au 20, michango unaomba ili iweje sasa?

Au msiba unapotokea ndugu kwanza mnatakiwa kusanyane na kushirikishana kuhusu swala la hiyo shughuli ya msiba muone mnaianzaje hadi kumaliza. Misiba huwa haitaki gharama kubwa sana kuimaliza maana sio sherehe ile kusema watu wale wakasaza.

Shida iliyopo ni kuna wale vimbelembele kwenye magroup haya unakuta ni group la shule au chuo ambao mlisoma pamoja, wanafosi kuwe na utaratibu wa kuchanga pesa za rambirambi hata pale muhusika hakuwa na shida ya kuchangiwa. Sasa watu wanaweka ni kama Deni yaani deni la kulipishwa kabisa hadi unamind.

Tukumbuke changamoto zipo nyingi sana, sasa unakuta kila group mara huyu anauguza mtoto tumchangie ya kumpa pole, kule yule kafiwa na nani tumchangie ya kumpa pole, huku hawa wanaoa, kule yule amejifungua mtoto, ni michango kila kona. Hizo hela tunaokota kwan aisee?
 
Vipi kuhusu michango ya harusi na sherehe zingine za anasa na ufahari ipo kwenye makundi hayo? Afadhali huko kwenye whatsaap, hapa mtaani balozi kachosha kukusanya hela za rambirambi kila mara. Hata kama haupo umesafiri ukirudi tu atakuambia kuna misiba mitano ilitokea mtaani unatakiwa utoe rambirambi kila msiba ni elfu moja na kuendelea ukimpa tu hapeleki kulikotokea msiba anachikichia mwenyewe. Mbaya zaidi kumbe mchango ni mia tano yeye huongeza kwa hila tu anakula cha juu. Wakati mwingine huongeza idadi ya misiba ambayo haikutokea anajua hutahoji ni wapi ulipo msiba na hutafuatilia kwa kuwa mjini kuna watu wengi na huwajui wote zaidi ya majirani tu. Cha ajabu ni kama unalazimika uchangie msiba usiokugusa na humjui kabisa marehemu wala wafiwa
duh hii ya balozi kupitisha bakuli la rambirambi ni mpya. bila shaka itakuwa ni maporini ndanindani huko au uswazini labda maana kwa town hlf ushuani mbona ngumu hii.

mimi michango ya alumni nilishaikataa kitambo maana watu mpo sehem mbalimbali ni ngumu hata kupata uhakika wa hiyo misiba yenyewe kama ni ya kweli au ni sanaa hlf unakuta mpo wengi mno unaweza kuta unachanga kila siku.

wkt flani kuna jamaa alinyooka (alikufa) kitaani kwetu sasa yeye hakuwepo kwenye magrupu ya kuchangishana ya pale mtaani.
uzuri jamaa kumbe alikuwa ameajiliwa kwaiyo mwajili wake akaendesha shoo mwanzo mambo yote sijui misosi usafiri ikaenda sawa mwanzo mwisho adi msiba ukaisha bila kwere yyote yaani.
 
Kuweka list ya wasiotoa michango, kuishi maisha ya kutegemea michango, ni kuendekeza umasikini.

Kila mtu anatakiwa kuwa na bima ya maisha si tu kuweza kukidhi gharama za mazishi, bali pia hata kuacha kiasi fulani kwa familia.

Na hata vikundi vinavyochangishana vinaweza kununua bima za maisha za vikundi ambazo zitakuwa na gharama rahisi zaidi, zinazotabirika zaidi na zenye ufanisi zaidi.

Tunapenda mifumo ya kijima tu ya kuchangishana kwa tukio hata kama kuna mifumo mipya yenye ufanisi zaidi.
BIMA nyingi za kibongo ni ubabaishaji. Unaweza jiunga ukapatwa Jambo usilipwe instantly ikawa tabu tupu
 
duh hii ya balozi kupitisha bakuli la rambirambi ni mpya. bila shaka itakuwa ni maporini ndanindani huko au uswazini labda maana kwa town hlf ushuani mbona ngumu hii.

mimi michango ya alumni nilishaikataa kitambo maana watu mpo sehem mbalimbali ni ngumu hata kupata uhakika wa hiyo misiba yenyewe kama ni ya kweli au ni sanaa hlf unakuta mpo wengi mno unaweza kuta unachanga kila siku.

