min -me
JF-Expert Member
- Jul 20, 2022
- 23,322
- 64,738
Wadai na yeye hato changiwa akifa au akifiwa 😊.Hivi mtu akikataa kuchangia inakuwaje?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wadai na yeye hato changiwa akifa au akifiwa 😊.Hivi mtu akikataa kuchangia inakuwaje?
duu hahahaKuna group lilianzishwa miaka ya 2017 la members wa hapa JF lilikuwa na members 75 kama sijasahau, ila kila siku huku kwenye group kila member kafiwa anahitaji mchango, sasa nani atamchangia mwingine? Baadae tukaamua kuweka utaratibu wa kuchanga 10k kila mwezi kuwe na shida kusiwe na shida. Baada ya miezi kama mitano admin akadelete group lile la whatsapp na hela zetu kamega. Ukija huku jukwaani JF anajifanya great thinker sana. Baada ya kuopoa kimwana humu kapotea jukwaani na iD kaitelekeza, kumbe alienda unganishwa kwenye gridi ya taifa bila kujijua. Saivi anashinda huko X ana kazi ya kuretweet maneno ya biblia. Hela za rambi rambi sio za kuzila. 😏
kama kuna mikopo kausha damu mpaka inajadiliwa bungeni na michango umiza nayo ipo, hatusemi tu.Kama ni kweli basi tumefikia hali mbaya sana kama nchi katika hili.
Achana na magroup ya Primary na sekondari. Walau baki na la kazini, ikiwezekana na la Chuo. Pia baki na la familia. Niliweka block hakuna mtu kuniadd kijinga jinga.
Uko really sana mkuu.Unapata faida gani kua member kwenye hayo magroup?
Kwani hua mnalazimishwa kujiunga kwenye hayo magroup?
Mkuu,ishi maisha yako,usiishi kwa kuogopa watu kua eti watanionajee,
Fanya ambacho kitakupa peace kwenye nafsi yako badala ya kujitesa,
Life is too short,enjoy it.
Setting-Groups-My contacts except-select all.Unaweka je block usiaddiwe.
Nani huyo?? 😡Kuna group lilianzishwa miaka ya 2017 la members wa hapa JF lilikuwa na members 75 kama sijasahau, ila kila siku huku kwenye group kila member kafiwa anahitaji mchango, sasa nani atamchangia mwingine? Baadae tukaamua kuweka utaratibu wa kuchanga 10k kila mwezi kuwe na shida kusiwe na shida. Baada ya miezi kama mitano admin akadelete group lile la whatsapp na hela zetu kamega. Ukija huku jukwaani JF anajifanya great thinker sana. Baada ya kuopoa kimwana humu kapotea jukwaani na iD kaitelekeza, kumbe alienda unganishwa kwenye gridi ya taifa bila kujijua. Saivi anashinda huko X ana kazi ya kuretweet maneno ya biblia. Hela za rambi rambi sio za kuzila. 😏
Jitoe tu kwenye hayo makundi acha kutuchosha. Kwani imelazimishwa kuingia?Ukiwa member wa makundi ya Whassap, ya kifamilia, ukoo, mliosoma wote primary, O-Level, High School, Chuo, Kazini, Mtaani Kuna mzigo mzito sana wa michango ya rambirambi inakungoja.
Kila kundi unakuta lina wastani wa watu 20 mpaka 50 na mengine yanafika watu 100. Katika makundi haya, ndani ya miezi miwili unakuta angalau kuna msiba katika kundi mojawapo. Wakati mwingine unakuta zaidi ya makundi 3 kuna msiba na unahitajika mchango!.
Michango ya misiba imekuwa ni kitanzi kizito sana kwa members ila wanaugulia kimyakimya ili wasionekane wabaya.
Na Michango ya Rambirambi kimsingi imetengenezwa in such a way siyo ya hiyari kivile japo haluna kulazimishwa kwa nguvu bali kuna kulazimishwa kisaikolojia na pia jinsi hiyo michango ilivyo haiko kwa namna ya kuonyesha upendo au kuguswa na msiba, bali imegeuka kuwa kama VIKOBA kuwa Ukichanga basi na wewe utachangiwa!. Usipochanga basi hakuna hata kuitisha rambirambi kwenye kundi ili kila mtu atoe kwa hiyari yake bila kujali policy ya kundi!.
Katika maisha haya ambayo uchumi unazidi kuwa mgumu, Hii michango ya rambirambi katika makundi ya Whassap imegeuka shubiri kwelikweli.
Kutoa salamu nilikuwa mara chache labda mara moja kwa mwezi, Nadhani ilikuwa ni kuhusu michango, maana walikuwa wanawazodoa wote ambao hawakutoa na nilikuwa naona jina langu kwenye list ya wasiotoa michango lakini napiga kimya, ikaeenda mpaka wakanichoka na kunitema.Wamekutema kwa sababu huchangii hela au huchangii hata salamu?
Kuweka list ya wasiotoa michango, kuishi maisha ya kutegemea michango, ni kuendekeza umasikini.Kutoa salamu nilikuwa mara chache labda mara moja kwa mwezi, Nadhani ilikuwa ni kuhusu michango, maana walikuwa wanawazodoa wote ambao hawakutoa na nilikuwa naona jina langu kwenye list ya wasiotoa michango lakini napiga kimya, ikaeenda mpaka wakanichoka na kunitema.
Nilikuwa natoa michango kama naona ni sahihi kutoa kama kufiwa mtoto au mzazi, sasa ikawa hata ya hospitali na ya harusi nikaona hii sasa ni kuchoshana
Kuna group lilianzishwa miaka ya 2017 la members wa hapa JF lilikuwa na members 75 kama sijasahau, ila kila siku huku kwenye group kila member kafiwa anahitaji mchango, sasa nani atamchangia mwingine? Baadae tukaamua kuweka utaratibu wa kuchanga 10k kila mwezi kuwe na shida kusiwe na shida. Baada ya miezi kama mitano admin akadelete group lile la whatsapp na hela zetu kamega. Ukija huku jukwaani JF anajifanya great thinker sana. Baada ya kuopoa kimwana humu kapotea jukwaani na iD kaitelekeza, kumbe alienda unganishwa kwenye gridi ya taifa bila kujijua. Saivi anashinda huko X ana kazi ya kuretweet maneno ya biblia. Hela za rambi rambi sio za kuzila. [emoji57]
Wabongo wameshazoea kupewa msaada na kuombaombaKuweka list ya wasiotoa michango, kuishi maisha ya kutegemea michango, ni kuendekeza umasikini.
Kila mtu anatakiwa kuwa na bima ya maisha si tu kuweza kukidhi gharama za mazishi, bali pia hata kuacha kiasi fulani kwa familia.
Na hata vikundi vinavyochangishana vinaweza kununua bima za maisha za vikundi ambazo zitakuwa na gharama rahisi zaidi, zinazotabirika zaidi na zenye ufanisi zaidi.
Tunapenda mifumo ya kijima tu ya kuchangishana kwa tukio hata kama kuna mifumo mipya yenye ufanisi zaidi.