Michango ya Rambirambi za Misiba kwenye makundi ya Whassap imegeuka mzigo kwa wachangiaji

Michango ya Rambirambi za Misiba kwenye makundi ya Whassap imegeuka mzigo kwa wachangiaji

Kuna group lilianzishwa miaka ya 2017 la members wa hapa JF lilikuwa na members 75 kama sijasahau, ila kila siku huku kwenye group kila member kafiwa anahitaji mchango, sasa nani atamchangia mwingine? Baadae tukaamua kuweka utaratibu wa kuchanga 10k kila mwezi kuwe na shida kusiwe na shida. Baada ya miezi kama mitano admin akadelete group lile la whatsapp na hela zetu kamega. Ukija huku jukwaani JF anajifanya great thinker sana. Baada ya kuopoa kimwana humu kapotea jukwaani na iD kaitelekeza, kumbe alienda unganishwa kwenye gridi ya taifa bila kujijua. Saivi anashinda huko X ana kazi ya kuretweet maneno ya biblia. Hela za rambi rambi sio za kuzila. 😏
Aysee
 
Ukiwa member wa makundi ya Whassap, ya kifamilia, ukoo, mliosoma wote primary, O-Level, High School, Chuo, Kazini, Mtaani Kuna mzigo mzito sana wa michango ya rambirambi inakungoja.

Kila kundi unakuta lina wastani wa watu 20 mpaka 50 na mengine yanafika watu 100. Katika makundi haya, ndani ya miezi miwili unakuta angalau kuna msiba katika kundi mojawapo. Wakati mwingine unakuta zaidi ya makundi 3 kuna msiba na unahitajika mchango!.

Michango ya misiba imekuwa ni kitanzi kizito sana kwa members ila wanaugulia kimyakimya ili wasionekane wabaya.

Na Michango ya Rambirambi kimsingi imetengenezwa in such a way siyo ya hiyari kivile japo haluna kulazimishwa kwa nguvu bali kuna kulazimishwa kisaikolojia na pia jinsi hiyo michango ilivyo haiko kwa namna ya kuonyesha upendo au kuguswa na msiba, bali imegeuka kuwa kama VIKOBA kuwa Ukichanga basi na wewe utachangiwa!. Usipochanga basi hakuna hata kuitisha rambirambi kwenye kundi ili kila mtu atoe kwa hiyari yake bila kujali policy ya kundi!.

Katika maisha haya ambayo uchumi unazidi kuwa mgumu, Hii michango ya rambirambi katika makundi ya Whassap imegeuka shubiri kwelikweli.
Tumiaa kitochii acha kulalamika wakija na huko ukasafishe nyotaaa
 
Bro,suala la msiba siyo la kuzungumza kwamba shida ni uchumi umekuwa mgumu.

Jiulize yule aliyefiwa anajisikiaje maana kibongo bongo unakuta wote wewe na yeye ni unga unga mwana siku ziende na umekuja msiba juu unadhani kumpa 5K yako kama rambirambi kutazidi kukufanya maskini?kama tumefikia hadi kuhoji ishu za rambirambi na kabisa tupo hapa tunajadili basi mentality tutakuwa tuna shida kubwa mahali.
Ndiyo maana nimesema ni kwa ajili ya kumfariji mfiwa, maana mleta mada amasema Rambirambi za misiba zimekuwa mzigo.
 
Ukiwa member wa makundi ya Whassap, ya kifamilia, ukoo, mliosoma wote primary, O-Level, High School, Chuo, Kazini, Mtaani Kuna mzigo mzito sana wa michango ya rambirambi inakungoja.

Kila kundi unakuta lina wastani wa watu 20 mpaka 50 na mengine yanafika watu 100. Katika makundi haya, ndani ya miezi miwili unakuta angalau kuna msiba katika kundi mojawapo. Wakati mwingine unakuta zaidi ya makundi 3 kuna msiba na unahitajika mchango!.

Michango ya misiba imekuwa ni kitanzi kizito sana kwa members ila wanaugulia kimyakimya ili wasionekane wabaya.

Na Michango ya Rambirambi kimsingi imetengenezwa in such a way siyo ya hiyari kivile japo haluna kulazimishwa kwa nguvu bali kuna kulazimishwa kisaikolojia na pia jinsi hiyo michango ilivyo haiko kwa namna ya kuonyesha upendo au kuguswa na msiba, bali imegeuka kuwa kama VIKOBA kuwa Ukichanga basi na wewe utachangiwa!. Usipochanga basi hakuna hata kuitisha rambirambi kwenye kundi ili kila mtu atoe kwa hiyari yake bila kujali policy ya kundi!.

Katika maisha haya ambayo uchumi unazidi kuwa mgumu, Hii michango ya rambirambi katika makundi ya Whassap imegeuka shubiri kwelikweli.
Kwani kuna mtu analazimishwa?
 
Vipi kuhusu michango ya harusi na sherehe zingine za anasa na ufahari ipo kwenye makundi hayo? Afadhali huko kwenye whatsaap, hapa mtaani balozi kachosha kukusanya hela za rambirambi kila mara. Hata kama haupo umesafiri ukirudi tu atakuambia kuna misiba mitano ilitokea mtaani unatakiwa utoe rambirambi kila msiba ni elfu moja na kuendelea ukimpa tu hapeleki kulikotokea msiba anachikichia mwenyewe. Mbaya zaidi kumbe mchango ni mia tano yeye huongeza kwa hila tu anakula cha juu. Wakati mwingine huongeza idadi ya misiba ambayo haikutokea anajua hutahoji ni wapi ulipo msiba na hutafuatilia kwa kuwa mjini kuna watu wengi na huwajui wote zaidi ya majirani tu. Cha ajabu ni kama unalazimika uchangie msiba usiokugusa na humjui kabisa marehemu wala wafiwa
Kama ni kweli basi tumefikia hali mbaya sana kama nchi katika hili.
 
Nadhani kila mtu afanye anachoona kinamfaa,as long as hakuna anayelazimishwa kutoa/changa wewe ukiona acha lipite wenye kuguswa watoe wewe baki kufanya yale unaona yanakufaa ndani ya kundi.

Kuna jamaa yangu nilisoma nae primary alimuuguza baba yake almost 9 years alipofariki kwenye group la shule yetu ilichangwa karibia 1.5mill kusaidia msiba na jamaa anasema ilimtosha kumzika baba yake so haya mambo ya misiba kama halijakukuta huwezi kuona umuhimu wa kumchangia mwenzako Tsh 5,000/=
Hata asingechangaiwa baba yake angezikiwa tu hata na Halmashauri ya wilaya, mji au Manisipaa.
 
Hatachangiwa na yeye akifa au akifiwa.
Mimi huwa nachangia lakini nataka kuweza kuishi bila kuchangiwa.
Na sipendi harusi wala misiba inayonihusu kufanyiwa some big production.

Ila, jambo la ajabu, ukiwaambia watu hutaki mchango napo unaweza kuwakwaza.

Kuna jamaa mmoja alikuwa anaoa, akawaambia watu kuwa hatahitaji mchango wa mtu, kama kuna mtu anaona haja ya kumchangia atume mchango wake kwenye kijiji kimoja cha uMasaini huko (hata si kwao, alichagua kijiji tu) ambacho kinahitaji msaada kwenye miradi ya maji.

Alifikiri anawaondolea watu mzigo wa kuchangia harusi.

Ila kuna watu walikuwa wanamsema kwamba huyu bwana anajidai sana, anajiona anaweza kufanya harusi yake bila kuhitaji mchango wa mtu.
 
Back
Top Bottom