Michango ya Rambirambi za Misiba kwenye makundi ya Whassap imegeuka mzigo kwa wachangiaji

Kutobao maisha Afrika ni kazi sana,tumeletewa teknolojia badala ya kuendelea tunazidi kudidimizana,na hapo bado michango ya harusi,bado kuna wengine wanakwama kushindwa kulipia ada za shule english medium wanaleta kwenye magroup...
 
Hakuna mtu anaomba kufiwa mkuu, mi nilidhani sherehe.

Na mambo ya msiba wanaoguswa ni wengi na wengine wanakua apeche alolo, hawana kitu.
Tatizo lako/lenu ni kua kuna kakiasi fulani huwa mkitoa ndo mnajihisi mmechangia.
Kuna baadhi ya groups kiwango cha chini ni 10k, wengine 5k. Wengi ni jinsi utavyoguswa.
Je hizo groups zenu mna kiwango maalumu kwenye mambo ya majanga??
 
Ndo maana Serikali imekuja na majibu yote.
Vikundi,magroup vyama visajilliwe na vilipie.

Ujanja ujanja utaisha Kwa Maadmin kuderete magroup hayo.
Changamoto ya maokoto ndo shida.

Hela yako ndo itakayokukutanisha na watu,na sio roho nzuri.

Chochote kile kinalenga pesa.
 
Worst case scenario, mtu akipata msiba kisha akachangisha milioni milioni ktk makundi yake matano, ana milioni zake TANO. akishakunja mshiko wake anasepa, anajitoa kabisa ktk makundi wasike wakamsinga pindi akiamua kula buyu huko mbeleni.

Kwenye makundi mengine mwanzoni nakubaliana msiba uhusu mke, mume,baba, mama na watoto. Baadae wanatokea wajuaji wanasisistiza hata mama mkwe na baba mkwe wawemo. Yaani ngoma inazidi kuwa ngumu

Wengine wanafake misiba ya mama mkwe, au baba mkwe ili wapate michango
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…