Michango ya Rambirambi za Misiba kwenye makundi ya Whassap imegeuka mzigo kwa wachangiaji

Michango ya Rambirambi za Misiba kwenye makundi ya Whassap imegeuka mzigo kwa wachangiaji

Ukiwa member wa makundi ya Whassap, ya kifamilia, ukoo, mliosoma wote primary, O-Level, High School, Chuo, Kazini, Mtaani Kuna mzigo mzito sana wa michango ya rambirambi inakungoja.

Kila kundi unakuta lina wastani wa watu 20 mpaka 50 na mengine yanafika watu 100. Katika makundi haya, ndani ya miezi miwili unakuta angalau kuna msiba katika kundi mojawapo. Wakati mwingine unakuta zaidi ya makundi 3 kuna msiba na unahitajika mchango!.

Michango ya misiba imekuwa ni kitanzi kizito sana kwa members ila wanaugulia kimyakimya ili wasionekane wabaya.

Na Michango ya Rambirambi kimsingi imetengenezwa in such a way siyo ya hiyari kivile japo haluna kulazimishwa kwa nguvu bali kuna kulazimishwa kisaikolojia na pia jinsi hiyo michango ilivyo haiko kwa namna ya kuonyesha upendo au kuguswa na msiba, bali imegeuka kuwa kama VIKOBA kuwa Ukichanga basi na wewe utachangiwa!. Usipochanga basi hakuna hata kuitisha rambirambi kwenye kundi ili kila mtu atoe kwa hiyari yake bila kujali policy ya kundi!.

Katika maisha haya ambayo uchumi unazidi kuwa mgumu, Hii michango ya rambirambi katika makundi ya Whassap imegeuka shubiri kwelikweli.
Kutobao maisha Afrika ni kazi sana,tumeletewa teknolojia badala ya kuendelea tunazidi kudidimizana,na hapo bado michango ya harusi,bado kuna wengine wanakwama kushindwa kulipia ada za shule english medium wanaleta kwenye magroup...
 
Hakuna mtu anaomba kufiwa mkuu, mi nilidhani sherehe.

Na mambo ya msiba wanaoguswa ni wengi na wengine wanakua apeche alolo, hawana kitu.
Tatizo lako/lenu ni kua kuna kakiasi fulani huwa mkitoa ndo mnajihisi mmechangia.
Kuna baadhi ya groups kiwango cha chini ni 10k, wengine 5k. Wengi ni jinsi utavyoguswa.
Je hizo groups zenu mna kiwango maalumu kwenye mambo ya majanga??
 
Ndo maana Serikali imekuja na majibu yote.
Vikundi,magroup vyama visajilliwe na vilipie.

Ujanja ujanja utaisha Kwa Maadmin kuderete magroup hayo.
Changamoto ya maokoto ndo shida.

Hela yako ndo itakayokukutanisha na watu,na sio roho nzuri.

Chochote kile kinalenga pesa.
 
Worst case scenario, mtu akipata msiba kisha akachangisha milioni milioni ktk makundi yake matano, ana milioni zake TANO. akishakunja mshiko wake anasepa, anajitoa kabisa ktk makundi wasike wakamsinga pindi akiamua kula buyu huko mbeleni.

Kwenye makundi mengine mwanzoni nakubaliana msiba uhusu mke, mume,baba, mama na watoto. Baadae wanatokea wajuaji wanasisistiza hata mama mkwe na baba mkwe wawemo. Yaani ngoma inazidi kuwa ngumu

Wengine wanafake misiba ya mama mkwe, au baba mkwe ili wapate michango
 
Back
Top Bottom