Ulivyo sema Much know mithili ya Gwajima nimeona niweke na mdhamini Gwaji boy.Nikishuka wanastuka kama wamemwona masih/
marapa wenu vipusa kwenye game wanaanguka, course hawana plan b/
Fungua roho upokee flow za uzima, mc wengi much know mithili ya Gwajima/
kutwa wanahit na kiki wakati pikipiki za kuazima/
Ni kama hujui unapokwenda kwaiyo ulipo utaona kama umefikaKwanza nawapa salamu, nazingatia itifaki/
Nadhani Mvumbo mnamfahamu, kwenye mistari mimi ndiye chaki/
Naandika zaidi ya kalamu, mwana Hip hop kindaki ndaki/
Ma mc's wa Jamii Forum, karibuni nyuma msibaki/
Leo mitandaoni ukisema usome, habari zimejaa ukakasi/
Huku Kiba anasema UNIKOME, huku Idriss akaripoti Polisi/
Huku Kigwa kavunja ngome, Le M'bebez kapiga pasi/
Haya yasikufanye ulale ukorome, pambana watoto wasile nyasi.
Hii nchi bado inaujinga mwingi, vitu bei juu afu eti mama anaupiga mwingi.../Viongozi tuliowachagua wanatutesa nakututia doa, wanakomba pesa hawaachi hata nyoya/
Nchi inaendeshwa kiboya, bungeni wamejaa mabogas/ hawana hoja wala umoja mda wote wamepoa/
Polisi wanatufilisi badala ya kulinda nchi/
Wanyonge wanazidi kunyongeka, biashara za madawa na umalaya zinadidi kuongezeka/