wkt flani kuna jamaa alinyooka (alikufa) kitaani kwetu sasa yeye hakuwepo kwenye magrupu ya kuchangishana ya pale mtaani.
uzuri jamaa kumbe alikuwa ameajiliwa kwaiyo mwajili wake akaendesha shoo mwanzo mambo yote sijui misosi usafiri ikaenda sawa mwanzo mwisho adi msiba ukaisha bila kwere yyote yaani.
ni mjini mitaa ya uswahilini, balozi anatembea na daftari nyumba kwa nyumba anakusanya rambirambi. Mchango ni bukubuku, akiona unachekacheka anakuambia mchango umepanda sio buku ni buku mbili utoe, unatoa anakuandika jina, anakula cha juu buku akijua hutahoji
 
Haya magrupu ya shule/chuo, familia, kazini yanaleta utajiri? Kama hayaleti utajiri basi ni kero tu na usumbufu wa kuombana hela. Kama lengo lake ni kuombana hela ijulikane ili mtu ajue akijiunga ajiandae kutoa hela atakapoombwa
 
Hivi mtu akikataa kuchangia inakuwaje?
Kuna group nilikuwepo hadi wanaslogani chuna uchuniwe😂. Jamaa sijui wanamradi, rambirambi ina hamasishwa hatari. Mwisho wa siku wanakutoa kwenye group.

Mpo watu karibia 200, misiba kila mwezi imo tena hamjuani kbs na members wengine.

Kuna group tuliamua hakuna kuweka mambo ya michango, ila tutapeana taarifa tu za matukio. Ukiona poa unamchek mshikaji inbox maisha yanaendelea.
 
Mimi huwa nachangia lakini nataka kuweza kuishi bila kuchangiwa.
Na sipendi harusi wala misiba inayonihusu kufanyiwa some big production.

Ila, jambo la ajabu, ukiwaambia watu hutaki mchango napo unaweza kuwakwaza.

Kuna jamaa mmoja alikuwa anaoa, akawaambia watu kuwa hatahitaji mchango wa mtu, kama kuna mtu anaona haja ya kumchangia atume mchango wake kwenye kijiji kimoja cha uMasaini huko (hata si kwao, alichagua kijiji tu) ambacho kinahitaji msaada kwenye miradi ya maji.

Alifikiri anawaondolea watu mzigo wa kuchangia harusi.

Ila kuna watu walikuwa wanamsema kwamba huyu bwana anajidai sana, anajiona anaweza kufanya harusi yake bila kuhitaji mchango wa mtu.
Shida kubwa sana ya watanzania hii. Angewachangisha tu kisa hizo hela siku ya harusi akawaambia tu tena mbele ya kamati ya hiko kijiji 😂😂
 
Kuna group lilianzishwa miaka ya 2017 la members wa hapa JF lilikuwa na members 75 kama sijasahau, ila kila siku huku kwenye group kila member kafiwa anahitaji mchango, sasa nani atamchangia mwingine? Baadae tukaamua kuweka utaratibu wa kuchanga 10k kila mwezi kuwe na shida kusiwe na shida. Baada ya miezi kama mitano admin akadelete group lile la whatsapp na hela zetu kamega. Ukija huku jukwaani JF anajifanya great thinker sana. Baada ya kuopoa kimwana humu kapotea jukwaani na iD kaitelekeza, kumbe alienda unganishwa kwenye gridi ya taifa bila kujijua. Saivi anashinda huko X ana kazi ya kuretweet maneno ya biblia. Hela za rambi rambi sio za kuzila. 😏
😀
 
Kuweka list ya wasiotoa michango, kuishi maisha ya kutegemea michango, ni kuendekeza umasikini.

Kila mtu anatakiwa kuwa na bima ya maisha si tu kuweza kukidhi gharama za mazishi, bali pia hata kuacha kiasi fulani kwa familia.

Na hata vikundi vinavyochangishana vinaweza kununua bima za maisha za vikundi ambazo zitakuwa na gharama rahisi zaidi, zinazotabirika zaidi na zenye ufanisi zaidi.

Tunapenda mifumo ya kijima tu ya kuchangishana kwa tukio hata kama kuna mifumo mipya yenye ufanisi zaidi.
[emoji16][emoji16][emoji16]watu hawataki kuendana na nyakati
 
Kuna group nilikuwepo hadi wanaslogani chuna uchuniwe[emoji23]. Jamaa sijui wanamradi, rambirambi ina hamasishwa hatari. Mwisho wa siku wanakutoa kwenye group.

Mpo watu karibia 200, misiba kila mwezi imo tena hamjuani kbs na members wengine.

Kuna group tuliamua hakuna kuweka mambo ya michango, ila tutapeana taarifa tu za matukio. Ukiona poa unamchek mshikaji inbox maisha yanaendelea.
[emoji1]
 
Back
Top Bottom