Michango ya Rambirambi za Misiba kwenye makundi ya Whassap imegeuka mzigo kwa wachangiaji

Mimi binafsi Sina magroup na wala Sina mpango wa kua na magroup sijui ya tuliosoma nao, mara nyingi huwa ni umbea tu unaendelea humo, watu niliosoma nao primary mpaka chuo na tukawa marafiki Basi tunawasiliana binafsi,sio mpaka tukutane kwenye group, Nina group Moja tu la ofisini ambako ni lazima kujoin, Hilo ndo hua nachangia hata misiba na harusi maana ni watu ambao nipo nao Kila siku na Ninajua nikipatwa na jambo watanibeba.
Lakini mtu ambae tangu tuachane shule hajawahi hata kunijulia hali, halafu from nowhere naombwa mchango wa harusi kwangu ni big NO.(bora hata rambirambi nitachangia lakini sio harusi)
Kama hayo magroup yanatija kwenye maisha yako endelea nayo lakini Kama unaona kabisa mzani haubalance yaani faida yake ni ndogo Sana ukilinganisha na stress unayopata kwasababu yake achana nayo,Baki na magroup machache yenye tija.
 
d
duu hahaha
 
Nani huyo?? 😡
 
Jitoe tu kwenye hayo makundi acha kutuchosha. Kwani imelazimishwa kuingia?

Kuna haja gani kuingia kwenye Group ambayo hamuwezi kuchangia kwenye raha na shida.
 
Wamekutema kwa sababu huchangii hela au huchangii hata salamu?
Kutoa salamu nilikuwa mara chache labda mara moja kwa mwezi, Nadhani ilikuwa ni kuhusu michango, maana walikuwa wanawazodoa wote ambao hawakutoa na nilikuwa naona jina langu kwenye list ya wasiotoa michango lakini napiga kimya, ikaeenda mpaka wakanichoka na kunitema.
Nilikuwa natoa michango kama naona ni sahihi kutoa kama kufiwa mtoto au mzazi, sasa ikawa hata ya hospitali na ya harusi nikaona hii sasa ni kuchoshana
 
Kuweka list ya wasiotoa michango, kuishi maisha ya kutegemea michango, ni kuendekeza umasikini.

Kila mtu anatakiwa kuwa na bima ya maisha si tu kuweza kukidhi gharama za mazishi, bali pia hata kuacha kiasi fulani kwa familia.

Na hata vikundi vinavyochangishana vinaweza kununua bima za maisha za vikundi ambazo zitakuwa na gharama rahisi zaidi, zinazotabirika zaidi na zenye ufanisi zaidi.

Tunapenda mifumo ya kijima tu ya kuchangishana kwa tukio hata kama kuna mifumo mipya yenye ufanisi zaidi.
 
Kule X anajiita nani?

 
Wabongo wameshazoea kupewa msaada na kuombaomba
Hii nchi wakiona mtu anaendesha maisha yake mwenyewe wanaanza uchuro wa anajifanya anaringa subiri apate shida tutamuona anakuja kuomba msaada, huyo wanaemuogelea hivi unakuta kajitosheleza na wala hawezi hata siku moja kuomba asaidiwe.
Huu ujamaa ulitulemaza sana, sasa mtu ukishaamua kuwa na familia, inakuwaje siku una mgonjwa hospital unategemea eti washkaji ndio wakuuguzie mtoto wako au mke wako, wakati anaoa na kuzaa hakujua kuwa hii kazi yake kuwahudumia.
 
Dah! Mleta uzi inaonekana unakereka sana watu wanavyofiwa. Kama hutaki kuchangia hata msiba wewe ni mtu wa hovyo. Pia kulikuwa hakuna haja ya kuleta huu uzi wa kipumbavu hapa... ukiona grupu linakuboa unajitoa tu. Mimi nilijitoa magrupu yote ya watsapp hadi la familia. Ila niliwaambia mkinihitaji nipo mnicheki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…