Michango ya Rambirambi za Misiba kwenye makundi ya Whassap imegeuka mzigo kwa wachangiaji

Aysee
 
Tumiaa kitochii acha kulalamika wakija na huko ukasafishe nyotaaa
 
Ndiyo maana nimesema ni kwa ajili ya kumfariji mfiwa, maana mleta mada amasema Rambirambi za misiba zimekuwa mzigo.
 
Kwani kuna mtu analazimishwa?
 
Kama ni kweli basi tumefikia hali mbaya sana kama nchi katika hili.
 
Hata asingechangaiwa baba yake angezikiwa tu hata na Halmashauri ya wilaya, mji au Manisipaa.
 
Hatachangiwa na yeye akifa au akifiwa.
Mimi huwa nachangia lakini nataka kuweza kuishi bila kuchangiwa.
Na sipendi harusi wala misiba inayonihusu kufanyiwa some big production.

Ila, jambo la ajabu, ukiwaambia watu hutaki mchango napo unaweza kuwakwaza.

Kuna jamaa mmoja alikuwa anaoa, akawaambia watu kuwa hatahitaji mchango wa mtu, kama kuna mtu anaona haja ya kumchangia atume mchango wake kwenye kijiji kimoja cha uMasaini huko (hata si kwao, alichagua kijiji tu) ambacho kinahitaji msaada kwenye miradi ya maji.

Alifikiri anawaondolea watu mzigo wa kuchangia harusi.

Ila kuna watu walikuwa wanamsema kwamba huyu bwana anajidai sana, anajiona anaweza kufanya harusi yake bila kuhitaji mchango wa mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…